Naibu waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameagiza timu ya Wataalamu wa
sekta ya ardhi iende katika tarafa ya Ingwe wilaya ya Tarime mkoa wa Mara
kwenda kubainisha mipaka ya kiutawala kwa ajili ya kutatua mgogoro wa muda
mrefu wa mipaka baina ya kijiji cha Mrito na Kibaso.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula |
Uamuzi huo Dkt Mabula
unafuatia jitihada za kutafuta suluhu ya mgogoro huo kwa njia ya mazungumzo
kati ya pande hizo mbili kukwama kutokana na kila upande kudai sehemu ya eneo
la kijiji cha Mrito liko upande wake.
Kwa mujibu wa Naibu
Waziri wa Ardhi, timu hiyo itahusisha wataalamu wa sekta hiyo kutoka ofisi ya
Ardhi Kanda ya Simuyu na wale wa ofisi ya mkoa wa Mara badala ya Tarime kufuatia baadhi yao kutuhumiwa
na pande hizo kuwa wamekuwa wakichangia
kuendelea kwa mgogoro baina ya vijiji hivyo.
Naibu Waziri wa Ardhi Alisema,
baada ya kukamilika kwa zoezi la kubainisha mipaka ya kiutawala taarifa yake
itawasilishwa kwa mkuu wa wilaya ya Tarime mkoani Mara Mtemi Msafiri ambaye
jumanne ijayo tarehe 22 Oktoba 2019 atatakiwa kuwaeleza wananchi wa vijiji hivyo
makubaliana yatakayofikiwa kwa nia ya kumaliza mgogoro huo.
Awali kulikuwa na
mabishano makali ya pande zinazopingana katika mgogoro huo ambapo wananchi wa
kijiji cha Mrito walidai wenzao wa Kibaso wamevamia eneo lao huku wale wa
Kibaso wakidai sehemua ya eneo linalodaiwa ni la Mrito ni la kwao.
Joseph Mangure
aliyekuwa Mwenyekiti wa kijiji cha Mrito tangu mwaka 2009 hadi 2014 alisema
sehemu ya eneo la kijiji cha Mrito inayodaiwa na wananchi wa Kibaso kuwa ni la
kwao siyo sahihi kwa kuwa kijiji cha Mrito kina nyaraka zote zinazoonesha mipaka
yake tofauti na wananchi wa Kibaso alioeleza kuwa hawana Nyaraka zinazoonesha uhalali
wa eneo lake.
Naye Diwani wa Kata ya Bihanja
wilayani Tarime Mustafa Masiani alieleza kuwa suluhu pekee ya mgogoro baina ya
vijiji hivyo ni kwa viongozi wa serikali za vijji husika kukaa pamoja na na kutafuta suluhu ya mgogoro na kubainisha
kuwa tatizo lililopo ni baadhi ya wananchi kuufanya uongozi wa vijiji kama
uongozi wa Koo.
No comments:
Post a Comment