Katibu Mkuu-Idara Kuu Afya Dkt. Zainab Chaula akiwaonesha kadi ya bima ya afya ya NHIF wakazi wa chato waliofika kwenye kongamano la wajasiliamali ambapo huduma za kupima afya zitatolewa bila malipo |
Wajasiliamali wote nchini wametakiwa kujikinga dhidi ya magonjwa ya milipuko wanapofanya biashara zao ndani na nje ya nchi
Elimu
hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Zainabu Chaula wilayani hapa kwenye
kongamano la wajasiriamali lililoandaliwa na Chama cha Wanataaluma
Waadventista Tanzania (ATAPE).
Katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula akisalimiana na viongozi wa kongamano hilo ambalo linatarajia kuwahudumia wananchi elfu tatu |
Amesema
kongamano hilo la wajasiriamali, ni tendo jema lenye baraka, "nimekuwa
kwenye ziara mikoa ya kigoma na kagera tukiangalia utayari wa nchi
hususan mipakani, namna tulivyojiandaa kukabiliana na magonjwa ya
mlipuko kama ebola na Corona".
Dkt.
Chaula amesema kongamano hilo limewakutanisha wajasiriamali wengi,
wajasiriamali wapo nchi nzima, mikoa halmashauri kata vitongoji hadi
vijijini kwahiyo ni fursa nzuri ya kupatiwa elimu juu ya dalili pamoja
na jinsi ya kujikinga na magonjwa ya milipuko kwakuwa wao wanakutana na
watu wengi na wanasafiri mara kwa mara.
"Nimefika
Chato usiku nikaelezwa kuhusu uwepo wa kongamano hili, nikasema
sitaondoka bila kufika hapa nizingumze nanyi, maana magonjwa ya milipuko
yameripotiwa kwenye maeneo mbalimbali hasa Ebola na Corona, nchini
mwetu hatuna magonjwa haya.
"Lakini
hatutaki kunyanyapaana, tunapaswa kuelimishana jinsi ya kuzuia na
kujikinga tusipate,Hivyo, mnapokutana mnapata mawazo mbalimbali, kwa
mfano kwenye kilimo tutalimaje, tutapandaje na tutavunaje na kupata soko
la uhakika, Tanzania tuna rutuba, maji ya kutosha hatupaswi kuwa na
njaa wala maradhi.
Wakazi wa chato waliofika kuhudhuria kongamano hilo litakalokuwa linatoa huduma za upimaji afya pamoja na huduma za kiroho |
"Aidha,Dkt.
Chaula alisema amefarijika kuelezwa kwamba kwenye kongamano hilo
watapata huduma ya kiroho (neno la Mungu) na kimwili (uchunguzi wa afya
na matibabu), ni sehemu nzuri kupata elimu namna ya kujikinga na
maradhi mbalimbali na jinsi ya kupata tiba.
Hata
hivyo aliwasisitiza wajasiriamali hao kukata bima ya afya "Gharama za
matibabu zimekuwa ghali, kongamano hili mmepata wadau wamewawezesha
lakini ili jambo hili liwe endelevu, ni muhimu kila mwananchi akate bima
ya afya ili aweze kupata huduma popote pale aendapo baada ya kumaliza
kongamano hili," alisisitiza.
Baadhi ya kwaya zilizofika kuhudumu kwenye kongamano la afya na wajasiriamali lililobeba kaulimbiu isemayo "Afya yako,Moyo Wako" |
Alisema kukata bima ya afya ni jambo la hiyari lakini la lazima kwani hakuna anayejua kesho itakuwaje.
Akizungumza,
mratibu wa Kongamano hilo, Dkt. Samwel Kikaro alisema wanatarajia kuona
na kutibu watu 3,000 ndani ya siku saba kuanzia jana.
Na.Catherine Sungura-Chato
No comments:
Post a Comment