Waziri wa Ardhi Nyumba ,Maji na
Nishati Salama Aboud Talib akifungua kitambaa kuashiria uwekaji wa Jiwe
la Msingi Barabara yenye urefu wa Kilomita 6.3 ya Koani-Jumbi Wilaya ya
Kati Unguja .Ikiwa ni shamra shamra za miaka 56 ya Mapinduzi ya
Zanzibar.
Barabara ya kilomita 6.3 ya Koani
-Jumbi iliowekwa Jiwe la msingi na Waziri wa Ardhi Nyumba ,Maji na
Nishati Salama Aboud Talib.Ikiwa ni shamra shamra za miaka 56 ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi
,Mawasiliano na Usafirishaji Mustafa Aboud Jumbe akitoa maelezo ya
Kitaalamu kuhusu Ujenzo wa Barabara katika hafla ya uwekaji wa Jiwe la
Msingi Barabara yenye urefu wa Kilomita 6.3 ya Koani-Jumbi Wilaya ya
Kati Unguja .Ikiwa ni shamra shamra za miaka 56 ya Mapinduzi ya
Zanzibar.
Naibu Waziri wa Ujenzi
,Mawasiliano na Usafirishaji Mohamed Ahmed Salum akitoa hotuba ya
makaribisho kwa Mgeni Rasmi katika hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi
Barabara yenye urefu wa Kilomita 6.3 ya Koani-Jumbi Wilaya ya Kati
Unguja .Ikiwa ni shamra shamra za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Waziri wa Ardhi Nyumba ,Maji na
Nishati Salama Aboud Talib akitoa hotuba ya uwekaji wa Jiwe la Msingi
Barabara yenye urefu wa Kilomita 6.3 ya Koani-Jumbi Wilaya ya Kati
Unguja .Ikiwa ni shamra shamra za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.PICHA N A YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.
…………………..
Na Kijakazi Abdalla,Maelezo .
Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar imesema itaendelea kuzijenga barabara kwa kiwango cha
lami barabara ambazo hazijajengwa katika Mkoa wa Kusini ili kuhakikisha
wananchi wanaondokana na usumbufu.
Hayo ameyasema
Waziri wa Ardhi,Nyumba,Maji na Nishati Salama Aboud Talib mara baada ya
kuweka jiwe la msingi Barabara ya Koani Jumbi ikiwa ni shamra shamra za
Sherehe za miaka 56 Mapinduzi matukufu ya Januari 12.
Amesema katika
kipindi cha miaka 56 ya Mapinduzi Zanzibar mtandao wa barabara za Unguja
na Pemba umeimarika hivyo jitihada zitachukuliwa ili kuhakisha
zinakuwa za kiwango kinachohitajika.
Aidha amesema
kuimarika kwa miundo mbinu ya barabara ni moja ya jitihada
zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika awamu ya saba
ya uongozi wa Dkt Ali Mohamed Shein.Hata hivyo Waziri
Salama aliwataka wakandarasi kuwa makini wanapojaza mikataba ya ujenzi
wa barabara ili kuhakikisha ujenzi unamalizika kwa wakati ambao
umepangwa.
Vilevile
amewataka Madereva wa vyombo vya moto wanaotumia barabara wawe wangalifu
na kufuata alama ambazo zilizokwekwa ili kuondoa ajali zisizotarajiwa.Pia amewata
wananchi wa Zanzibar kuepuka kujenga katika maeneo ya hifadhi ya
barabara ili kuondosha usumbufu na kuepuka kuvunjia pale utanuzi
unapohitajika kufanywa.
Nae Katibu Mkuu
Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Mustafa Abuod Jumbe amesema
jitihda za kuimarisha miundo mbinu ya barabara zinaimarika kwa
kuhakisha wananchi wa mjini na vijijini wananapata huduma zenye uhakika.Aidha amesema
katika kuhakisha wananchi wanajengewa barabara zenye ubora tayari Wizara
imeweza kulipa fidia za vipando kwa wale wote waliongo’lewa.
Nae Mkandarasi
wa Kampuni ya Mecco Nassor Ramadhan Korowa amesema watahakikisha ujenzi
wa barabara ya Jumbi Koani unakamilika kwa wakati ili kuhakisha wananchi
wanaondokana na usumbufu.Ujenzi wa
Barabara wa Jumbi Koani unatarajiwa kuwa na urefu wa kilomita 6.3 na
upana wa mita 7 utagharimu Bilioni 5 na unatarajiwa kumaliza mwishoni
mwa mwezi wa Febuari mwaka huu.
No comments:
Post a Comment