 |
| Waziri wa Nishati Dkt
Medard Kalemani (kulia), akiwaongoza Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Nishati na Madini, kutembelea Mradi wa Umeme wa Kinyerezi I Extension, Machi
16, 2020. Kulia kwa Waziri ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dunstan Kitandula.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeipongeza
Serikali kupitia Wizara ya Nishati, kwa hatua ilizochukua katika kuhakikisha
Mradi wa umeme wa Kinyerezi I Extension (megawati 185) unakamilika mapema
iwezekanavyo.
Mwenyekiti wa Kamati, Dunstan Kitandula alitoa pongezi
hizo mbele ya waandishi wa habari, wakati akizungumzia msimamo wa Kamati hiyo
baada ya kutembelea Mradi husika uliopo eneo la Kinyerezi jijini Dar es Salaam,
Machi 16, 2020.
| |
 |
| Sehemu ya mitambo iliyopo katika Mradi wa Umeme wa
Kinyerezi I Extension jijini Dar es Salaam. Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Nishati na Madini (hawapo pichani), walitembelea Mradi huo, Machi 16
mwaka huu.
Alisema, Kamati iliamua kutembelea Mradi huo ili
kujiridhisha kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali baada ya kupata taarifa
kwamba Mkandarasi aliyekuwa akitekeleza Mradi husika ambaye ni Kampuni ya
Jacobsen Electro AS kutoka Norway, amefilisika hivyo haendelei tena na kazi.
Akieleza zaidi, Kitandula alisema, Kamati ilitaka
kujiridhisha kwamba kufilisika kwa Mkandarasi hakuiingizi nchi kwenye migogoro
ya kimkataba inayosababisha Taifa kuingia gharama zaidi, lakini pia kujionea
hatua zilizochukuliwa katika kuhakikisha Mradi unatekelezwa.
|
 |
| Meneja wa Mradi wa
Umeme wa Kinyerezi I Extension, Mhandisi Abdallah Chikoyo (kulia), akitoa
maelezo kuhusu Mradi huo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na
Madini, walipotembelea eneo hilo, Machi 16, 2020. Wa tatu kutoka kulia ni
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani na kulia kwake ni Mwenyekiti wa Kamati
husika, Dunstan Kitandula.“Kusema kweli sisi kama Kamati tumeridhishwa sana na
hatua zilizochukuliwa kuhusiana na suala hili, hivyo kwa niaba ya Kamati
nitumie nafasi hii kuipongeza Serikali.”Katika hatua nyingine, Kamati imekiri kuridhishwa na
kufurahishwa na uhakika uliotolewa na Serikali kuwa umeme kwa ajili ya matumizi
ya Treni ya mwendokasi (SGR) pindi itakapokamilika upo tayari na kwamba
hauhusiani na kukamilika au kutokamilika kwa Mradi huo wa upanuzi wa Kinyerezi
I. | |
 |
| Mwenyekiti wa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dunstan Kitandula (mbele) na Wajumbe
wa Kamati hiyo, wakikagua Mradi wa Umeme wa Kinyerezi I Extension, Machi 16,
2020. |
Kuhusu suala la malipo kwa wakandarasi wa ndani
waliokuwa wamepewa mkataba na mwekezaji husika ambaye amefilisika, Kitandula
alibainisha kuwa Kamati yake imejiridhisha na maelezo yaliyotolewa na Serikali
kuwa mchakato unaohusisha kuainisha mchanganuo wa malipo hayo, uko katika hatua
za mwisho ili waanze kulipwa.
Awali, akiwasilisha taarifa fupi ya Mradi kwa Kamati
husika, Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani alisema hatua zilizochukuliwa na
Serikali katika kuhakikisha nchi haipati hasara baada ya Mkandarasi kufilisika
ni pamoja na kuhakikisha vifaa vyote vinavyohusika katika utekelezaji wa mradi
viko katika eneo hilo.
 |
| Waziri wa Nishati Dkt
Medard Kalemani akiwasilisha maelezo mafupi ya utekelezaji wa Mradi wa Umeme wa
Kinyerezi I Extension kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na
Madini, baada ya kutembelea Mradi huo Machi 16, 2020 jijini Dar es Salaam.
Aidha, alibainisha kuwa Serikali ilijiridhisha kuwa
malipo yaliyofanyika kwa Mkandarasi huyo ni yale tu yanayoendana na kiwango cha
kazi aliyofanya na siyo zaidi.
“Mkandarasi amekamilisha kazi kwa wastani wa takribani
asilimia 85 na amelipwa kwa kazi ya asilimia 68 hivyo hakuna hasara,” alifafanua
Waziri.
Aliongeza kuwa, Serikali kwa kushirikiana na taasisi
nyingine mbalimbali ikiwemo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, imejipanga
kuhakikisha kazi iliyobaki, ambayo ni takribani asilimia 14, inakamilika ndani
ya kipindi kisichozidi mwezi Desemba mwaka huu.
| |
 |
| Wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, wakikagua Mradi wa Umeme wa Kinyerezi I
Extension uliopo jijini Dar es Salaam, Machi 16, 2020. |
“Nimeshatoa maelekezo kwa wataalamu kutoka taasisi
zote zinazohusika kuhakikisha tunampata Mkandarasi mwingine ndani ya siku 30
zijazo ili aanze kazi mara moja na kukamilisha kabla ya Desemba.”
Akieleza zaidi, Dkt Kalemani alisema Serikali
imedhamiria kumpata Mkandarasi mwenye uwezo ambaye gharama yake haitazidi
mpango mahsusi wa gharama halisi ya mradi.
Naye Meneja wa Mradi huo, Mhandisi Abdallah Chikoyo,
aliwaeleza Wajumbe wa Kamati kuwa, jumla ya miradi saba ya umeme unaotokana na
gesi imepangwa kutekelezwa na Serikali.
 |
| Wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, wakikagua Mradi wa Umeme wa Kinyerezi I
Extension uliopo jijini Dar es Salaam, Machi 16, 2020. |
 |
| Wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, wakikagua Mradi wa Umeme wa Kinyerezi I
Extension uliopo jijini Dar es Salaam, Machi 16, 2020. |
 |
| Wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, wakikagua Mradi wa Umeme wa Kinyerezi I
Extension uliopo jijini Dar es Salaam, Machi 16, 2020. |
Aliitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na wa Kinyerezi I (megawati
150) ambao ulikamilika mwaka 2016, Kinyerezi I Extension (megawati 185) ambao
ndiyo uliotembelewa na Kamati na uko katika hatua za mwisho kukamilika pamoja
na Kinyerezi II (megawati 148) uliokamilika mwaka 1918.
Mwingine ni Mradi wa Kinyerezi III utakaotekelezwa kwa
awamu mbili huku kila awamu ikitarajiwa kuzalisha megawati 300. Utekelezaji
wake uko katika hatua za kukamilisha utafiti na upembuzi yakinifu ili uanze
kutekelezwa.
 |
| Wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, wakikagua Mradi wa Umeme wa Kinyerezi I
Extension uliopo jijini Dar es Salaam, Machi 16, 2020. |
Veronica Simba – Dar es Salaam
Mhandisi Chikoyo alitaja miradi mingine kuwa ni
Kinyerezi IV (megawati 430), Mradi wa Mtwara (megawati 300) pamoja na Mradi wa
Somanga Fungu (megawati 350 hadi 370).
Mradi wa Kinyerezi I Extension unagharamiwa na
Serikali ya Tanzania kwa asilimia 100 na gharama yake ni Dola za Marekani milioni
188 sawa na shilingi za Tanzania takribani 435.48.
No comments:
Post a Comment