Mkutano wa 23 wa Taasisi zinazosimamia Mawasiliano kwa Nchi za Afrika Mashariki, (EACO) umeanza leo Julai 1, 2019 jijini Mwanza.
Sambamba
na mkutamno huo pia wajumbe watashiriki Mkutano Mkuu wa 26 wa EACO
ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Kuiweka Afrika Mashariki katika eneo
la Uchumi wa Kidijitali".Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Mhandisi, Atashasta Nditiye, ndiye aliyefungua mkutano huo utakaodumu
hadi Julai 5, wenyeji ni Tanzania, pamoja na mataifa mengine ya WAC,
ambayomni Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.
Naibu
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (wapili
kushoto), akiongozana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasilkiano
Tanzania (TCRA), Mhandisi James M. Kilaba (watatu kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya (TCRA), Dkt. Jones Killimbe (wanne kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa EACO
Dtk. Ally Yahya Simba(wakwanza kulia) na Mwakilishi wa Katibu Mkuu
Mawasiliano Bw.Mulembwa Munaku. (wakzwanza kushoto), baada ya kufungua
mkutano wa 23 wa Taasisi zinazosimamia Mawasiliano Afrika Mashariki
(EACO), utakaofuatiwa na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 26 wa EACO jijini
Mwanza Julai 1, 2019
Muwakilishi wa Umoja wa Shirika la Posta
Duniani (upu), Kusini mwa Afrika na Asia, Bi. Gladys Mutyavaviri ambaye
alimwakilisha Katibu Mkuu wa upu, akizungumza kwenye mkutano huo wakati wa
ufunguzi.
Mkurugenzi
Mkuu wa TCRA, Mhandisi James M. Kilaba, akizungumza na waandishi wa
habari kufafanua baadhi ya mambo kuhusu mkutano huo.
Wajumbe kutoka Burundi, wakisikilzia hotuba ya Mhe. Naibu Waziri.
Wajumbe kutoka Kenya, wakisikilzia hotuba ya Mhe. Naibu Waziri.
Wajumbe kutoka Rwanda, wakisikilzia hotuba ya Mhe. Naibu Waziri.
Wajumbe wenyeji Tanzania, wakimsikiliza Mhe. Naibu Waziri Mhandisi Nditiye wakati akifungua mkutano huo.
Mhe. Naibu Waziri Mhandisi Nditiye na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka mataifa wanachama wa EACO. |
No comments:
Post a Comment