Matokeo chanyA+ online




Monday, June 10, 2019

DKT. AGNES KIJAZI AJITOSA KINYANG’ANYIRO CHA UMAKAMU WA TATU WA RAIS WMO

Na. Christopher Philemon, Monica Mutoni-Geneva.  
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt.Agnes Kijazi yupo nchini Uswisi –Geneva kwenye Mkutano wa 18 wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO-18 Congress) .Mkutano huu hufanyika kila baada ya miaka 4 ambapo mwaka huu unafanyika jijiji Geneva kuanzia tarehe 3- 14 juni ,2019.

Katika Mkutano huo utafanyika uchaguzi wa viongozi wakuu wa WMO ,ambao ni pamoja na Rais ,Makamu wa Kwanza wa Rais ,Makamu wa Pili wa Rais ,Makamu wa Tatu wa Rais na viongozi wengine wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani(WMO).

Tanzania kupitia Dkt Agnes Kijazi amejitosa katika kinyang’anyiro cha kugombea nafasi ya makamu wa tatu wa Rais wa WMO. Dkt Kijazi anaungwa mkono na wakuu wote wa taasis za hali ya hewa barani Afrika na azimio hili lilipitishwa katika Mkutano wa Mawaziri wenye Dhamana ya Huduma ya Hali ya Hewa Barani Afrika (African Ministerial Conference on Meterology - AMCOMET) tarehe18 - 23 Februari, 2019 Jijiji Cairo Misri  ambapo Tanzania iliwakilishwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye ambaye kupitia hotuba yake alifanikiwa kuwaombea wajumbe  kumpitisha Dkt Kijazi kama mgombea pekee barani Afrika.

“Kutokana na umuhimu wa nafasi tunayoiomba kwa Taifa na Afrika kwa ujumla, na hasa ukizingatia heshima ambayo tumepewa na Nchi za Afrika kuweka azimio la kumuunga mkono Dkt Kijazi, ili achaguliwe katika nafasi ya makamu wa tatu wa rais ambayo ina wagombea wengine kutoka mabara mengine, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa Kushirikiana Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,zinazendelea kushiriki katika kuomba wajumbe  kutoka nchi mbalimbali  hapa mjini Geneva kumpigia kura Dkt.Kijazi ili ashinde nafasi hiyo” alisema Nditiye.

Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii iliandaa hafla ya kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana Tanzania kwa kuwaalika wajumbe mbalimbali wa mkutano wa 18 wa WMO. Aidha katika  salamu za viongozi wakuu wa WMO akiwepo Rais wa sasa wa WMO  Bw David Grimes  aliwaomba wajumbe kumuunga mkono Dkt Kijazi kutokana na uchapa kazi wake, kauli ambayo ilirudiwa pia na Katibu Mkuu wa WMO Prof. Petteri Telaas alisema pamoja na utendaji uliotukuka wa Dkt Kijazi, bado shirika hilo halijawahi kupata kiongozi kike kwenye nafasi ya juu kama hiyo hivyo akawaomba pia wamuunge mkono.
IMG_0545 Naibu waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye  na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Hali ya Hewa Tanzania(TMA) Dkt.Agnes Kijazi katikati wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe  kutoka nchi mbalimbali walioudhuria kwenye Mkutano wa 18 wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO-18 Congress)  unaofanyika nchini Uswisi –Geneva.( Picha na Christopher Philemon)

No comments:

Post a Comment