Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akiongoza Kikao cha
Makadirio ya Mapato, Matumizi na Miradi ya Maendeleo ya Jeshi la
Magereza kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Makao Makuu ya wizara,
jijini Dodoma.Aliyesimama ni Mkuu wa Kitengo cha Mipango wa Jeshi la
Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Ambayuu Kitiku.Picha na Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Jeshi la Magereza nchini limedhamiria
kuanzisha Kiwanda cha Mikate kitakachojengwa katika Chuo cha Taaluma ya
Urekebishaji Ukonga ili kwenda sambamba ya dhana ya Viwanda ya Serikali
ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Hayo yamesemwa leo Machi,20 na Mkuu wa Kitengo cha Mipango wa Jeshi
hilo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Ambayuu Kitiku wakati akiwasilisha
maelezo ya Randama kuhusu Makadirio ya Mapato, Matumizi ya Kawaida na
Miradi ya Maendeleo kwa mwaka 2020/2021 mbele ya Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, George Simbachawene wakati wa kikao kilichofanyika jijini
Dodoma.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio,
akizungumza wakati wa Kikao cha Makadirio ya Mapato, Matumizi na Miradi
ya Maendeleo ya Jeshi la Magereza kilichofanyika leo katika Ukumbi wa
Makao Makuu ya wizara, jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi
“Katika mpango wa bajeti wa mwaka 2020/2021 Jeshi limeweka vipaumbele
katika maeneo ya ajira na maendeleo ya watumishi, utawala wa magereza,
uboreshaji miundombinu ya majengo ya magereza, kuimarisha shughuli za
kilimo ili kujitosheleza kwa chakula, kuimarisha shughuli za Shirika la
Magereza na kuimarisha shughuli za Viwanda ikiwepo Ujengaji wa Kiwanda
cha Mikate kitakachojengwa katika Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji
Ukonga kilichopo jijini Dar es Salaam” alisema SACP Kitiku
Akizungumza wakati akichangia hoja hiyo Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, George Simbachawene aliwataka Jeshi la Magereza pindi mradi huo
utakapoanza watengeneze mkate bora wakizingatia suala nzima la masoko,
teknolojia bora ikiwepo ladha ya mkate huo, vifungashio vyake ili waweze
kwenda sambamba na hitajio la mtumiaji wa mwisho
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, Suleiman Mzee akizungumza wakati wa
Kikao cha Makadirio ya Mapato, Matumizi na Miradi ya Maendeleo ya Jeshi
la Magereza kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Makao Makuu ya wizara
jijini Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Christopher Kadio.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkurugenzi
wa Sera na Mipango wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Wanja Mtawazo
akizungumza mbele ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George
Simbachawene (kulia), wakati wa Kikao cha Makadirio ya Mapato, Matumizi
na Miradi ya Maendeleo ya Jeshi la Magereza kilichofanyika leo katika
Ukumbi wa Makao Makuu ya wizara, jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi.
Mkuu wa
Kitengo cha Mipango wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi,
Ambayuu Kitiku akimpitisha katika randama Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, George Simbachawene wakati wa Kikao cha Makadirio ya Mapato,
Matumizi na Miradi ya Maendeleo ya Jeshi la Magereza kilichofanyika leo
katika Ukumbi wa Makao Makuu ya wizara, jijini Dodoma. Picha na Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
“Ni wazo zuri kwa mlichopanga kwani mtakapofanikiwa mtakua mmeongeza
kipato na ile dhana ya jeshi la magereza kujitegemea itakua sasa
imeingia kwenye utekelezaji sambamba na kujitosheleza kwa chakula cha
kulisha wafungwa, lakini katika mpango huo lazima baadhi ya mambo
muyafanyie utafiti ikiwepo soko linataka nini, teknolojia mtakayotumia
muhakikishe ni nzuri itakayowafanya mpate bidhaa yenye ladha nzuri
sambamba na kifungashio cha bidhaa hiyo, ni vizuri mmeliweka wazo wazi
mapema nadhani mtapata michango ya kuliboresha” alisema Simbachawene
Jeshi la Magereza limeomba kuidhinishiwa kiasi cha Shilingi
201,251.298,000/- katika mwaka wa fedha 2020/2021 kwa ajili ya matumizi
mbalimbali ikiwemo miradi ya maendeleo huku likiweka lengo la kukusanya
maduhuli ya Shilingi 2,000,000.000/- kwa mwaka wa fedha wa 2020/2021.
No comments:
Post a Comment