Muonekano wa barabara ya Itoni- Ludewa- Manda sehemu ya Lusitu- Mawengi (Km 50) inayojengwa kwa kiwango cha zege, mkoani Njombe.
Mhandisi Mshauri, Moon Dong Ryeol,
anayesimamia barabara ya Itoni- Ludewa- Manda sehemu ya Lusitu- Mawengi
(Km 50) inayojengwa kwa kiwango cha zege akifafanua jambo kwa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, anayeshughulikia
Sekta ya Ujenzi, Mbunifu Majengo, Elius Mwakalinga (Kushoto), wakati
akikagua barabara hiyo mkoani Njombe.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Mbunifu
Majengo, Elius Mwakalinga, amemtaka Mhandisi Mshauri anayesimamia
barabara ya Itoni- Ludewa- Manda sehemu ya Lusitu- Mawengi (Km 50),
inayojengwa kwa kiwango cha zege kujipanga upya kutokana na
kutoridhishwa na kasi ya utendeji kazi ya mkandarasi wa mradi huo.
Akizungumza wakati akikagua mradi
huo mkoani Njombe, Mwakalinga amemuagiza Mhandisi Mshauri huyo
kuhakikisha anawasilisha taarifa zote na muhtasari wa vikao wanavyokaa
na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), ofisini kwake, ili aone kama
anahifadhi taarifa hizo na anatekeleza yatokanayo na vikao hivyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Mbunifu
Majengo, Elius Mwakalinga, akitoa maagizo kwa Mhandisi Mshauri, Moon
Dong Ryeol, anayesimamia barabara ya Itoni- Ludewa- Manda sehemu ya
Lusitu- Mawengi (Km 50) inayojengwa kwa kiwango cha zege wakati akikagua
barabara hiyo mkoani Njombe.
“Sijafurahishwa na utendaji kazi
wa Mkandarasi, nimewaagiza waniletee taarifa zao zote pamoja na
muhtasari wa vikao vyote wanavyokaa wakiwa na TANROADS ili nione kama
anatekeleza maagizo anayopewa, na kama hatekelezi ni kwa nini yupo mpaka
sasa hivi”, amesema Mwakalinga.
Mwakalinga, amefafanua kuwa
Mkandarasi huyo hajawajibika kama inavyotakiwa kwani kuna baadhi ya
maeneo alitakiwa awe amefanya kazi zaidi, licha ya kuelezea kuwa na
changamoto ya hali ya hewa, uhaba wa rasilimali watu na vifaa, jambo
ambalo akijipanga vyema linaweza kutatulika.
Mhandisi Mshauri, Moon Dong Ryeol,
anayesimamia barabara ya Itoni- Ludewa- Manda sehemu ya Lusitu- Mawengi
(Km 50) inayojengwa kwa kiwango cha zege akimuonesha Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, anayeshughulikia Sekta ya
Ujenzi, Mbunifu Majengo, Elius Mwakalinga (Wa Kwanza Kushoto mbele),
maungio ya zege yaliyopo katika barabara hiyo, mkoani Njombe.
Mwakalinga, ameongeza kuwa lengo
la kutaka mradi huo kuharakishwa ni kutokana na umuhimu wa barabara hiyo
katika kukuza uchumi kwani ni kiungo cha usafiri na usafirishaji wa
watu na mizigo kati ya mkoa wa Njombe na Ruvuma.
Kwa upande wake, Mhandisi Mshauri
wa mradi huo, Moon Dong Ryeol, amemhakikishia Katibu Mkuu huyo kuwa
ataleta wataalamu wengine wa kusaidia kuongeza nguvu ya usimamizi pamoja
na kuongeza kasi ya ujenzi na muda wa kufanya kazi.
Muonekano wa barabara ya Itoni- Ludewa- Manda sehemu ya Lusitu- Mawengi (Km 50) inayojengwa kwa kiwango cha zege, mkoani Njombe.
Aidha, Ryeol, ameahidi kununua
mtambo wa pili wa kuzalisha zege pamoja na mashine ya kisasa ya kuweka
tabaka la zege ili kwa pamoja visaidie katika ufanisi wa mradi huo.
Katika hatua nyingine, Mwakalinga
amekagua barabara ya Mbinga – Mbamba Bay yenye urefu kilometa 66 ambapo
ameridhishwa na utendaji kazi wa Mkandarasi anayejenga mradi huo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Mbunifu
Majengo, Elius Mwakalinga, akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mshauri kutoka
SMEC International (katikati) anayesimamia barabara ya Mbinga – Mbamba
Bay (Km 66) kwa kiwango cha lami. Barabara hiyo imefika asilimia 49.6.
PICHA NA WUUM
Mwakalinga, amesema kuwa mradi huo
sio tu kwamba unatekelezwa kwa haraka, bali pia unajengwa kwa ubora
kwani mkandarasi amejipanga na kuzingatia misingi ya kitaalamu ya ujenzi
wa barabara.
Sambamba na hilo, Mwakalinga,
wakati akikagua barabara hiyo, wilayani Nyasa mkoani Ruvuma, amefafanua
kuwa mpaka sasa mradi unaendelea vizuri kwani mkandarasi yupo ndani ya
mkataba na anaamini kwa utaratibu anaoenda nao, mkandarasi huyo anaweza
kumaliza kazi hiyo kwa wakati.
“Nimekagua mwanzo hadi nwisho wa
mradi, kwa kweli kazi imefanyika haswa tena yenye ubora, nampongeza
mkandarasi huyu kwa kufanya kazi kwa juhudi kubwa, naomba endelea
kukamilisha kipande kilichobakia”, amesema Mwakalinga.
Katika hatua nyingine Mwakalinga,
amekagua daraja la Mto Ruhuhu ambapo amesema kuwa kwa sasa ujenzi wa
daraja hilo umesimama kutokana na mto kufurika maji na wataalamu
kushindwa kuendelea mpaka maji yatakapopungua.
Ukaguzi huu ni mwendelezo wa ziara
ya Katibu Mkuu Mwakalinga katika mikoa mbalimbali nchini ili kukagua
miradi inayotekelezwa na Sekta ya Ujenzi.
No comments:
Post a Comment