Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amemrejeshea eneo
lake lililoko Jangwani Beach wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam Brigedia
Jenerali Mstaafu Francis Mbena kufuatia kuhangaika kwa miaka 20
kulirejesha eneo alilodhulumiwa.
Akizungumza
wakati akimkabidhi hati ya kiwanja chake leo eno la Mbezi Beach Dar es
Salaam Lukuvi alisema, Brigedia Mstaafu Mbena alitaka kudhulumiwa eneo
lake na Idan Mongi aliyeuziwa eneo hilo na John Rwechungura.
Kwa
mujibu wa Lukuvi, kiwanja hicho chenye ukubwa wa takriban mita za mraba
2000 hati yake iligushiwa na baadaye kiwanja hicho kuuzwa kwa Mongi
ambapo alieleza mnunuzi huyo alitapeliwa kwa kuwa kiwanja kilikuwa
kimefutwa.
Lukuvi
alitoa onyo kwa wanasheria kuacha tabia ya kuchelewesha kesi kwa
kutowaeleza ukweli wateja wao iwapo kesi wanayoishughulikia hawezi
kushinda na kufafanua kuwa ni bora wanasheria wakawaeleza ukweli
kuhusiana na mwenendo wa kesi wanazoziendesha kuhusina na masuala ya
ardhi.
Aidha,
amewataka wananchi wanaotaka kununua viwanja kufanya utafiti katika
ofisi ya Msajili wa Hati Wizarani kwa lengo la kujiridhisha umiliki wa
muuzaji wa eneo husika.
Kwa
upande wake Brigedia Jenerali Mstaafu Mbena amefurahishwa na uamuzi
uliofanywa na Lukuvi wa kumpatia hati yake aliyoihangaikia kwa miaka 20
na kueleza kuwa eneo hilo limekuwa likimtesa sana kwa kuendesha kesi
kwa muda mrefu na kutumia fedha yake ya pensheni kuendeshea kesi.
Mbena
alisema eneo hilo alilipata mwaka 1988 Oktoba 3 na kuingia katika
mgogoro baina yake na watu wanaodai kulimiki kuanzia mwaka 1999ambapo
kesi ilianzia Baraza la Ardhi na Nyumba na kufikia Mahakama Kuu amapo
iliisha mwaka jana Julai na Mbena kushinda.
Naye
Idan Mongi aliyetapeliwa kiwanja hicho alieleza kuwa kiwanja
alichotapeliwa kina historia ndefu ambapo kabla yeye kukinunua
kilipitia kwa wamiliki wengine watatu na kubainisha kuwa yeye alikinunua
kwa John Rwechungura mwaka 2009.
Alisema
kuwa, anamkabidhi eneo lake Brigedia Mstaafu Mbena kwa moyo mmoja na
hatabomoa nyumba na ukuta aliojenga na ameomba kuhamisha vitu vyake
ndani ya miezi mitatu.
Lukuvi
alisema, kutokana na uungwana aliounesha Idan Mongi Wizara itamzawadia
kiwanja katika eneo la Pemba na Mnazi Kigamboni kwa ajili ya ujenzi wa
nyumba ya kuishi tu.
No comments:
Post a Comment