Waratibu wa
Mfumo wa Taarifa za Utoaji wa Huduma za Afya (MTUHA) nchi wametakiwa
kuimarisha upatikanaji wa takwimu sahihi za sekta ya afya katika maeneo
yao ya kazi.
|
Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali.Dkt. Saitole Laizer akifungua kikao kazi
cha waratibu wa mfumo wa taarifa wa ufuatiliaji wa huduma za afya wa
mikoa na halmashauri unaofanyika chuo cha mipango jijini Dodoma | |
Rai hiyo imetolewa leo na Kaimu
Mganga Mkuu wa Serikali ambaye pia ni mkurugenzi wa mafunzo na
rasiliamali watu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Saitole Laizer wakati akifungua kikao kazi cha waratibu
MTUHA wa mikoa na halmashauri Tanzania kinachofanyika jijina hapa.
Dkt.
Saitole amesema kuwa Wizara imeboresha mfumo wa takwimu kulingana na
mahitaji ya sasa na zinaingizwa na kuchanganuliwa kwa kutumia program
maalum ya kompyuta katika ngazi ya wilaya ijulikanayo kama ‘District
health information software-DHIS 2’, hivyo ana imani watasimamia na
kuratibu kwa umakini.
|
Waratibu hao wakimsikiliza mgeni rasmi(hayupo pichani) wakati wa
ufunguzi wa kikao kazi hicho.kinachofanyika chuo cha mipango Dodoma |
|
Waratibu wa mfumo wa taarifa wa ufuatiliaji wa huduma za afya wakiwa kwenye makundi wakiandaa mpango kabambe wa utekelezaji |
“Matarajio ya wizara ni
kuwa takwimu zinazopatikana kutoka katika program hii zitakuwa sahihi
na mtatengeneza orodha ya kielekroniki ya vituo vya kutolea huduma za
afya ili kusaidia katika mipango na kutoa maamuzi katika Sekta ya
Afya”.
Vile vile Dkt. Saitole aliwataka
waratibu hao kuweka mipango kabambe ili kuhakikisha mrejesho wa zoezi la
uhakiki wa ubora wa takwimu za afya uliofanywa na Mkaguzi Mkuu wa
Ndani wa Serikali pamoja na kutoa mafunzo ya mrejesho katika meza
maalum zitakazoandaliwa ili kutoa msaada wa watumishi ambao wanahitaji
kujifunza,kupata ufafanuzi au kuuliza na kupata majibu ya masuala ya
MTUHA yanayowasumbua katika maeneo ya kazi .
|
Mwenyekiti wa waratibu hao Dkt. Ally Msoke akitoa neno la shukrani wakati wa ifunguzi wa mkutano huo |
|
Kaimu mkurugenzi msaidizi ufuatiliaji na tathimini kutoka wizara ya afya Tumainiel Macha akiongea kwenye kikao kazi hicho |
|
Picha ya pamoja ya watumishi kutoka wizara ya afya na OR-TAMISEMI na mgeni rasmi |
Hata
hivyo aliwataka waratibu hao kuhakikisha halmashauri zinatenga fedha
kwa ajili ya MTUHA katika mpango kabambe wa halmashauri(CCHP) na timu
za za afya za mikoa na halmashauri na Wadau wa Maendeleo wanashiriki
kikamilifu katika kuimarisha upatikanaji wa takwimu sahihi za Sekta ya
Afya.
Mfumo wa taarifa za utoaji wa huduma za
afya nchini umesaidia kuwezesha sekta ya afya kupata takwimu sahihi na
kwa wakati zinazowezesha kufanya maamuzi sahihi katika kupanga na
kutekeleza malengo yake ili hatimaye kufikisha huduma bora kwa wananchi
kutoka asilimia 43 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 85 mwaka 2019. Na. Catherine Sungura, Dodoma
No comments:
Post a Comment