Naibu Waziri Constantine Kanyasu |
Serikali
imetolea ufafanuzi wa kauli iliyotolewa na baadhi ya Wananchi
wanaodai kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii imekuwa ikithamini uhai wa
wanyamapori kuliko uhai wa Binadamu.
Akizungumza
na viongozi wa vijiji vitano vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti katika wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Naibu Waziri Constantine Kanyasu amesema uhai wa binadamu una thamani kubwa na kamwe hauwezi
kufananishwa na uhai wa wanyamapori
Amesema
licha ya kuwa Binadamu anaaminika kuwa akili kuliko Wanyamapori hata
hivyo Wizara hiyo imekuwa ikifanya kila liwezekalo ili kuondoa migogoro
kati ya Wanyamapori na binadamu.
" Tunaamini kila binadamu angetamani kuona yupo salama na ndio madhumuni na matamanio ya serikali" Amesisitiza Naibu Waziri Kanyasu.
Amesisitiza
kuwa binadamu ana uwezo wa kukwepa mienendo ya wanyamapori na kuwa
katika mazingira salama kuliko mnyama mwenyewe na ameongeza kuwa
wanyamapori hao wapo kwa ajili ya Binadamu na sio vinginevyo.
Akitaja
baadhi ya mikakati iliyochukuliwa na Serikali ili kunusuru uhai wa
binadamu ni pamoja na kuhamisha jumla ya Simba 36 kutoka Hifadhi ya
Taifa ya Serengeti na kupelekwa katika Hifadhi nyingine lengo likiwa ni
kupunguza madhara kwa binadamu wanaoishi karibu na Hifadhi hiyo.
Amesema
jitihada hizo zilizochukuliwa na Serikali kufuatia Simba kula ng'ombe
wapatao 360 kwa kipindi cha mwezi Januari na Februari mwaka huu huku
baadhi ya Wananchi kuuawa na wengine kujeruhiwa na wanyamapori wakali na
waharibifu ni mkakati wa kuona maisha ya binadamu yanakuwa salama.
Licha
ya jitihada hizo zilizofanywa na Serikali, Mhe.Kanyasu amewataka
wananchi kuchukua tahadhari kwa kujiepusha kulima mazao pamoja kujenga
nyumba karibu na vigingi ili kuepuka athari za wanyamapori hao kwa
vile wanyamapori wanakapokuja hawajui kuwa wamevuka mpaka.
Amesema maamuzi hayo ni moja ya jitihada za Serikali kuhakikisha uhai wa binadamu unalindwa kwa gharama yoyote ile.
Amesema
licha ya kuwa moja ya jukumu la msingi la Wizara hiyo ni kulinda na
kuendeleza Wanyamapori kwa ajili ya kizazi cha sasa na cha badae lakini
hata hivyo thamani ya Uhai wa binadamu ipo pale pale .
No comments:
Post a Comment