Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta
utepe pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi
Isaack Kamwelwe kuashiria ufunguzi wa barabara ya Sumbawanga-Kanazi km
75 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami katika sherehe
zilizofanyika Kanazi mkoani Rukwa.
Rais Dkt. John Magufuli
tarehe 08 Oktoba, 2019 amefungua barabara ya Sumbawanga – Kanazi, ameweka jiwe
la msingi la ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Nkasi, amefungua Kituo cha Afya
Nkomolo na kuzindua uandikishaji katika orodha ya wapiga kura wa Mamlaka za
Serikali za Mitaa (2019)
ulioanza leo hapa nchini.
Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS)
Mhandisi Patrick Mfugale amesema ujenzi wa barabara ya Sumbawanga – Kanazi
yenye urefu wa kilometa 75 ambayo ni sehemu ya barabara ya Sumbawanga – Kanazi
– Mpanda yenye urefu wa jumla ya kilometa 245, uliogharimu shilingi Bilioni
100.7 umekamilika mwaka 2017 na barabara hiyo imekabidhiwa mwaka 2018.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na wananchi wa Kanazi mara baada ya kufungua barabara ya
Sumbawanga-Kanazi km 75 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami
katika sherehe zilizofanyika Kanazi mkoani Rukwa.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
Mkewe Mama Janeth Magufuli watano kutoka kulia walioshika utepe, Wabunge
wa mkoa wa Rukwa, Kamati ya Miundombinu, Mawaziri, akakata utepe
kufungua barabara ya Sumbawanga-Kanazi km 75 iliyokamilika kujengwa kwa
kiwango cha lami katika sherehe zilizofanyika Kanazi mkoani Rukwa.
Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Mhe. Selemani Jafo amesema Hospitali ya Wilaya ya Nkasi ambayo inajengwa kwa
ghamara ya shilingi Bilioni 1 na Milioni 500 ni moja kati ya hospitali mpya 69
zenye hadhi ya Wilaya zinazojengwa hapa nchini na kwamba katika bajeti ya mwaka
huu Serikali imetenga fedha za ujenzi wa Hospitali zingine 27 na kufanya jumla
ya hospitali zenye hadi ya wilaya zilizojengwa katika Awamu ya tano kufikia 96.
Sehemu ya Barabara ya Sumbawanga-Kanazi km 75 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami kama inavyoonekana.
Kituo cha Afya
Nkomolo kilichojengwa kwa gharama ya shilingi Milioni 500 tayari kimeanza kutoa
huduma na kimefunguliwa kwa niaba ya vituo vingine 10 vya Mkoa wa Rukwa ambavyo
vimejengwa katika Wilaya zote za Mkoa huo.
Mhe. Rais Magufuli
amezindua uandikishaji katika orodha ya wapiga kura wa Mamlaka za Serikali za
Mitaa ambao umeanza nchini kote leo tarehe 08 Oktoba, 2019 hadi tarehe 14 Oktoba,
2019 na amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ili waweze
kushiriki kupiga kura na kuchagua viongozi wanaowafaa katika Uchaguzi wa
Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 24 Novemba, 2019.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua
moja ya chumba cha hospitali ya Wilaya ya Nkasi mara baada ya kuweka
jiwe la msingi.
Akizungumza katika
mkutano wa hadhara Mjini Namanyere, Mhe. Rais Magufuli amewapongeza wananchi wa
Nkasi na Mkoa mzima wa Rukwa kwa maendeleo makubwa ya kuimarishwa kwa
miundombinu ya barabara, hospitali, vituo vya afya, umeme na huduma nyingine na
amewahakikishia kuwa Serikali itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya
kuboresha zaidi maisha ya wananchi.
