Mkuu Wa
Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo amewaagiza wakuu wa shule zote za Sekondari katika Halmashauri hiyo kuacha
mara moja tabia ya kuwazuia wanafunzi wanaojiunga na kidato cha chanza kuanza
maso kutokana na kutokamilisha mahitaji yao ya shule.
Chongolo ametoa agizo hilo jana wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu kwa
ufaulu mzuri wa mitihani ya kumaliza elimu ya msingi mwaka 2019 iliyofanyika katika
viwanja vya Polisi Officers Mess.
“ Kuna
baadhi ya maeneo nimesikia kuna wakuu wa shule wanawarudisha nyumbani watoto
kwa sababu hawajakamilisha mahitaji yao, kama mtoto hana viatu, sijui nini
waache wasome wakati wazazi wao wanawatafutia mahitaji hayo, naomba nisikie
mwanafunzi amerudishwa nyumbani kwenye wilaya yangu” amesisitiza Chongolo.
Chongolo aliongeza kuwa mafanikio ya kufanya vizuri kwa wanafunzi wa darasa la
saba mwaka 2019 kwenye Halmashauri hiyo ni uthibitisho tosha unao onysesha
namna walimu, wazazi na wanafunzi katika wanashirikiana kikamilifu katika nyanja
ya elimu na hivyo kutoa wito kwa wazazi kuendeleza ushirikiano huo katika
usimamizi wa wanafunzi hususani kwenye masuala ya taaluma.
Alisema ofisi
ya Mkuu wa Wilaya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ilianzisha mkakati wa
ujenzi wa madarasa 100 ambapo kwa shule ya Sekondari ni madarasa 40 huku shule
ya msingi madarasa 60 lengo likiwa ni kuongeza tija katika taaluma na kupunguza
changamoto ya miundombinu inayoikabili shule hizo na kwamba jumla ya vyumba 24
vya madarasa kwa shule ya msingi zipo katika hatua ya ukamilishaji.
Mhe.
Chongolo alitumia nafasi hiyo kumpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo , Ndugu
Aron Kagurumjuli kwa usimamizi mzuri wa elimu na kwamba anatambua jitihada zake
za kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanapata elimu bure na kwamba anatimiza
kimamilifu majukumu na maagizo yanayotolewa na Rais Dk. John Magufuli.
Kwa upande
wake Mstahiki Meya wa Halmashauri hiyo, Benjamini Sita alisema kuwa hafla hiyo
ni mahususi kwa ajili ya kuwapongeza walimu kwa kuwa Halmashauri hiyo imekuwa
kwenye nafasi ya tatu kitaifa katika matokeo ya darasa la saba na kwamba inajipanga
kuhakikisha kuwa inashika nafasi ya kwanza kitaifa katika matokeo ya mtihani
ijayo.
Aidha Kaimu
Afisa elimu wa Halmashauri hiyo, Bi Chitegets Dominick alieleza kuwa mafanikio
hayo yametokana na uongozi mahiri wa Mstahiki Meya Benjanimi Sita, Mkurugenzi
Aron Kagurumjuli kwa kushirikiana na watendaji wa Idara ya Elimu na Idara
nyingine na hivyo kumhakikishia Mhe. Chongolo kuwa watahakikisha wanafanya
vizuri zaidi katika mitihani ijayo.
Aliongeza kuwa
Halmashauri hiyo imefanya vizuri katika mtihani wa darasa la saba mwaka 2019
kwa kuwapa ufaulu wa asilimia 97.17 ambapo imekuwa ya tatu kati ya Halmashauri
186 kitaifa kwa jumla ya wanafunzi waliosajiliwa kufanya mtihani huo walikuwa
12,619, wavulana 6,115 na wasichana 6,450, huku walioganya wakiwa 12,523
,wavulana 6,058 na wasichana 6,465.
No comments:
Post a Comment