Muonekano wa sehemu ya jengo Mradi wa Mradi wa ujenzi wa jengo la Ofisi za Tume hiyo zilizopo eneo la Njedengwa Jijini Dodoma tarehe 15 Februari, 2020. |
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Anthony
Mavunde (Mb) katikati, akifuatana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Mhe. Aeshi Khalfan Hilaly (Mb),
wakati kamati hiyo ilipokagua hatua za Mradi wa ujenzi wa jengo la Ofisi
za Tume ya Taifa ya Uchaguzi zilizopo eneo la Njedengwa Jijini Dodoma tarehe 15 Februari, 2020
Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeridhishwa na
utekelezaji wa maagizo iliyoyatoa mwezi Oktoba mwaka jana, kwa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC), ambapo iliitaka Tume hiyo kuhakikisha
inasimamia ukamilishwaji wa Mradi wa ujenzi kwa wakati wa ofisi za Tume
hiyo jijini, Dodoma kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
Akiongea mara baada ya kukagua hatua ya Mradi wa ujenzi wa jengo la Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi zilizopo eneo la Njedengwa Jijini Dodoma leo tarehe 15 Februari, 2020, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Mhe. Aeshi Khalfan Hilaly (Mb), amebainisha kuwa Kamati imeridhishwa na hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa ofisi za Tume hiyo kwa Jengo Kuu la Ofisi, Jengo la kutangazia matokeo na ghala la kuhifadhi vifaa.

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali,
wakifuatilia hoja za kikao na viongozi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kabla ya
kamati hiyo kukagua hatua za Mradi wa ujenzi wa jengo la Ofisi za Tume
ya Taifa ya Uchaguzi zilizopo eneo la Njedengwa Jijini Dodoma tarehe
15 Februari, 2020.
“Tunaipongeza serikali kwa hatua ilizozichukua
kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu katika kuhakikisha kuwa ujenzi wa Ofisi
hizi unakamilika kwa wakati, kimsingi ni nia njema kamati kutembelea
miradi ya serikali lakini tunapoona inafanya vizuri hatunabudi
kuipongeza na ni imani yetu kuwa kwa malengo iliyoyaweka mwezi Aprili
mwaka huu hatua kubwa ya utekelezaji itakuwa imefikiwa ” Amesisitiza,
Mhe. Aeshi
Kwa upande wake, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Anthony Mavunde (Mb) amefafanua kuwa tayari wanatekeleza maelekezo ya Mhe.Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ambaye ameitaka tume hiyo kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa Ofisi za Tume hizo kwa wakati ili shughuli za uchaguzi za mwaka huu zinafanyika kwenye majengo hayo.
Kwa upande wake, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Anthony Mavunde (Mb) amefafanua kuwa tayari wanatekeleza maelekezo ya Mhe.Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ambaye ameitaka tume hiyo kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa Ofisi za Tume hizo kwa wakati ili shughuli za uchaguzi za mwaka huu zinafanyika kwenye majengo hayo.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Anthony
Mavunde (Mb) kulia, akifuatana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Mhe. Aeshi Khalfan Hilaly (Mb),
katikati, na Mkurugenzi wa Uchaguz, Tume ya Taifa ya Uchaguzi , Wilson
Mahera, (kushoto) wakati kamati hiyo ilipokagua hatua za Mradi wa ujenzi
wa jengo la Ofisi za Tume hiyo zilizopo eneo la Njedengwa Jijini Dodoma tarehe 15 Februari, 2020.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Anthony
Mavunde (Mb) na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu
za Serikali, Mhe. Aeshi Khalfan Hilaly (Mb), pamoja na Mkurugenzi wa
Uchaguzi Tume ya Taifa ya Uchaguzi , Wilson Mahera, wakimsikiliza meneja
wa Mradi huo, Godwin Maro, wakati kamati hiyo ilipokagua hatua za
Mradi wa ujenzi wa jengo la Ofisi za Tume hiyo zilizopo eneo la
Njedengwa Jijini Dodoma tarehe 15 Februari, 2020.
