Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana kwa furaha na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es
Salaam Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa’ichi ambaye anapatiwa matibabu katika
Taasisi hiyo ya Mifupa Muhimbili (MOI) mara baada ya kufanyiwa upasuaji
wa Kichwa
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiongoza sala ya kumuombea Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es
Salaam Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa’ichi ambaye anapatiwa matibabu katika
Taasisi hiyo ya Mifupa Muhimbili (MOI)
Askofu
Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa’ichi
akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Magufuli ambaye alienda kumjulia hali katika Taasisi hiyo ya
Mifupa Muhimbili (MOI). Wakwanza kulia ni Askofu Msaidizi Eusebius
Nzigilwa wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, kushoto ni Padre Dkt.
Alister Makubi Paroko wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya
Oysterbay jijini Dar es salaam
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa na Askofu Msaidizi Eusebius Nzigilwa wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar
es Salaam kulia, Padre Dkt. Alister Makubi kushoto, Paroko wa Kanisa
Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es salaam wakifurahia
jambo pamoja na Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam Mhashamu
Yuda Thadeus Ruwa’ichi ambaye hali yake imezidi kuimarika mara baada ya
kufanyiwa upasuaji katika taasisi hiyo ya MOI. PICHA NA IKULU.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo
tarehe 23 Septemba, 2019 amemjulia hali Askofu Mkuu Mkuu wa Jimbo Kuu
Katoliki la Dar es Salaam Mhashamu Yuda Thaddaeus Ruwa’ichi anayepatiwa
matibabu katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) Jijini Dar es Salaam.
Mhe.
Rais Magufuli amemkuta Baba Askofu Mkuu Ruwa’ichi akiwa anaendelea
vizuri tofauti na hali ilivyokuwa alipomtembelea tarehe 10 Septemba,
2019 siku aliyoletwa MOI akitokea Hospitali ya KCMC Mkoani Kilimanjaro
alikougua ghafla baada ya kupatwa na ugonjwa wa kiharusi.
Akiwa
MOI, Baba Askofu Mkuu Ruwa’ichi amefanyiwa upasuaji na timu ya Madaktari
Bingwa wa ubongo na mishipa ya fahamu kwa mafanikio na sasa anaendelea
vizuri.
Mhe.
Rais Magufuli ameeleza kufurahishwa kwake na kuimarika kwa hali ya Baba
Askofu Mkuu Ruwa’ichi na amewapongeza Madaktari Bingwa wa MOI kwa
kumtibu kwa mafanikio makubwa.
Aidha,
Mhe. Rais Magufuli, Baba Askofu Mkuu Ruwa’ichi, Baba Askofu Mkuu
Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mhashamu Eusebius Nzigilwa na
Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro Padre Dkt. Alister Makubi wamesali
sala ya pamoja ya kumshukuru Mungu kwa uponyaji na kuwaombea wagonjwa
wote wapone haraka.
Baada
ya kutoka MOI, Mhe. Rais Magufuli amewajulia hali wagonjwa waliolazwa
katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) akiwemo Baba Mzazi wa
Daktari wa Rais, Mzee Wilson Ngwale aliyelazwa hospitalini hapo.
Kabla
ya kutembelea wagonjwa, Mhe. Rais Magufuli amekwenda Msasani Jijini Dar
es Salaam kumpa pole Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (JWTZ) Jen. Venance
Salvatory Mabeyo ambaye amefiwa na mwanae Nelson Venance Mabeyo
(aliyekuwa Rubani) ambaye amefariki dunia leo asubuhi baada ya ndege
aliyokuwa akiiendesha kupata ajali muda mfupi baada ya kuruka kutoka
uwanja mdogo wa ndege wa Seronera Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara.
Mapema leo asubuhi, Mhe. Rais Magufuli ameongoza kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
23 Septemba, 2019
No comments:
Post a Comment