Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akizindua kitabu cha muongozo wa uwekezaji katika
Mkoa wa Kagera, baada ya kufungua Kongamano la Wiki ya Uwekezaji Mkoa
wa Kagera na Mwongozo wa Uwekezaji mkoani humo. Agosti 14.2019.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi, baada ya kufungua kongamano la uwekezaji mkoani Kagera, Agosti 14.2019.

Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akioneshwa maeneo ya uwekezaji Mkoa wa Kagera na
Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba, Benard Limbe, kabla ya kufungua
kongamano la uwekezaji mkoani Kagera, Agosti 14.2019.

Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wajasiriamali wa kikundi cha
Wanawake cha Bezaleli, wakati akikagua mabanda, kabla ya kufungua
kongamano la uwekezaji mkoani Kagera, Agosti 14.2019.

Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa ameshika madini ya kopa, akifafanuliwa
jambo na Mkurugenzi wa Tanzania Plus Minerals Kyerwa, Salim Mhando,
wakati akikagua mabanda, kabla ya kufungua kongamano la uwekezaji mkoani
Kagera, Agosti 14.2019.

Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia mvinyo uliyotengenezwa kwa kutumia
ndizi, wakati akikagua mabanda, kabla ya kufungua kongamano la uwekezaji
mkoani Kagera, Agosti 14.2019. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kagera
Women Group, Bertha Kokulengya, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia
Jenerali, Marco Gaguti. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akiwasili mkoani Kagera, kwa ajili ya kufungua
Kongamano la Wiki ya Uwekezaji Mkoa wa Kagera na Mwongozo wa Uwekezaji
mkoani humo. Agosti 14.2019.
…………………….
Azitaka halmashauri nchini kuondoa urasimu, vikwazo kwa wawekezaji
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwaamezindua Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Kagera
wenye lengo la kutangaza fursa za Uwekezaji na hivyo, kukuza maendeleo
ya mkoa huona ameziagiza halmashashauri zote za wilaya nchini ziondoe
urasimu na kupunguza vikwazo kwa wawekezaji.
Waziri
Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Agosti 14, 2019) wakati akizindua
Kongamano la Wiki ya Kagera na Mwongozo wa Uwekezaji mkoani Kagera,
lilifanyika Bukoba mjini.Amewataka Watanzania wahakikishe wanachangamkia
fursa za biashara zilizopo.
Amesema
Watanzania wanao uwezo wa kutumia fursa za uwekezaji na biashara
zilizopo nchini kwa kushirikiana na taasisi za kifedha na kuwekeza
katika miradi mbalimbali nchini, badala ya kuachia fursa hizo
kuchukuliwa na wageni.
Amesema
azma ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John
Magufuli ya kukuza uchumi kupitia sekta ya na kufikia wa kati ifikapo
mwaka 2025 itaendelea kutekelezwa, hivyo, ametumia fursa hiyo
kuwakaribisha wawekezaji wa nje nao waje kuwekeza.
“Serikali
itaendelea kusimamia utekelezaji wa Sera ya Maendeleo Endelevu ya
Viwanda Awamu ya Tatu (2010/2020) na Mpango wa Pili wa Maendeleo wa
Miaka Mitano (2015/2016 2020/2021) ambao lengo lake ni kuendeleza uchumi
wa viwanda”.
Akizungumzia
kuhusu maadhimisho ya Wiki ya Uwekezaji Kagera, Waziri Mkuu amesema
yamelenga kuwakutanisha wadau wa uwekezaji, ambao ni pamoja na
Wafanyabiashara kutoka ndani ya mkoa na nchi jirani zinazozunguka Mkoa
wa Kagera.
“Ni
ukweli usiofichika kwamba tunahitaji wawekezaji watakaosaidia uchumi wa
mkoa huu kukua kwa kasi kupitia fursa zilizopo kwenye nyanja za kilimo,
mifugo, uvuvi, viwanda, maliasili na utalii”.
Waziri
Mkuu amesema ukuaji mzuri wa uchumi wa mkoa utakuwa na manufaa katika
kuongezeka kwa pato la mwananchi wa Kagera, pato la mkoa na hata pato la
Taifa nalo litakuwa kwa kasi ndani ya kipindi cha muda mfupi.
Amesema
mkoa wa Kagera ndiyo unaoongoza kwa uzalishaji wa kahawa nchini, ambapo
zaidi ya nusu ya kahawa yote huzalishwa katika mkoa huo. Wastani wa
uzalishaji wa kahawa kwa mwaka ni kati ya tani 50,000 hadi tani 65,000
kutegemea na hali ya hewa ya mwaka husika.
Hivyo,
mkoa huo una fursa kubwa ya uwekezaji kwenye viwanda vya kukoboa na
kusindika kahawa.Pia mkoa wa Kagera ni miongoni mwa mikoa michache
Tanzania yenye fursa nyingi za uwekezaji ambazo kwa namna moja au
nyingine hazipatikani katika mikoa mingine ya nchini. Miongoni mwa fursa
hizo ni pamoja na soko kwani unapakana nan chi nne za Afrika Mashariki.
“Kagera
imepakana na Uganda, Rwanda, Burundi na Kenya. Kupakana na nchi hizo
zenye idadi kubwa ya watu katika ukanda huu wanaokadiriwa kufikia
takriban milioni 190 ambapo kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2018 ni fursa
ya uwepo wa soko kubwa la bidhaa zinazozalishwa au zinazoweza
kuzalishwa katika mkoa wa Kagera”.
Kadhalika,
Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kuboresha miundombinu
mbalimbali ya usafiri ukiwemo wa anga na wa barabara ili kurahisisha
usafiri kutoka Bukoba makao makuu ya mkoa wa Kagera kufika katika nchi
hizo.
“Kwa
mfano, umbali kutoka Bukoba hadi Kampala ni km. 340, Bujumbura km. 550
na Kigali km. 490. Kadhalika, itakuwa ni rahisi kufikia masoko ya nchi
za Sudan Kusini pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo
(DRC)”.
Awali,
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti alisema dhamira
ya kuandaliwa kwa wiki ya uwekezaji mkoani Kagera ina lengo la
kuhakikisha kwamba mkoa huo unafanya vizuri katika sekta ya uwezekezaji
na biashara, hivyo kuchangia katika ukuaji wa pato la Taifa.
Alisema
mkoa wa Kagera ni miongoni mwa mikoa 10 ambayo inamchango mdogo katika
pato la Taifa, hivyo wanataka watoke kwenye kuchangia asilimia 3.9 hadi
wafikie asilimia 10.
Kwa
upande wao, viongozi mbalimbali wakiwemo Magavana kutoka na
wafanyabiashara kutoka nchi za Rwanda na Burundi waliahidi kutumia fursa
zilizopo nchini, pamoja na kuwakaribisha wafanyabiashara na wawekezaji
wa Tanzania kwenda kuwekeza katika nchi zao.
No comments:
Post a Comment