Waziri wa
Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (Mb) akiwasilisha hotuba ya Bajeti ya Matumizi ya
kawaida ya wizara hiyo ya mwaka 2020/2021. tarehe 12 Mei 2020 (Picha
Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
|
1.
UTANGULIZI
1. Mheshimiwa
Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa leo ndani ya Bunge lako
Tukufu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo Mifugo na Maji
iliyochambua Bajeti ya Wizara ya Kilimo (Fungu 43), Tume ya Taifa ya
Umwagiliaji (Fungu 05) na Tume ya Maendeleo ya Ushirika (Fungu 24)
mnamo tarehe 25 na 26 Machi, 2020 Jijini Dodoma, naomba kutoa hoja
kwamba Bunge lako Tukufu sasa lipokee na kujadili taarifa ya utekelezaji
wa Mpango na Bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka wa fedha 2019/2020 na
makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa mwaka wa Fedha 2020/2021.
2. Mheshimiwa
Spika,kwanza ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kuwa na afya
njema na kuendelea kuijalia nchi yetu amani, utulivu na mshikamano na
kutuwezesha kushiriki katika mkutano huu wa Bunge la 19 la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania ambao ni mkutano wa mwisho katika uhai wa Bunge la 11.
3. Mheshimiwa
Spika, napenda kumshukuru kwa dhati Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuendelea
kuniamini kusimamia Kilimo ambacho ndio tegemeo la Watanzania walio wengi.
Vilevile, niwashukuru Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais na
Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano
wa Tanzania kwa kazi kubwa wanayofanya kusukuma maendeleo ya nchi hii, ikiwemo
Sekta ya Kilimo. Aidha, binafsi ninawashukuru viongozi wangu wote kwa
maelekezo, ushauri na miongozo wanayonipatia ambayo imenisaidia kutekeleza
majukumu yangu kwa ufanisi mkubwa.
4. Mheshimiwa
Spika, kwa mara nyingine naomba kumpongeza Waziri Mkuu, Mhe. Kassim
Majaliwa Majaliwa (Mb.) kwa hotuba yake nzuri aliyoitoa hapa Bungeni
tarehe 1 Aprili, 2020. Hotuba hiyo iligusa maeneo mengi ikiwemo Sekta ya Kilimo
ambapo alisisitiza uimarishaji wa huduma za ugani, kilimo cha umwagiliaji,
ushirika, upatikanaji wa pembejeo sahihi na miundombinu ya masoko.
Aidha,
napenda kumpongeza Mhe. Hussein Mohammed Bashe (Mb.) kwa kuteuliwa kwake kuwa
Naibu Waziri na Ndugu Gerald M. Kusaya kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Kilimo
na kuungana na viongozi wengine wa wizara kusukuma kilimo hapa nchini.
5. Mheshimiwa
Spika,naomba nitumie fursa hii kukupongeza wewe binafsi, na Naibu
Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson Mwansasu (Mb.) pamoja na Wenyeviti wa Bunge kwa
namna mnavyolisimamia na kuliendesha Bunge letu tukufu kwa weledi na umahiri
mkubwa. Aidha, niwapongeze Waheshimiwa Wabunge wote kwa ujumla kwa kazi nzuri
walizozifanya katika miaka hii mitano ya kuwawakilisha wananchi katika Bunge
hili. Nimpongeze pia Mheshimiwa Miraji Jumanne Mtaturu Mbunge wa Singida
Mashariki kwa kuchaguliwa kujiunga na Bunge lako Tukufu.
6. Mheshimiwa
Spika, naomba kuwapongeza Mawaziri walioteuliwa katika kipindi cha
mwaka wa fedha 2019/2020, Mheshimiwa George Boniface Simbachawene Mbunge wa
jimbo la Kibakwe kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu Mbunge wa jimbo la Ilala kwa kuteuliwa kuwa Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira na
Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Mbunge wa Iramba Magharibi kuwa Waziri
wa Katiba na Sheria.
7. Mheshimiwa
Spika,katika kipindi cha mwaka wa fedha 2019/2020 Bunge lako Tukufu
limewapoteza Wawakilishi wenzetu wanne ambao ni Mheshimiwa Rashid Ajali Akbar
aliyekuwa Mbunge wa Newala Vijijini aliyefariki tarehe 15 Januari 2020,
Mheshimiwa Mchungaji Dkt. Getrude Pangalile Rwakatare Mbunge wa Viti Maalum
aliyefariki tarehe 20 Aprili, 2020, Mheshimiwa Richard Mganga Ndassa Mbunge wa
Sumve aliyefariki tarehe 29 Aprili, 2020 na Mheshimiwa Balozi
Dkt Augustine Philip Mahiga (Mb) aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria
aliyefariki tarehe 1 Mei, 2020. Nitumie fursa hii kutoa pole kwako, Bunge lako
Tukufu, Chama cha Mapinduzi, familia za marehemu, ndugu, jamaa na wananchi wa
majimbo ya Newala Vijijini na Sumve.
8. Mheshimiwa
Spika,napenda kuwashukuru wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Kilimo, Mifugo na Maji chini ya Uenyekiti wa Mheshimiwa Mahmoud Hassan Mgimwa,
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini na Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Dkt.
Christine Gabriel Ishengoma Mbunge wa Viti Maalum kwa ushirikiano na
ushauri mzuri walioutoa katika kipindi chote cha mwaka 2019/2020 pamoja
na kuipitia taarifa ya utekelezaji ya mwaka 2019/2020 na Mpango wa Bajeti ya
Wizara ya Kilimo kwa mwaka 2020/2021. Naomba kulihakikishia Bunge lako Tukufu
kwamba, ushauri wao umezingatiwa na tutaendelea kushirikiana na Kamati ili
kuleta mageuzi ya kilimo na kufikia matarajio ya wananchi katika kufikia uchumi
wa kati.
9. Mheshimiwa
Spika, natoa shukrani zangu za pekee kwa Wananchi wa Jimbo la Vwawa kwa
ushirikiano wanaoendelea kunipa katika kipindi chote cha kuwawakilisha hapa
Bungeni. Napenda kuwahimiza kuendelea kuniamini na kuiamini Serikali ya Awamu
ya Tano na kwamba maendeleo ya Jimbo letu yanategemea sana kufanya kazi kwa
pamoja. Aidha kwa namna ya peke ninawabongeza sana Naibu mawaziri Mh. Omary
Tebeta Mgumba (mb) na Hussein Mohamed Bashe (Mb) kwa jinsi wanavyonisaidia
katika kusimamia na kutekeleza majukumu ya wizara ya kilimo. Vile nawapongeza
Katibu mkuu Ndg Gelard Kusaya, Naibu katibu Mkuu. Prof. Siza Tumbo,
wakurugenzi na vitengo, wakuu wa Taasisi, Bodi na wakala zilizo chini ya
wizara kwa ushirikiano na kazi nzuri wanazoendeleza kuzitekeleza ili
kufanikisha malengo ya kilimo nchini.
10. Mheshimiwa
Spika, Awali ya yote nampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa kutoa msukumo wa kuendeleza Sekta ya Kilimo. Aidha, katika hotuba
yake aliyoitoa tarehe 20 Novemba, 2015 akifungua rasmi Bunge la 11 la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania – Dodoma alisisitiza kutekeleza ahadi alizozitoa kwa
wakulima kupitia Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya 2015-2020. Wizara
imetekeleza ahadi hizo kupitia Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya
Pili (ASDP II) na kuwezesha kilimo kuchangia katika uchumi na maendeleo ya
Taifa letu, hususan katika maeneo ya usalama wa chakula na lishe, ajira,
upatikanaji wa malighafi za viwanda na kuchangia katika kupunguza umaskini na
kuongeza kipato cha wakulima.
11. Mheshimiwa
Spika, baadhi ya ahadi alizotoa ni pamoja na kuimarisha huduma za
ugani, upatikanaji na usambazaji wa pembejeo, zana za kisasa za kilimo, masoko
ya uhakika ya mazao, kuimarisha upatikanaji wa mikopo kwa ajili ya kilimo na
kuondoa ushuru, kodi na tozo ambazo ni kero kwa ajili ya maendeleo ya kilimo.
2.
MCHANGO WA SEKTA YA KILIMO KATIKA UCHUMI
12. Mheshimiwa
Spika, kilimo kimeendelea kuwa ni mhimili muhimu katika maendeleo ya
uchumi wa taifa letu. Katika kipindi cha miaka mitano, Pato la Taifa
linalotokana na kilimo, kwa kutumia bei za Mwaka 2015 limeongezeka kwa asilimia
17 kutoka shilingi trilioni 25.2 Mwaka 2015 hadi shilingi trilioni 29.5 Mwaka
2019. Vilevile, sekta imeendelea kutoa ajira kwa Watanzania kwa asilimia
58 Mwaka 2018, imechangia asilimia 28.2 ya Pato la Taifa ambapo sekta ndogo ya
mazao imechangia asilimia 16.2. Hii imetokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa
bidhaa mbalimbali zikiwemo vyakula vinavyotokana na mazao ya kilimo.
Aidha, kati ya mwaka 2015 hadi 2019 sekta ya kilimo imeendelea kukua kwa
wastani wa asilimia 5.2 ambapo sekta ndogo ya mazao imeendelea kukua kwa
wastani wa asilimia 5.8.
3.1 Fedha
Zilizoidhinishwa
13. Mheshimiwa Spika,
Wizara ya Kilimo kupitia Fungu 43, Fungu 05 na Fungu 24 iliidhinishiwa na Bunge
lako tukufu jumla ya Shilingi bilioni 253.86 ili kutekeleza
majukumu yake. Kati ya fedha hizo Shilingi bilioni 77.78 ni
kwa matumizi ya kawaida na Shilingi bilioni 176.08 kwa ajili
ya miradi ya maendeleo.
5. HOMA
KALI YA MAPAFU (COVID-19)
14. Mheshimiwa Spika, mlipuko
wa ugonjwa wa homa kali ya mapafu (COVID-19) unaosababishwa na virusi vya
Corona umeathiri sekta mbalimbali za kiuchumi nchini ikiwemo sekta ndogo ya
mazao. Tathmini imefanyika na kubaini kuwa uzalishaji wa mazao ya chakula kwa
mwaka 2019/2020 haujaathirika kwa kuwa pembejeo zimeshawasili nchini.
Aidha, katika
kukabiliana na uhaba wa mbolea unaoweza kutokea kutokana na kuendelea kuwepo
kwa tatizo la COVID-19, Wizara imeagiagiza TFRA kuhakikisha mbolea zote
zinaagizwa mapema kipindi hiki kabla ya msimu ujao kuanza.
15. Mheshimiwa Spika, mazao
ya asili ya biashara ambayo ni pamba, korosho na kahawa misimu yake ya mauzo
imeishia mwezi Machi, 2020 na hivyo kutoathirika na ugonjwa huo. Aidha, kwa zao
la tumbaku wakulima wameshafunga mikataba na wanunuzi kwa ajili ya msimu
2020/21 na hivyo kutoathiriwa na Covid-19. Mazao ambayo yameonesha dalili za
kuathirika ni chai na mazao ya bustani ambayo masoko na usafirishaji wake nje
ya nchi umeathiriwa. Vilevile, ugonjwa wa COVID-19 iwapo utaendelea kwa muda
mrefu unaweza ukaathiri soko la pamba, korosho kahawa, na mazao mengine
yanategemea minada ya moja kwa moja.
16. Mheshimiwa Spika, ili
kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na ugonjwa wa COVID-19, serikali
imepanga kununua tani 300,000 za chakula kupitia NFRA, kuhakikisha sekta
binafsi zinahifadhi kwenye maghala, kutumia mfumo wa Soko la Bidhaa (TMX) kwa
mazao ambayo hutegemea zaidi wanunuzi kutoka nje ya nchi kama vile zao la
korosho, kahawa, pamba, n.k., kutumia balozi zetu nje ya nchi kutafuta manunuzi
na masoko, na kutumia soko la moja kwa moja, n.k. hivyo kwenye upande wa mazao
ya chakula hii ni fursa ya kuweza kuuza Zaidi kuliko muda mwingine.
3.2 Utekelezaji
wa Maeneo ya Kipaumbele kwa Mwaka 2019/2020
17. Mheshimiwa
Spika, katika
mwaka 2019/2020, Wizara imeendelea kutekeleza maeneo ya kipaumbele ya kuongeza
uzalishaji na tija kwenye kilimo kwa kuimarisha upatikanaji wa pembejeo za
kilimo, udhibiti wa visumbufu, matumizi ya zana bora za kilimo na huduma za
ugani; ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji; ujenzi wa miundombinu
ya kuhifadhi mazao ya kilimo na masoko; kufanya utafiti wa kilimo na kuzalisha
teknolojia kwa mazao ya mahindi, muhogo, ngano, michikichi, ufuta, alizeti,
pamba na mpunga.
4.
MAFANIKIO YA WIZARA YA KILIMO KATIKA KIPINDI CHA SERIKALI YA AWAMU YA TANO
18. Mheshimiwa
Spika, katika
kipindi cha miaka minne Wizara imepata mafanikio makubwa katika maeneo ya
usalama wa chakula na lishe; uzalishaji wa mazao makuu ya biashara; upatikanaji
wa pembejeo za kilimo; viwanda vya kuchakata mazao ya kilimo na masoko;
utafiti, huduma za ugani na mafunzo; hifadhi ya mazao; uzalishaji wa mazao ya
bustani; kuimarika kwa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko; kuimarika kwa
ushirika; kuimarika kwa kilimo cha umwagiliaji; ongezeko la ushiriki wa vijana
katika kilimo; matumizi bora ya ardhi; kuhuisha mifumo na sera za kilimo na
kuanzishwa kwa kanzidata ya wakulima na wadau mbalimbali wa kilimo.
4.1
Usalama wa Chakula na Lishe
19. Mheshimiwa
Spika,
katika kipindi cha miaka minne (4) upatikanaji wa chakula umeendelea kuimarika
na hivyo kuwezesha nchi yetu kujitosheleza kwa chakula kwa wastani wa asilimia
121 na kuwa na wastani wa ziada ya tani 2,798,700.60. Aidha katika mwaka
2019/2020 upatikanaji wa chakula ulifikia tani milioni 16.2 ukilinganisha na
mahitaji ya chakula ya tani milioni 13.8. Hivyo ziada ya chakula ilikuwa tani
2,473,774 na kuwa na kiwango cha utoshelevu cha asilimia 118.
Hali ya
Lishe nchini
20. Mheshimiwa
Spika, kulingana
na taarifa ya mapitio ya kati (Mid Term Review) ya hali ya lishe nchini katika
utekelezaji wa Mpango Jumuishi wa Kitaifa wa lishe wa mwaka 2016-2021)
uliyofanyika mwaka 2019, inaonesha kuwa udumavu kwa watoto chini ya miaka
mitano umepungua kutoka asilimia 34 mwaka 2015 kufikia asilimia 32 mwaka 2018.
Aidha, Kiwango cha ukondefu kwa watoto chini ya miaka mitano kitaifa
kimeendelea kushuka kutoka asilimia 3.8 hadi asilimia 3.5 na pia upungufu wa
damu kwa akina mama umepungua kutoka asilimi 44.7 hadi kufikia asilimia 28.7
kwa kipindi hicho.
21. Mheshimiwa
Spika, jukumu
la serikali ni kuhakikisha kuwa mazao mbalimbali ya chakula yenye virutubishi
kwa wingi yanazalisha yakiwemo viazi lishe” na maharagwe yaliyoongezewa madini
chuma na zinki. Uzalishaji na utumiaji wa mazao haya unachangia kupunguza
tatizo la upungufu wa damu unaosababishwa na ukosefu wa madini chuma na tatizo
la upungufu wa vitamin A hususan kwa akina mama walio katika umri wa kuzaa na
watoto chini ya miaka mitano.
4.2
Uzalishaji wa Mazao Makuu ya Biashara
22. Mheshimiwa
Spika, uzalishaji
wa mazao makuu ya biashara yakiwemo pamba, kahawa, chai, pareto, tumbaku,
korosho, mkonge na miwa umeongezeka kutoka jumla ya tani 796,502 Mwaka
2015/2016 hadi jumla ya tani 1,144,631 Mwaka 2018/2019 sawa na
ongezeko la asilimia 43.7. Aidha zao la miwa limeongoza likifuatiwa na korosho
na Pamba.
23. Mheshimiwa
Spika, vilevile
katika kipindi hicho cha miaka minne kiasi cha tani 1,613,000 za mazao ya
kahawa, pamba, katani, chai, tumbaku na korosho kiliuzwa nje ya nchi na
kuliingizia Taifa jumla ya Dola za Marekani Milioni 3,419.77 sawa na Shilingi
trilioni 6.9. Aidha, Wizara kupitia Bodi ya Tumbaku imeuza jumla ya tani 500 za
tumbaku ya daraja la chini (Reject) ambayo mapato yake yamesaidia kupunguza
gharama za uzalishaji kwa wakulima na kuwaongezea kipato.
Uzarishaji
wa miwa na sukari
24. Mheshimiwa
Spika, hadi
Aprili, 2020 uzalishaji wa Sukari ulifikia tani 298,948.61 sawa na asilimia 86
ya lengo la kuzalisha tani 345,296 za Sukari. Hata hivyo uzalishaji wa sukari
ulikumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uchakavu wa mitambo ya viwanda,
kuharibika kwa mitambo, mlipuko wa ugonjwa wa vidung’ata wa njano na mvua
nyingi zinazoendelea kunyesha sehemu mbalimbali. Ili kukabiliana na
upungufu huo, serikali ilitoa kibari cha kuingiza tani 40,000 za sukari kutoka
nje ya nchi kwa kampuni nne za Kagera Sugar, Mtibwa, Kilombelero na TPC Moshi
mwezi machi 2020. Kikao cha pamoja cha wawakilishi wa wazalishaji, serikali,
TRA, na Bodi ya sukari killikaa pamoja na kukubaliana bei kuwa haitapanda. Hata
hivyo kumejitokeza mambo yafuatayo; kuchelewa kiingia nchini kwa sukari
kutokana na tatizo la COVID 19, baadhi ya wanunuzi kuficha sukari, n.k.
Kutokana na hali hiyo, Wizara kupitia Bodi ya Sukari baada ya kufanya uchambuzi
wa kina, na kwa kutumia Sheria ya Tasnia ya Sukari Sehemu ya nne (4)(e) Kifungu
cha 11A ilichukua hatua ya kutangaza bei elekezi ya jumla na rejareja ya sukari
katika Mikoa yote ya Tanzania Bara kwa lengo la kukabiliana na
wafanyabiashara wasio waaminifu.
25. Mheshimiwa
Spika
4.3
Mazao ya Bustani
26. Mheshimiwa
Spika, katika
kipindi cha miaka minne, uzalishaji wa mazao ya bustani umeongezeka kutoka
tani 5,931,900 mwaka 2015/2016 hadi tani 6,556,102 mwaka
2018/2019. Thamani ya mauzo ya mazao ya bustani yakiwemo mbogamboga na maua nje
ya nchi yameongezeka toka Dola za Marekani milioni 412 mwaka 2015 hadi Dola za
Marekani milioni 779 mwaka 2018/2019. Ongezeko hilo la mauzo linaifanya Tasnia
ya mazao ya bustani kuchangia asilimia 38 ya fedha za kigeni zinazotokana na
sekta ya kilimo.
27. Mheshimiwa
Spika, Katika
kipindi hicho, uwekezaji katika mazao ya bustani kupitia sekta binafsi chini ya
mwamvuli wa TAHA umefikia Dola za Marekani milioni 30. Aidha zao la parachichi
limeonesha mafanikio makubwa katika kipindi cha miaka minne ambapo uzalishaji
umeongezeka kutoka tani 20,000 Mwaka 2015 hadi kufikia tani 190,000 Mwaka 2018.
Mauzo yenye thamani ya Dola za marekani Milioni 8.5 yamefanyika katika soko la
ulaya hususan nchi za Ufaransa, Uholanzi na Uingereza.
4.4
Upatikanaji wa Pembejeo za Kilimo
4.4.1
Mbegu
28. Mheshimiwa
Spika, katika
kipindi cha miaka minne upatikanaji wa mbegu bora umeongezeka kutoka tani
36,614.28 mwaka 2015/2016 hadi tani 76,725.52 mwaka 2019/2020 sawa na ongezeko
la asilimia 110. Aidha, uzalishaji wa ndani wa mbegu bora umeongezeka kutoka
tani 20,604.97 mwaka 2015/2016 hadi tani 69,173.17 mwaka 2019/2020.
Vilevile, uzalishaji wa miche umeongezeka kutoka miche 5,000,000 mwaka 2015/16
hadi kufikia miche 25,285,859 mwaka 2019/20. Pamoja na mambo mengine,
mafanikio hayo yametokana na kuongezeka kwa eneo la uzalishaji wa mbegu na
miche kutoka hekta 10,887 hadi hekta 94,368. Vile vile serikali imeimarisha
maabara ya TOSCI na hivyo kupata ithibati ya Shirika la Kimataifa la Uthibiti
wa Ubora wa Mbegu (International Seeds Testing Association – ISTA) pamoja na
kujiunga na Skimu za Mbegu za Shirika la Kimataifa (OECD Seed Schemes) ambayo
itaiwezesha nchi kufanya biashara ya mbegu kimataifa.
4.4.2
Mbolea
29. Mheshimiwa
Spika, katika
kipindi hicho Wizara imeimarisha upatikanaji wa mbolea nchini kwa kuanzisha
mfumo wa ununuzi wa pamoja (Bulk Procurement System - BPS) ambao umewezesha
kuongeza upatikanaji wa mbolea kutoka tani 302,482 mwaka 2015/2016 hadi 633,197
mwaka 2019/2020. Mfumo huo umewezesha wakulima kupata mbolea kwa wakati
na bei nafuu. Aidha, idadi ya viwanda vinavyotengeneza mbolea na visaidizi vya
mbolea (fertilizer suppliment) vimeongezeka kutoka viwanda vinne (4) mwaka 2015
hadi viwanda 13 mwaka 2019. Kati ya viwanda hivyo, viwanda viwili (2) ni vya
visaidizi na 11 ni vya mbolea.
4.4.3
Viuatilifu
30. Mheshimiwa
Spika, Upatikanaji
wa viuatilifu kwa ajili ya kudhibiti visumbufu vya milipuko kama vile panya,
nzige, kweleakwelea na viwavijeshi vamizi umeongezeka kutoka tani 4,111.50
mwaka 2015 hadi tani 16,869.10 mwaka 2019.
4.6
Mazingira ya Uwekezaji na Uanzishaji wa Viwanda vya Kuchakata Mazao ya Kilimo
31. Mheshimiwa
Spika, katika
kipindi cha mwaka 2015/16 hadi 2019/20, Serikali imefuta ushuru, tozo na ada
105 na kupunguza tozo nne (4) kati ya 146 zilizokuwa zinatozwa katika mazao ya
kilimo. Hatua hiyo imevutia Sekta binafsi kuwekeza takribani Shilingi Trilioni
3.7 kwenye mnyororo wa thamani wa kuendeleza mazao ya chai, kahawa, mkonge,
ngano, shayiri na mpunga. Aidha, ajira katika mnyororo wa thamani ya mazao ya
kilimo zimeongezeka kutoka wastani wa ajira 3,880,262 Mwaka 2015/16 hadi
kufikia wastani wa ajira 5,204,607 Mwaka 2018/19.
32. Mheshimiwa
Spika, Wizara
imehamasisha ujenzi wa viwanda ili kuongeza thamani ya mazao ya kilimo na
kutengeneza ajira kwa watanzania. Katika kipindi cha miaka minne, jumla ya
viwanda vipya 189 vya kuchakata mazao vimeanzishwa vikiwemo vya korosho 9, chai
3, kahawa 59, pamba 36, mkonge 81 na pareto 1.
4.7
Upatikanaji wa Masoko ya Mazao ya Kilimo
33. Mheshimiwa
Spika, katika
kipindi cha miaka minne (4) Wizara imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa
ajili ya upatikanaji wa masoko ya uhakika kwa mazao ya kilimo ndani na nje ya
nchi. Katika kufikia azma hiyo, Wizara imeanzisha kitengo cha Masoko
(Agricultural Marketing Division) katika Idara ya Maendeleo ya Mazao
inayosimamia utafutaji wa masoko, kufanya tafiti za masoko na bei za mazao
pamoja na kufuatilia mifumo ya uuzaji wa mazao.
4.8
Utafiti, Huduma za Ugani na Mafunzo ya Kilimo
34. Mheshimiwa
Spika, Katika
kipindi hicho TARI kwa kushirikiana na sekta binafsi imegundua aina 124 za
mbegu bora. Aidha, kati ya hizo kampuni binafsi zimegundua aina 35
za mbegu bora za mazao ya kilimo. Vilevile, utafiti wa kupima afya ya udongo na
kuandaa ramani zinazoonesha mtawanyiko na viwango vya mboji (Organic carbon)
pamoja na uchachu (pH) wa udongo katika mikoa yote nchini umefanyika.
35. Mheshimiwa
Spika, Wizara
kupitia vyuo vyake 14 imetoa wataalam wa kilimo 7,530 na 6,146 wamehitimu
katika vyuo binafsi 12 ngazi ya Astashahada na Stashahada za kilimo. Aidha, jumla
ya maafisa ugani 902 na wakulima 42,192 wamepatiwa mafunzo kuhusu kanuni za
kilimo bora, teknolojia mbalimbali za uzalishaji, jinsia na masoko.
4.9
Hifadhi ya mazao
36. Mheshimiwa
Spika, Mwaka
2015 nchi ilikuwa na jumla ya maghala 3,400 yenye uwezo wa kuhifadhi tani
2,774,106 za mazao ya chakula. ujenzi na kukarabati miundombinu ya hifadhi
yavihenge 57 na ghala 118 zenye uwezo wa kuhifadhi jumla ya tani 203,000 na
tani 100,700 mtawalia na hivyo kuongeza uwezo wa kuhifadhi kutoka tani
2,774,106 mwaka 2015/2016 hadi tani 3,077,806 mwaka
2019/2020 sawa na ongezeko la asilimia 11.
4.11
Kuimarisha Ushirika
37. Mheshimiwa
Spika, Ushirika
umeendelea kuimarika ambapo Vyama vya Ushirika vimeongezeka kutoka 7,394 mwaka
2015 hadi 11,626 mwaka 2019 sawa na ongezeko la asilimia 57. Vilevile, idadi ya
wanachama wa Vyama vya Ushirika imeongezeka kutoka 2,390,593 mwaka 2015 hadi
5,880,736 mwaka 2019 sawa na ongezeko la asilimia 146. Hata hivyo, Wizara
imechukua hatua ya kuvifuta jumla ya Vyama 3,348 ambavyo vilibainika kuwa ni
hewa na hivyo kubaki na jumla ya Vyama vya ushirika 8,611 kwenye
daftari/rejista ya Vyama vya ushirika nchini.
38. Mheshimiwa
Spika, katika
kipindi hicho, thamani ya mikopo inayotolewa na Vyama vya Ushirika wa Akiba na
Mikopo (SACCOS) imeongezeka kutoka Shilingi bilioni 899.2 mwaka 2015 hadi
Shilingi trilioni 1.5 mwezi Machi, 2020. Aidha, idadi ya viwanda
vinavyomilikiwa na Vyama vya Ushirika imeongezeka kutoka viwanda 304 mwaka 2015
hadi viwanda 379 mwaka 2019.
4.12
Kilimo cha Umwagiliaji
39. Mheshimiwa
Spika, eneo la
kilimo cha umwagiliaji limeongezeka kutoka hekta 461,326 mwaka 2015/2016
hadi hekta 694,715 mwaka 2019/20 sawa na ongezeko la asilimia 33.6.
Aidha, tija ya uzalishaji katika skimu za umwagiliaji zilizoendelezwa
imeongezeka kutoka wastani wa tani 1.8 – 2.0 kwa hekta mwaka 2015/2016 hadi
kufikia wastani wa tani 4.0 – 5.0 kwa hekta 2019/2020 kwa zao la mpunga; tani
1.5.
40. Mheshimiwa
spika, aidha
miradi 179 iliyogharimu shilingi 96,188,597,689.55 imetekelezwa. Kati ya miradi
hiyo, miradi 56 inasubiri kuzinduliwa. Miradi iliyokamilika ni pamoja na
mradi wa uboreshaji miundombinu ya skimu ya umwagiliaji ya Dakawa yenye ukubwa
wa hekta 2,000 iliyogharimu Shilingi 21,156,050,278; Skimu 9 kati ya skimu 16
zenye ukubwa wa hekta 2,547 za Mradi wa Kuendeleza Skimu za Umwagiliaji za
Wakulima Wadogo (SSIDP); ukarabati wa miradi 4 ya skimu za umwagiliaji zenye
jumla ya ukubwa wa hekta 2,000 iliyogharimu shilingi 1,166,220,000.
4.13
Mfumo wa Vibali kwa Njia ya Kielektroniki (ATMIS)
41. Mheshimiwa
Spika, mfumo
wa vibali kwa njia ya kielektroniki (ATMIS) unaolenga kutoa huduma za utoaji
vyeti vya usafi wa mazao ya mimea na vibali vya kuingiza na kuuza mazao nje ya
nchi umeanzishwa. Mfumo huo umepunguza muda wa kupata kibali kutoka siku saba
(7) za awali hadi siku moja (1) kwa wafanyabiashara. Vilevile, umechangia
kudhibiti mianya ya udanganyifu wa nyaraka na kuongeza ukusanyaji wa maduhuli
ya Serikali.
