Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge,akisisitiza jambo kwa waandishi
wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake wakati akitoa taarifa kuhusiana
na ziara ya kikazi ya Rais Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli,itakayoanza
kesho tarehe 21 hadi Novemba 25,mwaka huu jijini Dodoma,upande wa kulia
ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe.Patrobasi Katambi na kushoto ni Katibu
Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Kessy Maduka.
Rais
Dk John Magufuli anatarajia kuanza ziara ya kikazi Mkoani Dodoma Novemba
21,2019 ambapo katika ziara hiyo ataweka jiwe la msingi katika miradi
mbalimbali ya mandeleo ikiwemo Hospitali ya Uhuru, Stendi Kuu ya mabasi
pamoja na soko kuu Dodoma.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Binilith Mahenge
amesema ziara hiyo itaanza Novemba 21 mwaka huu ambapo Rais Magufuli
atakuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya kumi (10) ya Chuo Kikuu cha
Dodoma – UDOM yatakayofanyika kwenye ukumbi wa Chimwaga, Chuoni hapo.
Dk
Mahenge amesema Novemba 22, 2019 Rais ataweka mawe ya msingi kwenye
miradi ya Hospitali ya Uhuru, Wilayani Chamwino, ujenzi wa nyumba 118 za
Askari Polisi katika maeneo ya FFU Nzuguni na Medeli East, Ujenzi wa
Stendi Kuu ya mabasi iliyopo Nzuguni.
Miradi
mingine ni Soko Kuu linalojengwa katika eneo la Nzuguni pamoja
kuzungumza na Wananchi katika mkutano wa hadhara utakaofanyika katika
stendi ya mabasi Nzuguni.
“Jumatatu
Novemba 25, 2019 mheshimiwa Rais ataweka mawe ya msingi kwenye miradi
ya ujenzi wa Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi Tanzania Kikombo, ujenzi
wa Ofisi ya Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji na Ujenzi wa jengo la
Makandarasi katika eneo la National Capital City.
Ziara
hii ya mheshimiwa Rais (John Magufuli) kwetu ni fursa ya kumwonesha
hatua tulizofikia katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo aliyotupatia
na kupokea maelekezo ya namna ya kusonga mbele kwa uhakika katika hatua
mbalimbali za utekelezaji wake,” Amesema Dk Mahenge. Chanzo MichuziBlog
No comments:
Post a Comment