Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
akiongoza msafara wakati akifanya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa ghorofa
sita katika kitengo cha wazazi Meta Jijini Mbeya ambalo litakuwa na
uwezo wa vitanda 200.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
akiongozana na Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya kanda Mbeya
Dkt. Godlove Mbwanji wakati wa ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa ghorofa
sita katika kitengo cha wazazi Meta Jijini Mbeya ambalo litakuwa na
uwezo wa vitanda 200.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
akifuatilia ramani ya ujenzi wa mradi wa ujenzi wa ghorofa sita katika
kitengo cha wazazi Meta Jijini Mbeya ambalo litakuwa na uwezo wa vitanda
200.
Ujenzi
wa mradi wa ghorofa sita wenye gharama ya shilingi Bilion 7, katika
kitengo cha wazazi Meta Jijini Mbeya ambalo litakuwa na uwezo wa vitanda
200 ukiendelea katika kitengo cha wazazi Meta Jijini Mbeya.
Picha
ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na Mkurugenzi wa Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa ya kanda Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji baada ya ukaguzi wa
mradi wa ujenzi wa ghorofa sita katika kitengo cha wazazi Meta Jijini
Mbeya.
Na WAMJW- MBEYA
Serikali
kupitia Wizara ya Afya inajenga jengo la Wazazi lenye thamani ya
shilingi Bilioni 7 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ya kuboresha huduma
za Afya kwa wananchi wa Mkoa wa Mbeya na nyanda za juu kusini.
Hayo
yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya
utoaji huduma za Afya na ujenzi wa miradi katika Hospitali ya Rufaa ya
kanda Mbeya.
Waziri
Ummy amesema kuwa Serikali imedhamiria kuboresha upatikanaji wa huduma
za Afya nchini ikiwemo huduma za kibingwa ili kuondoa usumbufu kwa
Wananchi wanaohitaji huduma hizo kwa kusafiri umbali mrefu i jambo
linalopelekea gharama kubwa na usumbufu kwa wananchi.
“Tunajenga
jengo la wazazi na watoto wachanga la ghorofa sita, ambalo litakuwa na
jumla ya vitanda 200, vyumba vitatu vya upasuaji kwa ajili ya wanawake
wajawazito ,vyumba sita kwa ajili ya uangalizi maalum (ICU) kwa wanawake
wajawazito, pia vyumba maalum vinne kwa ajili ya vitoto vichanga
(NICU)” alisema Waziri Ummy.
Kwa
upande mwingine, Waziri Ummy amemwagiza Mkandarasi wa majengo hayo
kuhakikisha wanaharakisha ujenzi wa majengo hayo ili wananchi waanze
kupata huduma mapema jambo litalosaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto
nchini.
Aidha,
Waziri Ummy ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Mbeya na nyanda za juu
kusini kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya ili kurahisisha gharama za
matibabu.
“Nitoe
Wito kwa wananchi wa Mkoa wa Mbeya na nyanda za juu kusini ili waweze
kufurahia huduma nzuri lazima wajiunge na huduma za Bima ya Afya, Kuna
NHIF Toto Afya kadi kwa mtu yoyote mwenye umri wa chini ya miaka 18 ni
shilingi 50,400 huduma mwaka mzima ndani ya Mbeya na Tanzania kwa
ujumla” alisema Mhe. Ummy Mwalimu
Kwa
upande mwingine, Waziri Ummy amesema kuwa katika kila wanawake 100,
wanawake 85 wanajifungua bila matatizo yoyote, huku akisisitiza
kukamilika kwa ujenzi huu kutasaidia kukokoa wanawake 15 waliobaki
kutokana na huduma Bora zakibingwa zitakuwa zikitolewa.
Naye,
Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya kanda Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji
ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kukubali kutenga fedha
ili kujenga jengo la ghorofa sita katika kitengo cha wazazi Meta ambalo
litakuwa na uwezo wa vitanda 200 jambo litalosaidia kutatua changamoto
ya ufinyu wa nafasi.
“Tunapenda
kutoa shukurani za dhati kwa Serikali ya awamu ya tano, kwa kukubali
kutenga fedha kupitia Wizara unayoiongoza ili kuweza kujenga jengo la
ghorofa sita katika kitengo cha wazazi Meta, ambalo litakuwa na uwezo wa
vitanda 200.” Alisema Waziri Ummy
No comments:
Post a Comment