Afisa Viwango wa Kiwanda cha
kutengeneza saruji cha Dangote Bw. Issawema akiwaonesha Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki pamoja na
Naibu Waziri ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula matumizi
ya mifumo ya TEHAMA katika kuendesha kiwanda hicho.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Aidha amewapongeza Dangote kwa
uwekezaji huo mkubwa pamoja na kuanza ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme wao
wenyewe megawati 25 ambao megawati 5 zitaingia kwenye gridi ya taifa.
Amewataka wawekeze na maeneo mengine
siyo kwenye saruji tu na kuagiza TIC kupitia mikataba ya utendaji ya wawekezaji
wote mahiri kuona ni wapi wanaweza kuwekeza zaidi.
Wakiwa Mkoani Lindi Waziri Kairuki
na Mhe. Mabula walitembelea mgodi wa madini ya uno (graphite) uliopo katika Kijiji
cha Matambalale Kusini Wilaya ya Ruangwamkoani Lindi na kuona shughuli za awali
za mradi huo ambapo Meneja wa kampuni ya Lindi Jumbo inayochimba madini hayo Bw
Paul Shauri amesema mgodi utajengwa kwa muda wa miezi tisa na wanatarajia
kuwekeza zaidi ya dola za kimarekani milioni 30.
Akiongea mgodini hapo Dkt.Mabula
ameziagiza Halmashairi zote vijiji vyenye maeneo ya uwekezaji kufanya zoezi la
kuandaa mpango wa matumizi ya ardhi watenge maeneo ya uwekezaji wayahaulishe
yawe mali ya kijiji ili mwekezaji akipatikana watimize masharti mengine tu.
"Hakuna sababu ya mwekezaji
kuanza kuhangaika na mambo madogo kama hayo ambayo yanampotezea wakati ni
lazima halmashauri zijipange ili kumwekea mwekezaji mazingira mazuri avutiwe
kuwekeza"alisema Dkt.Mabula
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Ruangwa Hashim Mgandilwa akiwakaribisha Mawaziri hao amesema Serikali ione kuna
sababu ya kuharakisha ujenzi wa miundombinu ikiwemo barabara za wilaya hiyo
kwani kuna makampuni mengi makubwa yameonesha nia ya kuwekeza.
Amesema wilaya hiyo pia inakabiliwa
na changamoto ya mipaka ya asili na kwamba suala hilo tayari linaendelea
kutatuliwa kwa viongozi na watendaji kutoa elimu kwa wananchi.
|
No comments:
Post a Comment