|
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) na Waziri wa
Nishati, Dkt Medard Kalemani (kushoto) wakipongezana mara baada ya Waziri Mkuu,
kuweka jiwe la msingi katika mradi wa upanuzi wa kituo cha kupoza umeme
kilichopo Misuna, wilayani Singida, Mkoa wa Singida. Kituo hicho kinaongezewa
nguvu ya umeme kutoka kV 220 hadi kV 400.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameweka Jiwe la
Msingi katika mradi wa upanuzi wa vituo
vinne vya kupoza umeme vinavyoongezewa nguvu ya umeme kutoka kV 220 hadi kV 400
katika mikoa ya Iringa, Dodoma, Singida na Shinyanga.
Hafla hiyo ilifanyika tarehe 5 Oktoba, 2019 mkoani
Singida na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Nishati, Dkt
Medard Kalemani, Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),
Mussa Sima, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt Rehema Nchimbi, Katibu Mkuu, Wizara ya
Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Nishati na Madini, Dunstan Kitandula. | |
|
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akifunua kitambaa
kuashiria uwekaji jiwe la msingi katika mradi upanuzi wa kituo cha kupoza
umeme kilichopo Misuna, wilayani Singida, Mkoa wa Singida. Kituo hicho
kinaongezewa nguvu ya umeme kutoka kV 220 hadi kV 400
Viongozi wengine waliohudhuria ni Kamishna
Msaidizi wa Umeme, Mhandisi Innocent Luoga, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt
Tito Mwinuka, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini(REA),
Mhandisi Amos Maganga na watendaji kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)
na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA).
Waziri Mkuu, alisema kuwa, tukio hilo linaashiria
pia uzinduzi wa mradi wa njia ya kusafirisha umeme mkubwa wa msongo wa kilovoti
400 kutoka Singida, Manyara, Arusha, Namanga hadi Isinya nchini Kenya (KTPIP) ambao
tayari upo kwenye hatua za ujenzi.
Aliongeza kuwa, kukamilika kwa miradi hiyo
kutawezesha gridi ya Taifa kuwa na uwezo mkubwa wa usafirishaji umeme na kuwezesha
nchi kuwa na umeme wa uhakika, unaotosha mahitaji na unaotabirika. | |
|
Baadhi ya wafanyakazi katika mradi wa upanuzi wa kituo
cha kupoza umeme kilichopo Misuna, wilayani Singida, Mkoa wa Singida
wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (hayupo pichani) kabla ya kuweka jiwe
la msingi kwenye kituo hicho kinachoongezewa
nguvu ya umeme kutoka kV 220 hadi kV 400. |
|
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kushoto) akisalimiana
Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua mara baada ya kuwasili
katika eneo la Misuna wilayani Singida ili kuweka jiwe la msingi katika mradi
wa upanuzi wa kituo cha kupoza umeme. Kituo hicho kinaongezewa nguvu ya umeme
kutoka kV 220 hadi kV 400. |
|
Baadhi ya viongozi, wataalam kutoka Wizara ya Nishati,
TANESCO, Wakala wa Nishati Vijijini (REA), wakandarasi pamoja na wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
(hayupo pichani) kabla ya kuweka jiwe la msingi kwenye kituo cha kupoza umeme
kilichopo Misuna, wilayani Singida, Mkoa wa Singida. Kituo hicho kinaongezewa
nguvu ya umeme kutoka kV 220 hadi kV 400. |
|
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia, mbele) na Waziri wa
Nishati, Dkt Medard Kalemani (kushoto, mbele) na viongozi mbalimbali wakipiga
makofi mara baada ya Waziri Mkuu kuweka jiwe la msingi katika mradi wa upanuzi
wa kituo cha kupoza umeme kilichopo Misuna, wilayani Singida, Mkoa wa Singida. Kituo
hicho kinaongezewa nguvu ya umeme kutoka kV 220 hadi kV 400. |
Alisema, Serikali inaendelea na jitihada za
utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya uzalishaji, usafirishaji na usambazaji
umeme ukiwemo mradi wa umeme wa Julius Nyerere (MW 2115) kwani lengo ni kuwa na
megawati 10,000 ifikapo mwaka 2025 na kusambaza umeme kwenye maeneo yote nchini.
Waziri Mkuu, vilevile aliipongeza Wizara ya
Nishati, TANESCO na REA kwa usimamizi thabiti wa miradi mbalimbali ya nishati
ikiwemo ya usambazaji umeme vijijini ambapo ameeleza kuwa hadi kufikia mwezi
Septemba mwaka huu jumla ya Vijiji 8,102 vimesambaziwa umeme kati ya vijiji
12,268.
Awali, Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani
alieleza kuwa mradi wa upanuzi wa vituo hivyo vya kupoza umeme ni wa Awamu ya
Pili kwani Awamu ya kwanza ilijumuisha ujenzi wa njia kuu ya kV 400 kutoka
Iringa hadi Shinyaga, pamoja na upanuzi wa vituo vya kupoza umeme kwa msongo wa
Kv 220 kwenye miji ya Iringa, Dodoma, Singida na Shinyanga na ulikamilika
Disemba 2016.
Aliongeza kuwa mradi huo wa awamu ya kwanza
ulisambaza umeme kwenye vijiji 121 vilivyopitiwa na miundombinu ya umeme na kwa
mradi huu wa Awamu ya Pili, jumla ya vijiji 19 vitakavyopitiwa na miundombinu
ya umeme kutoka Singida, Manyara hadi Arusha vitasambaziwa umeme.
Alisema kuwa gharama zitakazotumika kwenye ujenzi
wa vituo hivyo vinne vya kupoza umeme ni Dola za Marekani milioni 120 na Kituo cha Singida kinatarajiwa kukamilika
mwezi Februari mwaka 2020. Na Teresia Mhagama, WN
No comments:
Post a Comment