
Hafsa Omar-Dodoma
Wakandarasi wanaotekeleza mradi wa umeme pembezoni mwa miji (
Peri-Uban) wametakiwa kukamilisha kazi ya usambazaji umeme katika
maeneo waliyopangiwa ifikapo Juni, 2020 la sivyo watachukuliwa hatua
za kisheria.
Maagizo
hayo yametolewa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, Machi 19,
2020, mkoani Dodoma wakati wa kikao chake na Wakandarasi wanaotekeleza
mradi huo.
Kikao
hicho kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Zena Said, Kaimu Kamishna wa Umeme
na Nishati Jadidifu Mhandisi Edward Ishengoma, Kamishna Msaidizi wa
Umeme, Mhandisi Innocent Luoga pamoja na viongozi mbalimbali wa Wizara,
Taasisi.
Dkt.
Kalemani aliwaelekeza wakandarasi wa mradi huo kuweka mpango madhubuti
ambao utabainisha vijiji vyote ambavyo havijawekewa umeme na mpango huo
uoneshe ni lini vijiji hivyo vitapelekewa umeme ndani ya muda
uliopangwa.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,(katikati) Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu,(kulia) Katibu Mkuu, Mhandisi Zena Said,(kushoto) wakiwa kwenye kikao na Wakandarasi wanaotekeleza mradi wa Peri Urban,Mkoani Dodoma, Machi 19,2020.
Aidha,
aliwataka wakandarasi hao kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha ndani
ya muda waliokubaliana wawe tayari wameanza kuwasha umeme kwenye vijiji
na miezi miwili inayofuata waitumie kusambazia wananchi umeme majumbani.
Aidha,
aliwaagiza wakandarasi wote wa mradi huo kupeleka orodha ya vijiji
vinavyosambaziwa umeme kwa Wakuu wa Mikoa, Wilaya, wenyeviti wa vijiji
na mtaa ili viongozi hao wasaidie katika ufuatiliaji wa mradi huo.
Pia,
aliwataka kuhakikisha kuwa nguzo zote ambazo zimelazwa chini kwenye
maeneo yao, ziwe zimesimikwa na nguzo ambazo zimesimikwa bila kuwa na
nyaya, ziwe zimefungwa nyaya ndani wa mwezi huu.
Kwa
upande wake, Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu aliwataka
wakandarasi hao kuupa kipaumbele mradi huo muhimu katika nchi na kwamba
wanachotaka kuona kwasasa ni uwashwaji wa umeme katika maeneo hayo.
Alisema, ana imani kuwa, wakandarasi hao watafuata maelekezo aliyoyatoa Waziri wa Nishati na kuyafanyia kazi.
Naye,
Katibu Mkuu, Mhandisi Zena Said, aliwakumbusha wakandarasi hao kuwa,
Serikali imewapa fursa na kuwaamini hivyo na wao wanatakiwa kutoiangusha
Serikali kwa kumaliza kazi zao kwa muda uliopangwa.
Vilevile,
aliwataka wasimamizi wa miradi hiyo ya umeme kufanya kazi kwa weledi na
kuwasimamia ipasavyo wakandarasi hao ili kuhakikisha wanamaliza kazi
zao kwa mujibu wa mkataba.
No comments:
Post a Comment