Naibu
Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akifungua mkutano wa wa wadau wa
kujadili mpango wa kuhamasisha matumizi ya Gesi Asilia nchini,
uliofanyika Jijini DSM.
Naibu
Waziri wa Nishati Subira Mgalu, amesema tayari Serikali imekamilisha
mpango wa awali wa kusambaza gesi kwenye Mikoa mitano ili kuhakikisha
kuwa Tanzania inatumia rasilimali hiyo inayochimbwa nchini katika
kuimarisha uchumi wa viwanda.
Mgalu alisema hayo wakati akifungua mkutano wa wadau wa kujadili mpango wa kuhamasisha matumizi ya Gesi Asilia nchini, uliofanyika Jijini DSM, Januari 17,2020.

Kamishna wa Petroli na Gesi, Adam Zuberi akizungumza na waandishi wa wabari wakati wa mkutano wa wadau wa kujadili mpango wa kuhamasisha matumizi ya Gesi Asilia nchini, uliofanyika Jijini DSM.
Mgalu
alisisitiza kuwa mpango huo ni matokeo ya utafiti wa miaka mitatu,
uliofanywa na Serikali kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa
la Japan (JICA). Aliitaja Mikoa hiyo kuwa ni Arusha, Dodoma, Tanga,
Kilimanjaro na Morogoro.
Aidha alieleza kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha mikoa yote Tanzania inapata nishati hiyo kwa matumizi mbalimbali.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) akipokea jarida maalumu lenye taarifa mbalimbali zinazohusu Shirika la Maendeleo la Japani, (JICA) kutoka kwa mwakilishi Shirika hilo, Naofumi Yamamura.

“Tanzania
tumegundua gesi asili yenye ujazo wa futi trilioni 57 hii sasa
tunaitengenezea mkakati wa matumizi yake, Kwa mijiibu wa takwimu
zinaeleza kuwa mpaka sasa gesi asilia inayochiimbwa chini inazalisha
Megawati 892.72 sawa na 57 % ya Megawati zote zinazozalishwa.
Aliweka wazi kuwa Gesi Asilia inatumika pia kwenye magari, tumeanza hapa Dar es Salaam ambapo magari takribani 200 yanatumia gesi na miundombinu ya kusambaza gesi hiyo inaendelea kuboreshwa ili kuwasogezea huduma watumiaji, na hii ndio maana hasa ya utafiti huu.
Naibu Waziri wa Nishati,Subira Mgalu( kulia) na Kamishna wa Petroli na Gesi wa Wizara ya Nishati, Adam Zuberi wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa wakati wa mkutano wa wadau wa kujadili mpango wa kuhamasisha matumizi ya Gesi Asilia nchini, uliofanyika Jijini DSM.

“Gesi asilia
inatusaidia pia kutunza mazingira hasa kwenye kupikia ambapo mpaka sasa
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), limesambaza miundombinu
ya gesi ya kupikia majumbani katika Mikoa ya Lindi, Mtwara, Dar es
Salaam na Pwani,” alisisitiza Mgalu.
Kuhusu matumizi ya gesi viwandani Mgalu alisema viwanda zaidi ya 50 vimeunganishwa na gesi asilia. “Huu ni mradi mkubwa Sana utakuwa wa muda mrefu pia hadi kufikia mwaka 2046 tangu kuanza kwa mradi huu mwaka 2017.
Naibu wa Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wawakilishi kutosha Shirika la Maendeleo la Japani ( JICA), Wakuu wa Taasisi ya Nishati na Uchumi kutoka Japani, baaadhi ya Viongozi Wakuu wa Wizara na Taasisi zilizochini yake, baada ya Naibu Waziri huyo kufungua mkutano wa wadau hao uliofanyika Jijini DSM.
Na Zuena Msuya, DSM
Kwa upande wake Kamishna wa Petroli na Gesi wa Wizara ya Nishati , Adam Zuberi alisema Tanzania ipo kwenye wakati sahihi hivyo jitihada za makusudi zinafanyika kufikisha gesi asilia kwenye mikoa yote Tanzania. “Tupo katika Muda muafaka wa utafiti huu unaolenga kuhakikisha kwamba Mikoa yote nchini inapata na kutumia gesi asilia kwa njia bora na sahihi,” alisema Zuberi.
Mshauri wa Taasisi ya Nishati na Uchumi kutoka Japan, Kensuke Kanekinyo alisema awamu ya kwanza ya mradi huo imetumia Dola Milioni mbili za Marekani kwa miaka mitatu.
Alisema gharama za mradi wote ni Dola milioni 250 zitakazotumika kupeleka gesi mikoa yote ya Tanzania.

No comments:
Post a Comment