Asteria Muhozya na
Nuru Mwasampeta - Dodoma
Watumishi wa Wizara ya
Madini wakiongozwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Issa Nchasi leo
Aprili 2, wametembelewa na wataalamu wa afya kwa lengo la kutoa elimu juu ya
ugonjwa wa corona unaosababishwa na virusi vya covid-19 na namna ya kujikinga
na ugonjwa huo.
Wataalamu hao ni
pamoja na Dkt. Shamza Said ambaye ni miongoni mwa wataalamu wa afya
wanaojishughulisha na magonjwa yanayoambukiza kwa kasi aliyeambatana na Toyi
Veronica mtaalamu wa mazingira katika masuala ya afya.
Watumishi wa Wizara wakifuatilia mafunzo juu ya ugonjwa wa corona kutoka kwa wataalamu wa afya (hawapo pichani) |
Akizungumzia virusi
vinavyosababisha ugonjwa huo Dkt. Shamza alisema virusi vya covid-19 ni virusi
vipya kuwepo duniani vya aina hiyo vinavyotoka kwa wanyama na kusababisha
madhara kwa binadamu.
Mtaalamu wa afya Dkt. Shamza Said akitoa elimu ya ugonjwa wa corona kwa
watumishi wa Wizara ya Madini ili kuwapa uelewa wa ugonjwa huo na namna ya
kujikinga
|
Amesema virusi hivi
pindi vinapoingia mwilini mwa binadamu vinasababisha madhara mbalimbali ikiwa
ni pamoja na kushambulia mfumo wa upumuaji, figo, ini na madhara mengine na
kuwasihi watumishi na jamii pindi wanapohisi kuwa na dalili za ugonjwa huo,
kuhakikisha wanawahi katika vituo vya afya ili kupatiwa huduma stahiki kabla ya
ugonjwa kusababisha madhara makubwa mwilini.
Mtaalamu wa afya Dkt. Shamza Said akitoa elimu ya ugonjwa wa corona kwa
watumishi wa Wizara ya Madini ili kuwapa uelewa wa ugonjwa huo na namna ya
kujikinga
|
Amesema, unapowahi
kupata huduma za kitabibu kuna uwezekano mkubwa wa kupona tofauti na mtu
anayekwenda kutibiwa awapo katika hali mbaya.
Aidha, Dkt Shamza
amewashauri watumishi kupunguza mikusanyiko isiyokuwa ya lazima, kunawa kwa
sabuni na vitakasa mikono kila wakati, kuacha kukusanyika katika masherehe,
matumizi ya vifaa vya vyakula yasiwe shirikishi, kuzingatia uvaaji sahihi wa
mask pamoja na kuwa wawazi wanapojihisi kuwa na maambukizi ya ugonjwa ili
kuepusha kuambukiza watu wengine.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Issa Nchasi akiwakaribisha wataalamu wa Afya kutoa mafunzo juu ya ugonjwa wa corona kwa watumishi wa Wizara ya Madini Makao Makuu jijini Dodoma, leo asubuhi. |
Kwa kuhitimisha, Dkt.
Shamza amewataka watumishi kutoa elimu ya corona kwa watu wengine katika
familia ndugu jamaa na marafiki ili elimu hii iwafikie wengi na waweze
kujikinga na hivyo kupunguza maambukizi nchini. “Unapopata elimu, elimisha na
wengine” amisisitiza Dkt. Shamza.
Kwa kuhitimisha, Dkt.
Shamza amewataka watumishi kutoa elimu ya corona kwa watu wengine katika
familia ndugu jamaa na marafiki ili
elimu hii iwafikie wengi na waweze kujikinga na hivyo kupunguza maambukizi
nchini. “Unapopata elimu, elimisha na wengine” alisisitiza.
Kwa upande wake,
Mtaalamu wa mazingira katika masula ya Afya, Koyi Veronika ameushauri uongozi
wa wizara kupunguza vikao kazi vya ana kwa ana na badala yake uongozi kwa
kushirikiana na wataalamu wa TEHAMA kuratibu mfumo wa kutumia mtandao katika
vikao vyao ili kuepusha maambukizo miongoni watumishi.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Issa Nchasi akiwakaribisha wataalamu wa Afya kutoa mafunzo juu ya ugonjwa wa corona kwa watumishi wa Wizara ya Madini Makao Makuu jijini Dodoma, leo asubuhi. |
Kwa kuhitimisha, Dkt.
Shamza amewataka watumishi kutoa elimu ya corona kwa watu wengine katika
familia ndugu jamaa na marafiki ili
elimu hii iwafikie wengi na waweze kujikinga na hivyo kupunguza maambukizi
nchini. “Unapopata elimu, elimisha na wengine” alisisitiza.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala, Issa Nchasi amewashukuru Wizara ya
Afya kwa mpango mzuri walioanzisha wa kupita na kutoa elimu kwa watumishi na
kuahidi kuyasimamia yote waliyoelekeza ili kupambambana na gojwa hatarishi la
corona.
Dkt. Shamza Said akijibu maswali juu ya ugonjwa wa Corona aliyoulizwa na watumishi |
Baada ya kutoa elimu
hiyo zilipo ofisi zaWizara Makao Makuu, wataalamu hao wameelekea zilipo ofisi
za Taasisi ya Jiolojia na Utafiti na Ofisi ndogo za Wizara ya Madini, Chuo cha
Madini na kumalizia mafunzo hayo ofisi za Tume ya Madini.
Msaidizi wa Ofisi Mwandamizi, Veneranda Charles akiuliza swali kwa wataalamu wa afya juu ya vitakasa mikono vinavyoshauriwa kutumika ili kujikinga na ugonjwa wa corona. |
No comments:
Post a Comment