Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo
Sept 03,2019 amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Dkt. John Pombe magufuli kwenye Shuhuli ya kuaga Mwili wa
Mwanasiasa Mkongwe Nchini Marehemu Ibrahim kaduma.
Katika
salam zake za pole kwa Wanafamilia, wafiwa na Watanzania wote kwa
Ujumla, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaomba kuwa na Subira
na Uvumilivu katika kipindi hiki cha Maombolezo na kumuomba Mwenyezi
Mungu kuwapa nguvu na Moyo wa Subira.
Wakati wa Uhai wake Marehemu Ibrahim Kaduma aliwahi kuwa Mwanasiasa pamoja na kupitia ngazi mbali mbali za Uongozi hapa nchini.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akitoa Heshima za Mwisho mbele ya Jeneza lenye Mwili wa Mwanasiasa
Mkongwe Nchini Marehemu Ibrahim Kaduma katika Kanisa la KKKT Makongo
Juu leo Sept 03,2019 ambapo Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John
Pombe Magufuli kwenye Msiba huo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akisani kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo kufuatia kifo cha Mwanasiasa
Mkongwe nchini Marehemu Ibrahim Kaduma alipowasili katika Kanisa la
KKKT Makongo Juu kwa ajili ya kumuwakilisha Rais Dkt. John Pombe
Magufuli kwenye Shuhuli ya kuaga Mwili wa Mwanasiasa huyo leo Sept
03,2019. Kushoto ni Dkt. Alex Malasusa Askofu wa KKKT Dayosis ya
Mashariki na Pwani.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akimfariji, Mjane wa Marehemu Marehemu IBrahim Kaduma katika Kanisa la
KKKT Makongo Juu, jijini Dar es salaam leo Sept 03,2019.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akisalimiana na Dkt. Alex Malasusa Askofu wa KKKT Dayosis ya Mashariki
na Pwani alipowasili katika Kanisa la KKKT Makongo Juu kwa ajili ya
kumuwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Shuhuli ya kuaga
Mwili wa Mwanasiasa Mkongwe Marehemu IBrahim Kaduma leo Sept 03,2019.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akisalimiana na kuwapa pole Baadhi ya Wajukuu na Vitukuu vya Mwanasiasa
Mkongwe Nchini Marehemu IBrahim Kaduma wakati wa shuhuli ya kuaga Mwili
wa Mwanasiasa huyo leo Sept 03,2019 katika kanisa la KKKT Makongo Juu,
Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Msiba
huo.
No comments:
Post a Comment