“Kutokana
na mkandarasi mpya wa mradi huu ambaye ni SUMA JKT, Tumewahakikishia
wanakamati wa PAC, kuwa ifikapo mwezi Aprili mwaka huu mradi wa ujenzi
wa ofisi za Tume utakuwa umefikia hatua kubwa kwa kiwango cha kuruhusu
shughuli za Tume kuanza kuendeshwa katika majengo haya, ambapo litakuwa
ni jambo kubwa kwa kuwa katika historia tume hiyo haijawahi kuwa na
ofisi yake yenyewe”Amesisitiza Mhe. Mavunde.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Anthony
Mavunde (Mb) katikati na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Hesabu za Serikali, Mhe. Aeshi Khalfan Hilaly (Mb),kulia pamoja na
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Tixon Nzunda
wakifuatilia hoja za wabunge wakati wa kikao na viongozi wa Ofisi ya
Waziri Mkuu kabla ya kamati hiyo kukagua hatua za Mradi wa ujenzi wa
jengo la Ofisi za Tume hiyo zilizopo eneo la Njedengwa Jijini Dodoma
tarehe 15 Februari, 2020.
Baadhi ya viongozi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, wakifuatilia hoja za kikao
na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kabla ya
kamati hiyo kukagua hatua za Mradi wa ujenzi wa jengo la Ofisi za Tume
ya Taifa ya Uchaguzi zilizopo eneo la Njedengwa Jijini Dodoma tarehe
15 Februari, 2020.
Mkurugenzi wa Uchaguzi Tume ya Taifa ya Uchaguzi , Wilson Mahera,
akiwaeleza wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali
kabla ya kamati hiyo kukagua hatua za Mradi wa utekezaji wa Mradi wa
ujenzi wa jengo la Ofisi za Tume hiyo zilizopo eneo la Njedengwa Jijini
Dodoma tarehe 15 Februari, 2020.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Anthony
Mavunde (Mb) kulia, akiwaongoza wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Hesabu za Serikali kukagua hatua za Mradi wa ujenzi wa jengo la Ofisi
za Tume hiyo zilizopo eneo la Njedengwa Jijini Dodoma tarehe 15
Februari, 2020.
Muonekano wa sehemu ya jengo Mradi wa Mradi wa ujenzi wa jengo la Ofisi
za Tume hiyo zilizopo eneo la Njedengwa Jijini Dodoma tarehe 15
Februari, 2020.
Naye, Katibu Mkuu
Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Tixon Nzunda, amefafanua
kuwa hatua ya ujenzi wa mradi huo imeendelea vizuri baada ya kutekeleza
maagizo ya Mhe. Waziri Mkuu ya kuvunja Mkataba wa mkandarasi wa awali wa
mradi huo TBA na kusaini mkataba mpya na Kampuni ya Ujenzi ya Jeshi la
Kujenga Taifa- SUMA JKT CCL.
Awali akiwasilisha taarifa ya
utekelzaji wa Mradi wa Ujenzi wa Ofisi hiyo, Mkurugenzi wa Uchaguzi,
Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Wilson Mahera amebainisha kuwa Tume hiyo kwa
kushirikiana na Chuo kikuu- Ardhi na Kampuni ya Ujenzi ya Jeshi la
Kujenga Taifa- SUMA JKT CCL wanaouhakika mnamo mwezi Aprili mwaka huu
Tume hiyo itaanza kuendesha shughuli zake kwenye majengo hayo.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Anthony
Mavunde (Mb) kulia, akiwaongoza wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Hesabu za Serikali kukagua hatua za Mradi wa ujenzi wa jengo la Ofisi
za Tume hiyo zilizopo eneo la Njedengwa Jijini Dodoma tarehe 15
Februari, 2020.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni idara huru iliyoanzishwa mwaka 1993 kwa mujibu wa Ibara ya 74(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1997, ambapo kwa kipindi chote hicho tangu kuanzishwa kwake Tume hiyo haijawahi kumiliki Jengo lake lenyewe, hivyo mnano mwaka 2016, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli alikubali ombi la Tume hiyokujenga jingo lake.
No comments:
Post a Comment