Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo
(Mb) katika picha ya pamoja na wataalam wa shirika la Plan International wakati
wa warsha ya tathimini na mipango.
Naye Meneja Ufadhili wa Plan
International Nicodemus Gachu alisema kuwa mpaka sasa Shirika lina watoto
rafiki elfu 30 ambao wanapata huduma mbalimbali kutoka Plan International.
Gachu alisema kwa sasa Plan
Internationa imekuja na mpango wa kutoa Bima ya Afya iliyoboreshwa kwa watoto
rafiki wa shirika hilo, ambao unatarajia kuzinduliwa hivi karibuni kwa
kuwakabidhi watoto hao Bima za Afya katika kila Mkoa ambako wana watoto rafiki.
Gachu alitumia fursa hiyo
kuanisha kazi ambazo Shirika limezifanya kuwa ni pamoja na kujenga miundombinu
ya Afya katika baadhi ya hospital na vituo vya Afya kama Buguruni, ujenzi wa
miundombinu ya Elimu, ujenzi wa miundombinu
ya Maji, kuwawezesha vijana kiuchumi na kuwajengea uwezo watoto kuzifahamu hazi
zao.
Naye Neema Moris ambaye ni
Meneja ya Uniti ya Kisarawe amesema kupitia warsha hiyo ya siku nne wameweza
kujitathmini utendaji kazi wa shirika, namna ya kutatua changamoto wanazokabiliana
nazo katika maeneo ya kazi na kuweka malengo ya utekelezaji wa kazi za Shirika.
Ikumbukwe kuwa Waziri Jafo
alianzia kazi katika Shirika la Plan Internationa akiwa kama Meneja wa Uniti ya
Kisarawe kabla ya kuwa Mbunge wa Kisarawe kisha kuteuliwa kuwa Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais TAMISEMI.
|
No comments:
Post a Comment