Mhe. Rais Magufuli
ambaye akiwa njiani kutoka Sumbawanga kwenda Namanyere Wilayani Nkasi
amesalimiana na wananchi wa Ntendo, Nkundi, Milundikwa, Kasu na Chala amewataka
wataalamu wa Wizara ya Maji kubadilika na kubuni mbinu za kutatua matatizo ya
maji yanayowakabili wananchi, ikiwemo kuvuna maji ya mvua katika mabonde
yaliyopo katika maeneo mengi yenye tatizo la ukosefu wa maji.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua
gril la dirisha la moja ya chumba cha hospitali ya Wilaya ya Nkasi mara
baada ya kuweka jiwe la msingi.
Akiwa katika mkutano
huo wa hadhara, Mhe. Rais Magufuli amesikiliza kilio cha Mama Mjane aitwaye
Felista Mkombo ambaye aliibiwa ng’ombe 25 lakini Askari Polisi walimwachia
mtuhumiwa na baadaye akafanikiwa kutoroka, ambapo ameagiza Polisi wakiongozwa
na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa Mathias Nyange na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi
Mhe. Said Mtanda kumlipa Mama huyo shilingi Milioni 15 kama fidia kutokana na
kutoshughulikia vizuri tatizo lake.
Mhe. Rais Magufuli
ameelezea kusikitishwa na namna viongozi wa Mkoa wa Rukwa wasivyoshughulikia
kero za wananchi na mara baada ya kumaliza hotuba yake ameagiza viongozi hao
wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Joachim Wangabo kubaki mkutanoni hapo ili
wasikilize kero za wananchi wote waliokuwa wamebeba mabango na kumpatia taarifa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kituo cha Afya cha Nkomolo Nkasi mkoani Rukwa.
“Tatizo la Mkoa huu viongozi hamshughulikii
kero za wananchi, kila mahali wananchi wanalalamika na hata hapa kuna mabango
mengi ya wananchi wenye kero mbalimbali, sasa nataka mbaki hapa muwasikilize na
mnipe taarifa” ameagiza Mhe. Rais Magufuli.
Amempongeza Mbunge
wa Nkasi Mhe. Ally Kessy kwa jinsi anavyoshughulikia kero za wananchi na kufuatilia
miradi ya maendeleo na amemuahidi kuwa Serikali itachukua hatua kutatua kero
hizo pamoja kuwachukulia hatua watumishi wa umma ambao wamekuwa wakishirikiana
na wakandarasi kuiba fedha za miradi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
Mkewe Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, Waziri wa
Tamisemi Selemani Jafo, Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugora, Mbunge wa
Nkasi Ally Keissy, akikata utepe kuashiria ufunguzi kituo cha Afya cha
Nkomolo Nkasi mkoani Rukwa.
Kesho tarehe
09 Oktoba, 2019, Mhe. Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth
Magufuli ataendelea na ziara yake ambapo atafungua barabara ya Kanazi – Kizi –
Kibaoni.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza
Mbunge wa Nkasi Ally Keissy mara baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi
wa Hospitali ya Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
Mkewe Mama Janeth Magufuli, wakiangalia zoezi la uandikishaji la wapiga
kura wa Viongozi wa Serikali za mitaa Nkasi mkoani Rukwa.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na mwanachi wa Nkasi Albina Kasanya (74) ambaye alikuwa amemaliza
kujiandikisha katika kituo cha Hospitali ya Wilaya ya Nkasi mkoani
Rukwa.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na Wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari wa Nkasi waliokuwa
pembezoni mwa majengo ya hospitali ya Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa.
Sehemu ya Majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Nkasi ambayo ipo katika hatua za mwisho kukamilika Nkasi mkoani Rukwa.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akimsikiliza Bi Paskalia Mikael mara baada ya kusimama katika kijiji cha
Chala mkoani Rukwa wakati akielekea Nkasi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na wanachi wa Chala mara baada ya kuwasili kijijini hapo.
Wanafunzi
wa Kasu Sekondary Wakishangilia mara baada ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwasili katika kijiji
hicho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanachi wa Kasu mkoani Rukwa. PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment