Mkurugenzi
wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Kilimo Bi Hilda Kinanga
akisisitiza jambo wakati akimuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Ndg Gerald Kusaya kwenye ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi lililofanyika tarehe 21 Mei 2020 katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha Ujenzi
Mkoani Morogoro. (Picha Zote Na Mathias Canal, NFRA)
Watumishi
wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) wametakiwa kutekeleza
majukumu yao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Maadili katika Utumishi wa
Umma.
Rai
hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya
Kilimo Bi Hilda Kinanga wakati akimuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya
Kilimo Ndg Gerald Kusaya wakati wa ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi
lililofanyika leo tarehe 21 Mei 2020 katika ukumbi wa mikutano wa chuo
cha Ujenzi Mkoani Morogoro.
Mkurugenzi
wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Kilimo Bi Hilda Kinanga
akisisitiza jambo wakati akimuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Ndg Gerald Kusaya kwenye ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi lililofanyika tarehe 21 Mei 2020 katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha Ujenzi
Mkoani Morogoro. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi
ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula
NFRA Ndg Milton Lupa (Kulia) na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi
TUGHE NFRA Makao Makuu Mathias Mganga.
Kinanga amewataka wafanyakazi hao kuhakikisha kuwa wanapambana na RUSHWA katika sehemu za kazi.
“Kama
mnavyofahamu nchi yetu ni kati ya nchi zinazopiga vita suala zima la
RUSHWA mahala pa kazi na katika jamii kwa ujumla. Hivyo ninasisitiza na
kuelekeza kuzingatia maadili ya Utumishi wa Umma kwa kutoshiriki katika
kutoa au kupokea rushwa” Amekaririwa Bi Hilda
Wajumbe
wa Baraza la wafanyakazi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula
(NFRA) wakifatilia hotuba ya mgeni rasmi-Mkurugenzi wa Utawala na
Rasilimali watu wa Wizara ya Kilimo Bi Hilda Kinanga akisisitiza jambo
wakati akimuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Gerald Kusaya
kwenye ufunguzi wa Baraza hilo lililofanyika leo tarehe 21 Mei 2020
katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha Ujenzi Mkoani Morogoro.
“Naomba
niwakumbushe kuwa Serikali haitasita kuchukua hatua kwa Mtumishi yoyote
atakayejihusisha na vitendo vya rushwa pamoja na vitendo vinavyokiuka
maadili ya Utumishi wa Umma” Amesema
Mwenyekiti
wa Baraza la wafanyakazi ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Ndg Milton Lupa akisisitiza jambo
kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi-Mkurugenzi
wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Kilimo Bi Hilda Kinanga kwa
ajili ya ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi lililofanyika tarehe 21
Mei 2020 katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha Ujenzi Mkoani Morogoro.
Aidha
amewahakikishia kuwa, Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za
kutatua changamoto hizo, huku akisema kuwa Wataalam hao katika majukumu
yao wanapaswa kutumia uwezo weo katika kuibua mikakati itayosaidia
kuwezesha Wakala kutekeleza majukumu yake na kujiendesha kibiashara.
Mkurugenzi
wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Kilimo Bi Hilda Kinanga
akisisitiza jambo wakati akimuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Ndg Gerald Kusaya kwenye ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi lililofanyika tarehe 21 Mei 2020 katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha Ujenzi
Mkoani Morogoro. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi
ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula
NFRA Ndg Milton Lupa (Kushoto) na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi
TUGHE NFRA Makao Makuu Mathias Mganga (Kulia).
Kwa
upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya
Chakula (NFRA) Ndg Milton Lupa amesema kuwa katika siku mbili za Kikao
hicho masuala mbalimbali yatajadiliwa yanayohusu Wakala na miongoni mwa
ajenda hizo ni Kupitia Mpango wa Biashara wa mwaka 2020/2021 (Business
Plan), taarifa ya utekelezaji ya robo ya tatu ya mwaka 2019/2020 na
kupitia Rasimu ya Miundo mipya ya Maendeleo ya Utumishi.
Lupa
amemuhakikishia mgeni rasmi kuwa mambo mengine muhimu yatajadiliwa
katika kikao hicho ambapo agenda ya kwanza itawapitisha watumishi katika
malengo/mipango ya Wakala, ya pili ni utekelezaji wa majukumu ya Wakala
uliofanyika kwa mwaka tulionao na tatu ni mpango wa kuboresha maslahi
ya wafanyakazi kwa lengo ya kuandaa majukumu mapya yanayoendana na
Muundo mpya wa Taasisi.
Wajumbe
wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula
(NFRA) wakiimba wimbo wa mshikamano wakati wa ufunguzi wa Baraza la
wafanyakazi lililofanyika leo tarehe 21 Mei 2020 katika ukumbi wa
mikutano wa chuo cha Ujenzi Mkoani Morogoro.
Na Mathias Canal, NFRA-Morogoro
Lupa
ameiomba serikali kupitia Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo kuwasiliana
na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora kwa
ajili ya kupatikana kwa wataalamu wa kuendesha mradi wa maghala na
vihenge vya kisasa punde vitakapokamilika.
Kadhalika
Lupa ameiomba serikali kuiruhusu NFRA kutumia fedha za mradi wa ujenzi
wa maghala na Vihenge vya kisasa Mkoani Rukwa kukarabati maghala
yaliyopo kwa ajili ya kutumika kuhifadhia mahindi kwani msimu wa ununuzi
umekaribia.
No comments:
Post a Comment