Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amewaomba wananchi wa mkoa
wa Geita pamoja na maeneo jirani na mkoa huo kujitokeza kwa wingi siku
ya jumatatu kwenye tukio la uzinduzi wa nyumba za Amakazi ya askari,
uzinduzi utakaofanyika katika eneo la magogo mkoani humo.
IGP
Sirro amesema kuwa, katika tukio hilo ambalo litaongozwa na Mhe. Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli, ambapo atazindua
zaidi ya nyumba 114 zilizokwisha kamilika huku matarajio ya mradi huo ni
kuwa na nyumba takribani 400 kwa nchi nzima.
Aidha,
IGP Sirro amewaomba wadau mbalimbali kuendelea kushirikiana na Jeshi la
Polisi katika kuhakikisha askari wanaishi kwenye mazingira mazuri jambo
ambalo litachangia weledi na uwajibikaji hususan kulinda maisha ya raia
na mali zao.
No comments:
Post a Comment