Waziri
wa Madini Doto Biteko amekutana na Mwekezaji wa Kampuni ya Ngwena
Tanzania Ltd “Ngwena” na kufanya nao mazungumzo kuhusu masuala
mbalimbali, kubwa likiwa ni kutoa Ufafanuzi kuhusu Marekebisho ya Sheria
ya Madini inavyotoa fursa na mazingira mazuri ya uwekezaji katika sekta
ya madini hapa nchini.
Hatua
hiyo inafuatia ombi la kampuni hiyo kuomba kukutana na waziri Biteko
ili kupata ufafanuzi wa moja kwa moja kutoka kwake kuhusu mabadiliko
hayo ya sheria.
Ombi
la kutaka kuonana na waziri ni kutokana na kampuni ya Ngwena kupata
taarifa za upotoshaji na zisizo sahihi kuhusu mabadiliko ya sheria ya
madini yaliyofanywa na Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu
taratibu mbalimbali za uwekezaji na shuguli nyingine zinazo husu sekta
ya madini.
Upotoshaji
unaofanywa kwa maksudi na baadhi ya watu ndani nan je ya nchi kwa lengo
la kutaka kuifanya Tanzania kama sio mahali sahihi pa kuwekeza.
Biteko
ameuambia ujumbe wa kampuni ya Ngwena kuwa, mabadiliko ya sheria
yamefanyika kwa kuzingatia maslahi ya pande zote mbili mwekezaji na
taifa kwa upande mwingine.
Amefafanua
kuwa, tangu mabadiliko hayo yapitishwe hakuna malalamiko ya kupingwa
kwa marekebisho hayo kwakuwa yalizingatia maslahi mapana ya kila upande
na kuhakikisha mazingira ya uwekezaji yanakuwa rafiki na ndio sababu
mpaka sasa tangu marekebisho hayo yafanyike hakuna kampuni au muwekezaji
alie acha wala kuonyesha nia ya kufunga shuguli zake kwa sababu ya
marekebisho ya sheria.
Ameongeza
kuwa, Tanzania inawahitaji sana wawekezaji na mara zote kila panapokuwa
na jambo haliendi sawa mara moja hukaa na kujadili na mwekezaji na
kutatua changamoto.
Ameitaka
kampuni ya Ngwena kwenda kuwa mabalozi ili kuwaeleza wengine kuhusu
ukweli ulivyo kuhusu marekebisho ya sheria yaliyofanywa na kuachana na
upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya watu ambao hawana dhamana ya
kuyazungumzia masuala hayo.
Amewakaribisha watu na wawekezaji wote wanaotaka kupata ufafanuzi wa jambo lolote kutembelea ofisini kwake jijini Dodoma.
Aidha,
kwa upande wa kampuni ya Ngwena ukiongozwa na Meneja Mkuu H.E Kavishe
amemshukuru Waziri kwa ufafanuzi mzuri alioutoa na kwamba walichokuwa
wanakisikia na alichokisema waziri ni vitu tofauti na kuongeza kuwa,
kuonana kwao kumewafungua masikio na kupata ukweli kutoka kwenye mtu
sahihi na mwenye dhamana ya sekta ya madini.
Ameongeza
kuwa, ni kweli upotoshaji waliokuwa wanaupata ungeweza hata kuwarudisha
nyuma, hivyo watakwenda kufikisha ujumbe kwa wenzao.
Kikao
hicho pia, kimehudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon
Msanjila, Kamishna wa Madini, Mhandisi David Mulabwa, Mkurugenzi wa
Huduma za Sheria Edwin Igenge, na Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara
ya Madini, Augustine Ollal, Kamishna masaidizi anaeshuugulikia Migodi na
Biashara Ali Ali na Kamishna masaidizi anaeshugulikia Lesseni Maduh.
Waziri
wa Madini Doto Biteko wa Kulia katikati akisisitiza jambo wakati wa
kikao chake na ujumbe wa Kampuni ya Ngwena Tanzania Ltd “Ngwena”
waliomtembelea waziri kupata ufafanuzi kuhusu marekebisho ya sheria ya
madini. Kulia kwake ni Katibu Mkuu wizara ya Madini Prof. Simon
Msanjila.
Waziri
wa Madini Doto Biteko wa Kulia na Katibu Mkuu wizara ya Madini Prof.
Simon Msanjila kushoto katikati wakiwasikiliza wageni wao wakati wa
kikao cha pamoja na ujumbe wa Kampuni ya Ngwena Tanzania Ltd “Ngwena”
waliomtembelea waziri ofisini kwake kupata ufafanuzi kuhusu marekebisho
ya sheria ya madini.
Waziri
wa Madini Doto Biteko hayupo pichani akimsikiliza kwa makini mmoja wa
wajumbe wa Kampuni ya Ngwena Tanzania Ltd “Ngwena” waliomtembelea
ofisini kwake kuja kupata ufafanuzi kuhusu marekebisho ya sheria ya
madini.
Na Issa Mtuwa – Dodoma
No comments:
Post a Comment