Serikali imewataka watanzania kuwa watulivu,makini na
kupenda kuwa na subira ya kupata maelezo,maelekezo na ufafanuzi rasmi wa
Serikali pale kunakotokea jambo badala ya kukimbilia kwenye mitandao na uvumi
ili kuondoa kueneza hali ya taharuki kwa wananchi bila ya kuwa na uhakika.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Prof. Palamagamba John Kabudi ameyasema hayo wakati akitoa ufafanuzi juu ya
hali ya Watanzania waishio nchini China kutokana na kuzuka kwa virusi vya homa
ya corona nchini humo.
Prof. Kabudi amesema Tanzania ina wanafunzi takribani 4000
ambapo katika mji wa Wuhan kuna wanafunzi 400 na kwamba kwa mujibu wa Balozi wa
Tanzania Nchini China Balozi Mbelwa Kairuki ameihakikishia serikali kuwa mpaka
sasa hakuna mtanzania yeyote aliyeathiriwa ama kukumbwa na maradhi hayo.
Ameongeza kuwa Tanzania inaendelea kufuatilia kwa ukaribu
kujua maendeleo na hali za watanzania wanaoishi jimboni Wuhan na China kwa
Ujumla.
Aidha amewataka Watanzania kuwa makini na suala la kutoa
taarifa zisizo rasmi ama uvumu kwani kwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria za
Tanzania na kuwataka kuwa na Subira kupata taarifa rasmi kutoka serikalini.
No comments:
Post a Comment