Matokeo chanyA+ online




Saturday, January 18, 2020

WAZIRI KAMWELWE AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA UMOJA WA POSTA AFRIKA

Mwonekano wa Jengo Jipya la Makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika(PAPU)ambapo Waziri wa Ujezi,Uchukuzi na Mawasiliano Isack Kamwelwe ameweka jiwe la msingi  jijini Arusha katika kuadhimisha miaka 40 ya Umoja huo,Ujenzi wa Jengo hili unafanyika eneo la Philips kata ya Sekei

Mwonekano wa Jengo Jipya la Makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika(PAPU)ambapo Waziri wa Ujezi,Uchukuzi na Mawasiliano Isack Kamwelwe ameweka jiwe la msingi leo jijini Arusha katika kuadhimisha miaka 40 ya Umoja huo,Ujenzi wa Jengo hili unafanyika eneo la Philips kata ya Sekei

Mwonekano wa Jengo Jipya la Makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika(PAPU)ambapo Waziri wa Ujezi,Uchukuzi na Mawasiliano Isack Kamwelwe ameweka jiwe la msingi leo jijini Arusha katika kuadhimisha miaka 40 ya Umoja huo,Ujenzi wa Jengo hili unafanyika eneo la Philips kata ya Sekei
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi  Isack Kamwelwe (wa kwanza kushoto) akiweka rasmi jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la ofisi za makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika wakati wa Maadhimisho ya Miaka 40 ya Umoja huo yalifanyika leo tarehe 18/01/2020 jijini Arusha. Wanaoshuhudia tukio hilo kutoka kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawwasiliano Tanzania (TCRA) James Kilaba akitoa maelezo ya awali ya ujenzi wa Makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika(PAPU) ambao utajengwa kwa ubia katika ya PAPU na TCRA kwa niaba ya Serikali,aidha Kilaba amesema jengo hilo litakapokamilika litakuwa na ofisi mbalimbali,kumbi za mkutano,migahawa na huduma zingine mbalimbali na TCRA itakuwa na hisa asilimia 40.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) Dkt Jim Yonaz wa tatu toka kulia anayemfatia ni Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Waziri Kindamba katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi  ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika(PAPU) eneo la Philips Mkoani Arusha.

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  Dkt Maria Sasabo  katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi  ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika(PAPU) eneo la Philips Mkoani Arusha.

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  Dkt Maria Sasabo  akizungumza katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi  ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika(PAPU) eneo la Philips Mkoani Arusha.

No comments:

Post a Comment