Waziri wa Nishati Medard Kalemani akizungumza kabla ya kuwasha umeme katika vijiji vya Matare na Nkuhi vilivyopo jimbo la Singida Mashariki,kulia kwake ni Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu na kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Edward Mpogolo. |
Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Miraji Mtaturu akizungumza katika ziara ya Waziri wa Nishati Medard Kalemani jimboni humo. |
Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani akitoa maagizo kwa wakandarasi wa umeme akiwa katika ziara wilayani Ikungi ambapo aliwasha umeme katika vijiji viwili vya Matare na Nkuhi. |
Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu akizungumza mbele ya Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani na Mkuu wa wilaya ya Ikungi Edward Mpogolo. |
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani amewasha umeme
katika vijiji viwili vya Matare na Nkuhi vilivyopo jimbo la Singida
Mashariki Mkoani Singida na hivyo kufanya jumla ya vijiji 19 kati ya 50
sawa na asilimia 38 kupata huduma ya umeme jimboni humo.
Ili
kukamilisha ahadi ya serikali ya kuhakikisha wanafikisha umeme vijijini
Dkt Kalemani ametoa agizo kwa Shirika la Umeme Nchini(TANESCO)
kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja wanaweka umeme kwenye vijiji vingine 11
vilivyopo katika jimbo hilo
Dkt
Kalemani ametoa maagizo hayo wilayani Ikungi akiwa katika ziara ya
kukagua miradi ya umeme ambapo pia ameagiza TANESCO Singida kumsimamia
mkandarasi aanze kusimika nguzo mapema katika Tarafa ya Mungaa
Lighwa,Ntuntu,Misughaa na Kikio ili umeme uwashwe kwenye Vijiji kabla ya
mwezi June mwaka huu
"Nampongeza
Sana Mbunge wenu Mhe Miraji Mtaturu, kwani anafuatilia sana miradi ya
wananchi wake,tangu amechaguliwa na kuapishwa ni miezi mitano tu lakini
mnaona mambo yalivyo, leo tu tumewasha vijiji viwili je angekaa miaka
minne hali ingekuwaje?,"alihoji Dkt Kalemani.
Ili
kuharakisha kazi hiyo amesema," Ndugu zangu Ugonjwa huu wa homa kali ya
mapafu(COVID 19)usikwamishe kazi za kuunganishia umeme wananchi ila
mfanye kazi kwa tahadhari,Rais Dkt John Magufuli ameidhinisha sh Bilion
40 kwa Mkoa wa Singida ili kutekeleza miradi hii hivyo ni lazima
tuisimamie,"alisema Dkt Kalemani.
Pamoja
na hayo Dkt Kalemani amesisitiza wananchi kutolipishwa nguzo na gharama
za kuunganishiwa umeme amesema ni sh 27,000 tu na sio vinginevyo.
"Katika
hili niagize hapa mkandarasi wa Cyba Contractors Ltd ya jiji Mbeya
aliyelalamikiwa kuwatapeli wananchi baada ya kuchukua pesa zao na
hajafanya wiring mpaka sasa atafutwe,"aliagiza Dkt Kalemani.
Awali
akizungumza katika ziara hiyo,Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Edward Mpogolo
amesema katika kata 28 zilizopo wilayani humo,ni kata 18 tu ndio
zimefikiwa na umeme hivyo kumuomba waziri aendelee kuwasaidia.
"Mh
Waziri kwanza nikupongeze na kukushukuru kwa kazi nzuri ya kusimamia
miradi ya umeme,wilaya ya Ikungi tulipewa Vijiji 30 na
vimeshaunganishiwa umeme,lakini waswahili wanasema kushukuru ni kuomba
tena,mh waziri naomba uendelee kutusaidia wananchi wa Ikungi tupate
umeme katika maeneo yote,"aliomba mkuu wa wilaya hiyo.
Amesema
katika wilaya hiyo viongozi wa serikali,chama na wabunge wote wawili
wanafanya kazi kwa ushirikiano hali inayopelekea kurahisisha upelekaji
wa maendeleo kwa wananchi.
Kwa upande wake mbunge Mtaturu amemshukuru
Rais
Magufuli kwa dhamira yake ya dhati ya kuwaletea wananchi maendeleo
kwani aliahidi kuwafikishia umeme wananchi na utekelezaji wa ahadi hiyo
unaonekana.
"Sisi
wananchi wa Singida Mashariki na Ikungi kwa ujumla tunatoa shukrani za
pekee kwake,miradi mingi tunaiona inatekelezwa,na tunaahidi kumpa kura
za kishindo katika uchaguzi mkuu ujao,"alishukuru mbunge huyo.
Amempongeza Dkt Kalemani kwa kumsaidia Rais Magufuli kusimamia sekta ya Nishati kwani miradi inaenda vizuri nchi nzima.
"Pamoja
na shukrani hizo mh waziri Tarafa ya Ikungi kwenye vijiji vya
Manjaru,Tumaini,Ng'ongosoro, Matongo,Kimbwi,Unyang'ongo na Mbwanjiki
vipo barabarani havina umeme kwa muda mrefu pamoja na miundombinu kuwepo
jirani,"aliongeza Mtaturu.
Nae
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa
ameipongeza serikali kupitia Rais Dkt Magufuli kwa kuendelea kutekeleza
Ilani ya uchaguzi ya chama hicho vizuri na kuomba Vijiji vilivyosalia
vikamilishiwe kuwekewa umeme.
No comments:
Post a Comment