 |
Mratibu wa kudhibiti Malaria mkoa wa Dar es
Salaam, Dokta Ford Chisongela akiangalia wataalamu wa Afya wa Halmashauri ya
Manispaa ya Kinondoni wakati wakikagua mtambo unaotumika kupulizia dawa kwa
ajili ya kuuwa wadudu wanaoambukiza homa inayosababishwa na Virusi vya Corona. |
 |
Wataalamu
wa Afya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni wakipuliza dawa katika vituo
vya mabasi ya endayo haraka katika eneo la Kinondoni Mkwajuni. | |
Halmashauri
ya Manispa ya Kinondoni kwa kushirikiana na wataalamu wa Afya wa Halmashauri hiyo
na mkoa wa Dar es Salaam wameendesha zoezi la upuliziaji dawa katika vituo vya
mabasi yaendayo haraka pamoja na vituo vya daladala ikiwa ni katika mkakati wa
kudhibiti maambukizi ya Vizuri vya
Corona.
Zoezi hilo limefanyika katika maeneo mbalimbali ikiwemo makazi
ya wananchi , maeneo ya kutolea huduma mbalimbali ikiwemo masoko sambamba na
kwenye mikusanyiko ya watu hususani Kanisani
na Msikitini.
Akizungumza na
waandishi wa habari, Mstahiki Meya wa Halmashauri hiyo, Mhe. Benjamini Sitta
amesema kuwa zoezi hilo linafanyika kwa lengo la kuuwa wadudu wanaosababisha maambukizi
ya Vizuri vya Corona (COVID 19) na kwamba maeneo yote katika Halmashauri hiyo
yatapuliziwa dawa.
Meya Sitta amefafanua
kuwa ugonjwa huo ambao umekuwa tishio kubwa duniani Halmashauri hiyo imejipanga
kikamilifu katika kuukabili ugonjwa huo usisambae ikiwa ni pamoja na kusambaza
wataalamu wa kupulizia dawa hiyo kwenye kata zote za Halmashauri hiyo.
“Kwa ujumla tunashiriki
ipasavyo katika kupambana na maambukizi ya virusi hivi, kwa pamoja
tunaunganisha nguvu kutoka kwenye ngazi ya mkoa, Kinondoni ni Halmashauri moja wapo ambayo
imeanza zoezi hili kwenye maeneo yote na
leo tumeanzia Kata ya Msasani ambapo ndio kuna wataalii wengi” amesema Mhe. Meya
Sitta.
Mhe. Meya
Sitta ameongeza kuwa “ ni jambo la muhimu kuchukua hatua kabla ya kupata
madhara , nakinga ni muhimu kuliko tiba , Kinondoni hatujasubiri janga hili
litufikie, tulianza kuchukua hatua mapema, tulijiandaa vizuri ndio mana hata
sasa tunaendelea kuchukua hatua kwakupiga dawa kwenye maeneo ya wananchi wetu.
Aidha Mhe.
Meya Sitta amesisitiza kuwa Kinondoni imejipanga na hivyo kuishukuru Serikali
ya awamu ya tano kwakudhibiti na kupambana dhidi ya kutokomeza ugonjwa huo
sambamba na kuwaelimisha wananchi jambo ambalo limepokelewa kwa asilimia 100.
Kwa upande wake
Mratibu wa Malaria mkoa wa Dar es Salaam, Dokta Ford Chisongela amesema kuwa mkoa unashirikiana na Halmashauri katika
kuhakikisha kuwa unatokomeza ugonjwa huo unaosababishwa na Vizuri vya COVID 19 (
Virusi vya Corona) kwa kupulizia dawa hizo katika maeneo yote ya mkoa huo.
Amefafanua kuwa
katika kuongeza nguvu ya kupulizia dawa hiyo, mkoa umeamua kutumia magari ya zimamoto
pamoja na yale ya Polisi kikosi Cha kutuliza ghasia (FFU) kwa lengo la kuongeza
nguvu katika zoezi hilo kwa kuwa magari hayo yanauwezo mkubwa wa kufanya kazi kwa haraka na hivyo kuwatoa hofu wananchi
wasishtuke pindi watakapo yaona mitaani.