Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Agustine Ndugai
akitoa taarifa ya kuanza kutumia mfumo wa Tehama badala ya badala ya
mfumo wa makaratasi katika kuwasilisha orodha ya shughuli za bunge
wakati wa Mkutano wa 16 wa Bunge, Kikao cha Kwanza leo jijini Dodoma
tarehe 3 Septemba 2019.
Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Miraji Mtaturu akila kiapo mbele ya
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Agustine
Ndugai wakati wa Mkutano wa 16 wa Bunge, Kikao cha Kwanza leo jijini
Dodoma tarehe 3 Septemba 2019.
Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Miraji Mtaturu akisalimiana na Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira na Wenyeulemavu, Mhe. Jenista Mhagama mara baada ya kula kiapo
wakati wa Mkutano wa 16 wa Bunge, Kikao cha Kwanza leo jijini Dodoma
tarehe 3 Septemba 2019. Kutoka kulia ni Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, Mhe. William Lukuvi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt.
Adeladus Kilangi
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison
Mwakyembe(kulia), Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce
Ndalichako(kushoto) na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu
Kijaji (katikati) wakifurahia jambo wakati wa Mkutano wa 16 wa Bunge,
Kikao cha Kwanza leo jijini Dodoma tarehe 3 Septemba 2019.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Faustine Ndugulile akijibu swali wakati wa Mkutano wa 16 wa Bunge,
Kikao cha Kwanza leo jijini Dodoma tarehe 3 Septemba 2019.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe.
Elias Kwandikwa akifafanua jambo walipokuwa akijibu swali katika
Mkutano wa 16 wa Bunge, Kikao cha Kwanza leo jijini Dodoma tarehe 3
Septemba 2019.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ulinzi, Mhe.
Mussa Hassan Zungu akiwasilisha Azimio la Bunge la kupmpongeza Mhe.
Rasi Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa SADC na
kuendesha vyema Mkutano wa 39 wa Jumuiya hiyo wakati wa Mkutano wa 16,
Kikao cha Kwanza leo jijini Dodoma tarehe 3 Septemba 2019.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira,
Boniphace Simbachawene (aliyesimama) akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la
Bumbuli mkoani Tanga ambaye pia ni Waziri wa Zamani wa Ofisi hiyo, Mhe.
Januari Makamba (wapili kushoto) walipokutana katika Kikao cha Kwanza
cha Mkutano wa 16 wa Bunge leo jijini Dodoma tarehe 3 Septemba 2019.
Kulia ni Mbunge wa Kibaha, Mhe. Sylivester Koka.
Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Miraji Mtaturu akiuliza swali la
nyongeza wakatiwa kikao cha kwanza cha Mkutano wa 16 wa Bunge leo tarehe
3 Septemba 2019 jijini Dodoma. Mbunge huyo ameapishwa leo baada ya
kupita bila kupingwa katika uchaguzi mdogo uliofanyika kutokana na
nafasi kuwa wazi baada ya aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo kukosa sifa ya
kuendelea na Ubunge.
Baadhi ya wananchi wa Jimbo la Singida Mashariki waliomsindikiza Mbunge
wao Mhe. Miraji Mtaturu kushuhudia hafla ya kuapishwa kwake wakipunga
mikono baada ya kutambulishwa Bungeni katika Mkutano wa 16 wa Bunge
kikao cha kwanza leo tarehe 3 Septemba 2019 jijini Dodoma. Mhe. Mtaturu
amesindikizwa na zaidi ya wananchi 200 kutoka jimboni kwake. (Picha na
Idara ya Habari – MAELEZO)
No comments:
Post a Comment