Matokeo chanyA+ online




Friday, April 17, 2020

BUNGE LAPITISHA BAJETI YA OFISI YA MAKAMU WA RAIS KWA MWAKA 2020/2021

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akijibu hoja za wabunge waliochangia mjadala wa hotuba ya Ofisi hiyo kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2020/2021 aliyoiwasilisha  Bungeni jijini Dodoma.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima akisisitiza jambo wakati akiibu hoja za waliochangia mjadala wa hotuba ya Ofisi hiyo kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2020/2021 iliyowasilisha  Bungeni jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji kutoka Ofisi hiyo pamoja na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) mara baada ya kuwasilisha hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2020/2021 leo Bungeni jijini Dodoma. Wa tatu kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (SeraUratibuBunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandis Joseph Malongo akiondoka katika viwanja vya Bunge mara baada ya kumaliza uwasilishwaji na upitishwa wa Bajeti ya Ofisi hiyo bungeni jijini Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Profesa Esnati Chagu.


No comments:

Post a Comment