Upanuzi
wa New Bagamoyo road awamu ya pili unaendelea,Upanuzi wa barabara hiyo
ukikamilika utapunguza adha kubwa ya msongamano wa magari wakati wa
kuingia na kutoka katikati ya jiji.
Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo (JICA), iliipatia Tanzania ruzuku ya Yen bilioni 3.78 sawa na Shilingi bilioni 77.3 kwa ajili ya upanuzi wa barabara ya New Bagamoyo, kuanzia Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es Salaam.
Makubaliano ya msaada huo yalitiwa saini Februari 28, 2018, Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, kwa niaba ya Serikali, na Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida na kushuhudiwa na Mwakilishi Mkazi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Japani (JICA), Toshio Nagase na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini-Tanroads, Mhandisi Patrick Mfugale.
Mradi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 4.3 utahusisha barabara yenye njia nne pamoja na kuanza kwa awamu ya nne ya ujenzi wa barabara itakayotumiwa na mabasi ya mwendo wa haraka (BRT phase IV).
Akizungumza baada ya kutiwa saini wa makubaliano hayo, Bw. Doto James alisema kuwa barabara hiyo ikikamilika itasaidia kutatua changamoto ya msongamano wa magari yanayotoka na kuingia katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
“Upanuzi wa Barabara ya New Bagamoyo si tu kwamba utaondoa msongamano wa magari, bali pia ni kiungo muhimu cha Bandari ya Bagamoyo ambayo itarahisisha usafirishaji wa abiria, mizigo na huduma kutoka Jiji la Dar es Salaam, mkoa wa Pwani na mikoa mingine nchini” Alisema Bw. Doto James.

No comments:
Post a Comment