Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Oktoba 20, 2019 ameondoka chini kwenda
Urusi ambako atamwakilisha Rais Dkt.John Pombe Magufuli katika Mkutano
wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika na Urusi. Pichani, Waziri Mkuu
akisalimiana na Spika wa Bunge Job Ndugai kwenye Uwanja Ndege wa Julius
Nyerere kabla ya kuondoka. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu anahudhuria mkutano huo kwa niaba ya
Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli.
Mkutano huo
utakaoendeshwa chini ya uenyekiti wa pamoja (Co-chaired) wa Rais wa Shirikisho
la Urusi, Vladimir Putin, na Rais wa Misri, Abdel Fattah el-Sisi, ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), unalenga kurejesha na kuimarisha uhusiano
baina ya mataifa ya Afrika na Urusi ambao uliyumba baada ya kusambaratika kwa “Union
of Soviet Socialist Republic” (USSR) mwaka 1991.
Mkutano huo
wa Wakuu wa Nchi na Serikali utafanyika katika sehemu mbili, ambazo ni
Kongamano la Biashara (Russia Business Forum) linalotarajiwa kufanyika Oktoba 23,
na Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa Nchi za Urusi na Afrika uliopangwa kufanyika Oktoba
24, 2019.
Waziri Mkuu atashiriki
kwenye mikutano yote miwili.
|
No comments:
Post a Comment