Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ametoa nafasi
kwa Wadau wa Utalii nchini kuwa Uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii
upo tayari kupokea ushauri, mapendekezo pamoja na mawazo mapya
yatakayosaidia kuchochea na kuinua idadi ya watalii wa ndani.
Pia,
Amewataka watu binafsi, mashirika pamoja na Wawekezaji wa ndani na nje
ya nchi wenye nia ya kutaka kuwekeza kwenye sekta ya utalii wasisite
ofisi yake ipo wazi kwa mtu yeyote.
"Kwa
yeyote atakayetaka kuniona kwa ajili ya kukuza na kuendeleza utalii
hasa utalii wa ndani kwangu Mimi pamoja Waziri milango ipo wazi muda
wote" alisisitiza Kanyasu.
Hayo
ameyasema wakati alipokuwa akizungumza na Watalii wa ndani wapatao 200
kutoka jijini Dar es Salaam ambao walitembelea katika Msitu Asilia wa
Magoroto katika wilaya ya Handeni mkoani Tanga kwa ajili ya kutalii
ndani ya msitu wenye kila aina ya vivutio vya utalii likiwemo ziwa la
kutengenezwa.
Kundi
hilo la watalii wa ndani liliratibiwa na Kampuni ya Dalida Tours and
Travel Agency kupitia chini ya Usimamizi wa Mratibu wa safari hiyo ,
Emma David.
Mhe.
Kanyasu amesema moja ya mkakati wa Wizara ni kutaka watalii wa ndani
wawe namba moja kwa kutembelea vivutio vya utalii badala ya kutegemea
Watalii wa kutoka nje kama ilivyo sasa.
Aidha,
Mhe.Kanyasu amesema pia Wizara yake ipo tayari kupokea na kutoa msaada
wa hali na mali kwa mtu au kikundi cha watu kitakacholenga kuhamasisha
utalii wa ndani.
''Tunataka
akili mpya na mawazo mapya ya namna ya kusukuma na kujenga utamaduni wa
watu wetu Wawe wa kwanza kutalii kama ilivyo kwa China'' Alisisitiza
Kanyasu
Ameongeza
kuwa Idadi ya watalii wa ndani hairidhishi hivyo kunahitajika mkakati
wa pamoja katika kuhamasisha utalii wa ndani kwa Watanzania ili waweze
kutembelea vivutio hivyo.
Katika
hatua nyingine, Mhe.Kanyasu amesema kama nchi haiwezi kuifanya sekta ya
utalii kama injini ya uchumi endapo Wazawa wenyewe wataendelea kuwa
nyuma huku utalii wa ndani ukiwa na mwitikio mdogo.
"
Kama taifa na kwa Mwananchi mmoja mmoja bado hatujaitendea hali sekta
ya Utalii ni sekta ambayo haijaguswa hata kidogo ni lazima wananchi
wawekeze na wakati huo huo wananchi watembelee vivutio vya
Utalii.Amesisitiza Kanyasu
Naye,
Emma David ambaye ni Mratibu wa kundi hilo la watalii wa ndani amesema
wamejipanga kuhamasisha idadi kubwa zaidi ya watalii wa ndani kwa
kupitia mitandao ya kijamii ili waweze kutembelea vivutio mbalimbali
vilivyoppo nchini.
''Sisi
tumejipanga kutembelea mikoa yote lengo letu ni kuunga mkono jitihada
za Wizara katika kuhamasisha Utalii wa ndani, Alisisitiza Emma.
Aidha,
Ameishukuru Wizara kwa jitihada inazozifanya za kutengeneza mazingira
rafiki kwa watu wenye nia ya kutaka kuwekeza kwenye utalii wa ndani.
Naye,
Meneja wa Magoroto, Jeremia Mchechu amesema mwitikio wa wa watalii
kutoka ndani na nje ya nchi umekuwa mkubwa tangu walipoanzisha eneo hilo
kama kivutio cha Utalii na eneo la ziwa ambalo ni la kutengeneza
limekuwa kivutio kikubwa cha Utalii.
Amesema
watalii wengi wanaofaika katika eneo hilo wamekuwa wakipendelea kupanda
milima, kuapnda baiskeli milimani pamoja na kutembelea vijijini kwa
ajili ya kujifunza tamaduni ya wakazi wa Tanga.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akimkabidhi
cheti Mratibu wa safari ya Utalii wa ndani, Dayna Saimoni ikiwa ni
ishara ya shukrani kwa kuunga mkono jitihada za Wizara ya Maliasili na
Utalii katika kuchochea na kuinua idadi ya watalii wa ndani katika Msitu
Asilia wa Magoroto katika wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akimkabidhi
cheti Mratibu wa safari ya Utalii wa ndani, Esta Satta ikiwa ni ishara
ya shukrani kwa kuunga mkono jitihada za Wizara ya Maliasili na Utalii
katika kuchochea na kuinua idadi ya watalii wa ndani katika Msitu Asilia
wa Magoroto katika wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Nhe, Constantine Kanyasu akizungumza na
watalii wa ndani walitembelea Msitu asilia wa Magoroto ambao ni kivutio
kikubwa cha Utalii wakati walipokusanyika usiku kufurahia ngoma za
kabila la wadigo.
Kundi
la watalii wa ndani kutoka jijini Dar es Salaam walioungana kwa pamoja
na kwenda kutembelea msitu Asilia wa Magoroto katika wilaya ya Handeni
mkoani Tanga.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwa kwenye
picha ya pamoja na watalii wa nje mara baada ya kuwasili katika msitu
Asilia wa Magoroto katika wilaya ya Handeni mkoani Tanga
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwa kwenye
picha ya pamoja na watalii wa ndani mara baada ya chakula cha jioni
katika msitu Asilia wa Magoroto katika wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
Baadhi
ya watalii wa ndani na wa nje nyakati za usiku wakifurahia ngoma ya
kabila wasambaa iliyokuwa ikitumbuizwa kwa watalii hao. (Picha na Wizara
ya Maliasili na Utalii)
No comments:
Post a Comment