|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan, akisalimiana na Balozi wa Sweeden Nchini Tanzania Mhe. Anders
Sjoberg wakati Balozi Sjoberg alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Jijini
Dar es salaam leo Januari 17,2020 kwa ajili ya kuzungumza na Makamu wa Rais. |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan, amesema Tanzania itahakikisha inazidi kuimarisha Uhusiano wake
na Sweeden katika Sekta ya Elimu, Uwekezaji wa Biashara, Utalii na Mazingira.
Makamu wa Rais ameyasema hayo leo Januari 17,2020 Ofisini
kwake Ikulu Jijini Dar Es Salaam wakati
alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Sweeden Nchini Tanzania
Mhe. Anders Sjoberg.
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan, akizungumza na Balozi wa Sweeden Nchini Tanzania Mhe. Anders
Sjoberg wakati Balozi Sjoberg alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Jijini
Dar es salaam leo Januari 17,2020. kushoto ni katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Mnyepe. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
) |
Aidha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amemhakikishia
Balozi Sjoberg kwamba Tanzania itaendeleza kukuza na kuimarisha Ushirikiano na
Uhusiano kati ya Nchi mbili hizi katika Sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Uwekezaji
wa kibiashara na Mazingira wakati Tanzania ikiwa mbioni kuelekea katika Uchumi
wa Viwanda.
Nae Balozi wa Sweeden Nchini Tanzania Mhe. Anders Sjoberg
amemuahidi Makamu wa Rais kwamba Nchi yake itashirikiana Bega kwa Bega na
Tanzania katika kuhakikisha kuwa Nchi mbili hizi zinafikia Malengo.
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia
Suluhu Hassan, akizungumza na Balozi wa Sweeden Nchini Tanzania Mhe. Anders
Sjoberg wakati Balozi Sjoberg alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Jijini
Dar es salaam leo Januari 17,2020. kushoto ni katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Mnyepe. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
) |
No comments:
Post a Comment