Muonekano
wa Jengo Jipya la Maabara ya Sayansi katika Skuli ya Sekondari ta
Kilindi linalojengwa na S erikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia.
Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba Maalim Mohamed
Nassor akitoa Taarifa ya ujenzi wa Mabara ya Sayansi Skuli ya Kilindi
mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
aliyefika kukagua Ujenzi huo.
Balozi
Sdeif akiambatana na Mkuu wa Mkoa Kusini Pemba Mh. Hemed Suleiman
Abdullah akiangalia ujenzi wa Maabara ya Sayansi Skuli ya Sekonmdari ya
Kilindi Mkoa wa Kusini Pemba.
Mkuu
wa Mkoa Kusini Pemba Mh. Hemed Suleiman Abdulla akiishukuru Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kwa jitihada inazochukuwa za kusogeza maendeleo
ndani ya Mkoa huo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na
Wananchi wa Kijiji cha Kilindi na Vitongopji vyake baada ya kulikagua
Jengo la Maabara ya Sayansi katika Skuli ya Kijiji hicho.
Balozi
Seif akizungumza na Viongozi wa Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa
Miwili ya Pemba kwenye Ukumbi wa Kiwanda cha Makonyo Wawi Chake chake
Pemba kujadili zoezi la uhakiki wa kuyatambua mashamba na Eka za
Serikali.
Balozi Seif akisisitiza jambo wakati akizungumza
na Viongozi wa Kamati za ulinzi na Usalama za Mikoa Miwili ya Kusini
na Kaskazini Pemba hapo Ukumbi wa Makonyo Wawi Chake Chakle Pemba.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeanza kuonyesha kwa vitendo
utekelezaji wa msingi wa uimarishaji wa Miundombinu katika Sekta ya
Elimu kwenye Fani ya Sayansi ili kwenda sambamba na mabadiliko ya
sayansi na Teknolojia yaliyopo Ulimwenguni.
Alisema utekelezaji huo umezingatia muelekeo wake katika Ujenzi wa
Majengo 24 ya Maabara ya Sayansi { School Hurb } katika Visiwa vya
Unguja na Pemba yatakayojikita na masomo ya Kemia, Fizikia na Biology.
Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo mwanzoni wa ziara yake ya Siku Nne
Kisiwani Pemba kuangalia Miradi ya Maendeleo pamoja na ufuatiliaji wa
Mashamba na Eka tatu tatu ambazo bado haliko kwenye Miliki ya
Serikali.
Alisema wakati umefika kwa wanafunzi wa Skuli za Sekondari Unguja na
Pemba kuchangamkia fursa hiyo ambayo katika siku za baadae itaweza
kuziba pengo la upungufu wa Wataalamu wa Fani ya Sayansi hapa Nchini.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameridhika na kiwango kizuri cha
Ujenzi kilichofikiwa na Wahandisi wa Majengo hayo Kampuni ya
Kizalendo ya Salim Contructor na kuzitaka Kampuni nyengine
zitakazopewa jukumu la ujenzi wa Majengo ya Serikali na Taasisi za
Umma kuzingatia ubora wa kiwango kinachokubalika.
Akitoa Taarifa ya Ujenzi wa Maabara ya Sayansi ya Skuli ya Kilindi
Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba Nd. Mohamed
Nassor alisema Maabara hiyo ni miongoni mwa Majengo 24 yanayoendelea
kujengwa katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar.
Nd. Mohamed alisema Maabara ya Sayansi {Shool Hurb} yameanzishwa kama
vituo vya kutoa huduma katika masomo ya Sayansi likiwemo pia somo mama
la Kingerezakwa Wanafunzi hasa waliko Vijijini ambao kwa muda mrefu
wamekuwa wakikosa fursa hizo.
Akitoa salamu Mkuu wa Mkoa Kusini Pemba Mheshimiwa Hemed Suleiman
Abdulla alisema Wananchi wa Mkoa huo wanafurahia Maendeleo makubwa
yanayopatikana chini ya Uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein.
Alisema huduma za Maji safi na salama, Umeme Bara bara za Lami pamoja
na miundombinu ya Miradi ya Kiuchumi imekuwa ikileta matumaini ya
kuongezeka kwa Kipato cha Wnanchi hao jambo ambali limestawisha Maisha
yao ya kila siku.
Mh. Hemed alisema Wananchi wana kila sababu ya kujivunia maendeleo
hayo makubwa yanayoonekana kila pembe katika dhana nzima ya
Utekelezaji wa vitendo wa ahadi zilizotolewa na Serikali ikiwemo
kuwasili kwa vifaa vya kutengenezea Miundombinu ya Mawasiliano
Kisiwani Pemba.
Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
alikutana na Viongozi wa Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa Miwili
ya Pemba katika Ukumbi wa Mikutano wa Makonyo Wawi Chake Chake Pemba.
Mkutano huo uliohudhuriwa pia na Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar ulijadili na kutafakari hatua zilizochukuliwa na
Taasisi mbali mbali Kisiwani Pemba zilizopewa jukumu la kufuatilia na
kubaini Mashamba na Eka za Serikali ambazo kwa kipindi kirefu ziko
mikononi mwa Watu.
Akitoa Taarifa ya zoezi hilo Afisa Mdhamini Wizara ya Kilimo,
Malisili, Mifugo na Uvuvi Pemba Nd. Sihaba Haji Vuai alisema Wizara
hiyo imekabidhiwa Madaftari yenye takwimu za Mashamba na Eka za
Serikali tokea Mwaka 20113.
Alisema vielelezo vilivyomo ndani ya Mabuku hayo Matatu vimeainisha
uwepo wa Mashamba na Eka 2,438 Wilaya ya Mkoani, eka 2,299 Wilaya ya
Chake chake na Ekari 2,273 Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Nd. Sihaba alisema Watendaji wa Wizara ya Kilimo ilianza zoezi la
kuyafuatilia Mashamba na eka za Serikali katika maeneo mbali mbali kwa
kushirikiana na Masheha wa Shehia zilizomo Shamba na Eka hizo.
Alisema zoezi hilo liliweza kubaini uwepo wa Eka 838 Wilaya ya Mkoani,
eka 295 Wilaya ya Chake chake, eka 992 Wilaya ya Wete na eka831 katika
Wilaya ya Micheweni.
Alifahamisha kwamba mashamba yote ya Serikali yaliyomo ndani ya mikono
ya Watu yamekadiriwa kufikia 9,982, ambapo hadi sasa yaliyobainika
hadi sasa ni mashamba 6,315 sawa na asilimia 63% ya mashamba yote
Kisiwani Pemba.
Afisa mdhamini huyo wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugona Uvuvi
Pemba alieleza kwamba uchambuzi wa mashamba na eka hizo umefafanua
kwamba Mashamba 2016 yana miti ya Mikarafuu, mashamba 721 miti ya
Minazi, 1,884 mazao mchanganyiko, 365 yameachwa muda mrefu, 600
yamegeuzwa kuwa Makaazi na 1200 mashamba yaliyofungishwa Mkataba.
Alisema Mashamba yapatayo Mia 732 yako kwenye utaratibu wa kutaka
kugaiwa kwa Wananchi kwa shughuli za kuendeleza Kilimo ili kusaidia
kunyanyua kipato chao kitakachokidhi maisha yao.
Nd. Sihaba alisema utayari mdogo wa baadhi ya Viongozi, Taasisi za
Umma pamoja na Wananchi ndio unaopelekea baadhi ya Eka walizopewa
Wananchi kwa shughuli za Kilimo kugezwa matumizi mengine jambo
linalokwenda kinyume na malengo ya utolewaji wa Eka hizo mnamo Mwaka
1964.
Wakichangia Taarifa hiyo Baadhi ya Wajumbe wa Kikao hicho walisema
Viongozi wanaosimamia zoezi hilo lazima wawe tayari kufuatilia kwa
kina mashamba hayo na kuondoa muhali unaopelekea kuzorotesha zoezi
hilo muhimu.
Walisema ipo haja ya kufuatilia kwa kina kuanzia ngazi ya Mtaa, shehia
hadi Jimbo ili kuibaini Mashamba na Eka ambazo hadi sasa ziko ndani ya
mikoni ya baadhi ya Watu.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
Ali Iddi alisema zoezi hilo la kubaini mashamba na eka za Serikali
zilizo mikononi mwa Watu halina lengo la kuwanyang’anya wale
wanaoendelea kuzitumia badhi kinachofanyika ni utambuzi wa kujua mali
za Serikali.
Balozi Seif alisema wapo baadhi ya Wananchi katika maeneo tofauti
Nchini wanayashughulikia mashamba na Eka za Serikali na unapofika
wakati wa mazao wao ndio wanaopewa nafasi ya kwanza kukodi hasa katika
upande wa zao la Karafuu.
Hata hivyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alitahadharisha kwamba
Serikali haitasita kuchukuwa hatua za kunyang’anya Eka ya Serikali Mtu
ye yote atakayebainika kuificha mali ya Serikali.
No comments:
Post a Comment