Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria imeipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu
– Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kwa mikakati iliyoweka katika
kuwajengea uwezo vijana kujiajiri na uwezeshwaji kiuchumi kwa vijana
kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana “Youth Development Fund” na Mikopo
kupitia mapato ya ndani ya halmashauri.
Akizungumza
wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya vijana katika Mkoa wa Morogoro,
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Najma
Giga ameipongeza Serikali kwa mikakati iliyokuja nayo katika kutatua
changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana kwa kuwajengea mazingira
wezeshi na yanayowahamasisha kuanzisha miradi mbalimbali ya kiuchumi.
Wajumbe
wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria wakiangalia kitanda
kilichotengenezwa na Kikundi cha Vijana cha Faraja Carpentry kilichopo
Mkoani Morogoro. (Wa tano kutoka kulia) ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri
Mkuu Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde. (Wa nne kutoka
kushoto) ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria
Mhe. Najma Giga.
|
“Matokeo
ya utekelezaji wa mikakati hiyo tumeona kwa kiasi kikubwa imewawezesha
vijana kutambua taratibu rasmi za kupata mikopo yenye riba nafuu na
ambayo imewasaidia kuazisha miradi ya kiuchumi,” alisema Mheshimiwa
Giga.
Aliongeza
kuwa Serikali iendelee kutenga bajeti zaidi ya uwezeshwaji wa vikundi
vya vijana kwa kuwa vina tija na vinapunguza tatizo la ajira kwa vijana
kwa kiasi kikubwa.
Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Najma Giga
akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo pamoja na watendaji wa halmashauri
ya Morogoro walipotembelea Mkoa huo kwa lengo la kukagua miradi ya
vijana walionufaika na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana na Mikopo kupitia
mapato ya ndani ya halmashauri.
Sambamba
na hayo Kamati hiyo iliitaka Ofisi ya Waziri Mkuu kuendelea kutoa
maelekezo katika halmashauri zote kuelimisha vijana zaidi ili waweze
kutambua taratibu za kupata mikopo kupitia mfuko wa maendeleo ya vijana
na asilimia 10 ya mikopo ambayo utolewa kwa Vijana 4%, Wanawake 4% na
Wenye Ulemavu 2% kupitia mapato ya ndani ya halmashauri.
Akitoa
maelezo ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde
ameihakikishia Kamati ya Bunge kwamba Serikali itaendelea kuviwezesha
kiuchumi vikundi vya vijana katika mkakati wa kuhamasisha vijana
kujiajiri lakini pia kuwajengea uwezo wa kiuchumi vijana ili nao pia
washiriki kikamilifu katika mnyororo mzima wa uchumi wa viwanda ambapo
matarajio ni kwamba ifikapo mwaka 2025 zaidi ya asilimia 40 ya nguvukazi
iwe imeajiriwa kwenye sekta ya viwanda.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira
Mhe. Anthony Mavunde akielezea jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya
Katiba na Sheria walipofanya ziara ya kukagua miradi ya vijana Mkoani
Morogoro. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba na
Sheria Mhe. Najma Giga
“Serikali
iliazisha mfuko wa maendeleo ya vijana na programu mbalimbali ili
kuwawezesha wananchi hususan vijana kuweza kupata mahitaji ya mitaji ya
kuanzisha shughuli za kiuchumi zitakazo waingizia kipato,” alisema
Mavunde
Akitolea
mfano mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vijana kutumia teknolojia ya
kitalu nyumba ni mkakati mzuri ambao Serikali imekuja nao katika kutatua
tatizo la ajira kwa vijana kupitia sekta ya kilimo.
Kiongozi
wa Kikundi cha Vijana cha Mazimbu Agro Enterprise Bw. Alexander Jokonia
(wa nne kutoka kushoto) akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge
ya Katiba na Sheria walipowatembelea katika eneo lao la kazi kujionea
miradi ya kiuchumi inayofanywa na vijana katika Mkoa wa Morogoro.
Kikundi hicho kimenufaika na mkopo kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Vijana
unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Najma Giga
wakipitia taarifa ya mradi wa vijana wa Mazimbu Agro Enterprise.
(Katikati) ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi,
Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde.
Aidha,
Naibu Waziri Mavunde aliwahamasisha vijana kuandaa maandiko ambayo
yataelezea shughuli zenye tija wanazotaka kuzifanya katika kujileta
maendeleo ili waweze kupata mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya vijana
na Mikopo kupitia mapato ya ndani ya halmashauri itakayowasaidia
kuendesha shughuli zao.
Kwa
nyakati tofauti vijana wa Mkoa wa Morogoro wameishukuru Serikali kwa
uwezeshaji kupitia Mfuko wa maendeleo ya vijana na kuomba kuwezeshwa
zaidi ili kukidhi matarajio yao ya uanzishwaji wa viwanda katika kuunga
mkono jitihada za Serikali ya Tano katika uchumi wa viwanda.
Kiongozi
wa Kikundi cha Vijana cha Faraja Carpentry Bw. James Luwanda akionyesha
vitendea kazi wanavyotumia kutengeneza bidhaa zao. Kushoto ni Naibu
Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde.
(Wa pili kutoka kushoto) ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya
Katiba na Sheria Mhe. Najma Giga.
Wajumbe
wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria wakipata maelezo kutoka kwa
Kiongozi wa Kikundi cha Vijana cha Faraja Carpentry Bw. James Luwanda
namna wanavyobuni urembo (nakshi) katika meza ya chakula “Dinning
Table”.
No comments:
Post a Comment