4.14
Uanzishwaji wa Kanzidata ya Wakulima
42. Mheshimiwa
Spika, Mfumo
wa Usajili wa Wakulima (Farmers Registration System-FRS) na kutengeneza
kanzidata ya wakulima ambayo itasaidia kuwatambua na kuwapatia vitambulisho,
kuainisha mahitaji yao ikiwemo pembejeo za kilimo, huduma za kifedha na masoko
na hatimae kuweka mipango ya kuwahudumia umeanzishwa. Hadi Aprili, 2020 jumla
ya wakulima 1,275,220 (88.1%) katika mazao nane makuu ya kibiashara
ambayo ni korosho, pamba, kahawa, chai, mkonge, pareto, tumbaku na
sukari wamesajiliwa kupitia mfumo huo
4.15
Bima ya mazao
43. Mheshimiwa
Spika, serikali
kwa kushirikiana na wadau wa huduma za Bima ikiwemo Mamlaka ya Kudhibiti
Shughuli za Bima nchini (TIRA), Shirika la Bima la Taifa (NIC), kampuni binafsi
tano (5) za bima zimeanzisha Bima ya Mazao kwa lengo la kumsadia mkulima
kujikinga na athari za majanga ya asili na mabadiliko ya tabianchi pamoja na
kupata dhamana ya mkopo.
44. Mheshimiwa
Spika, Wizara
imekamilisha mfumo wa kuwasajili wadau wote wa sekta ya kilimo ikiwemo Sekta
Binafsi (Stakeholders mapping). Hadi kufikia tarehe 30 Aprili, 2020, jumla
ya wadau wa sekta binafsi 564 wamesajiliwa ambapo Wazalishaji na wasambazaji wa
pembejeo ni 198, Wazalishaji wa bidhaa za kilimo 103 na wasindikaji 363. Aidha,
jumla ya miradi 105 inayofadhiliwa na Washirika wa Maendeleo yenye thamani ya
Shilingi Trilioni 3.3 imesajiliwa kwenye mfumo. Mfumo huo utaiwezesha Serikali
kutambua juhudi na uwekezaji wa wadau wote na kuimarisha ushirikiano kati yao
na Serikali katika kuendeleza sekta ya kilimo.
45. Mheshimiwa
Spika, katika
mwaka 2020/2021, Wizara itaendelea kutekeleza Maeneo 10 ya vipaumbele
kupitia Fungu 43, 24 na 05 katika Idara, Vitengo, Tume na Taasisi za
Wizara. Mpango wa bajeti umeweka msisitizo kwenye kilimo kitakachohakikisha
upatikanji wa chakula cha kutosha, upatikanaji wa malighafi kwa ajili ya
viwanda na kufanya kilimo cha kibiashara.
46. Mheshimiwa Spika, Maeneo
ya kipaumbele ni pamoja na Kuendelea na utekelezaji wa Progamu ya
Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II); Kuboresha mifumo ya
kitaasisi, Bodi na Sheria za Kilimo, kupata ujuzi na maarifa ya kilimo chenye
tija, kurahisisha upatikanaji wa huduma za pembejeo na masoko; Ujenzi na ukarabati
wa miundombinu ya umwagiliaji, maghala, masoko na miundombinu ya
kuhifadhi mazao ya kilimo; na Kuimarisha uzalishaji wa mbegu bora za mazao na
upatikanaji wa pembejeo nyingine za kilimo na kuzisambaza kwa wakulima.
47. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2020/2021,
Wizara imepanga kutekeleza malengo na shabaha zifuatazo; kuzalisha tani
18,000,000 za mazao ya chakula; kuzalisha jumla ya tani 5,269,858 za
mazao ya asili ya biashara yakiwemo pamba (400,000), korosho (300,000), chai
(40,000), kahawa (90,000), miwa (4,246,630), pareto (2,800), mkonge (125,428)
na tumbaku (65,000); Kuhakikisha upatikanaji wa mbolea tani 760,000;
Kuhakikisha upatikanaji wa Mbegu tani 115,000; Kuhakikisha upatikanaji wa
Viuatilifu tani 22,000; Kuzalisha tani 8,500,000 za mazao ya bustani; Kuhifadhi
chakula kiasi cha tani 300,000; Kusimamia utafutaji na upatikanaji wa masoko ya
mazao ya wakulima; Kununua na kuuza tani 500,000 za nafaka na tani 1,200,000 za
muhogo mkavu kupitia Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB). Aidha, wanafunzi
2,600 kupitia vyuo 14 vya mafunzo ya kilimo watadahiliwa (MATIs); Kukarabati
vyuo tisa (9) vya mafunzo ya Kilimo na Vituo vya utafiti wa kilimo vinne (5) na
Kuendelea na zoezi la usajili wa Wakulima katika mazao mengine pamoja na
usajili wa wadau wa kilimo.
48. Mheshimiwa
spika pia
wizara itakamilisha ujenzi na ukarabati wa skimu 17 za umwagiliaji zenye ukubwa
wa hekta 8,536; kukamilisha usanifu na upembuzi wa skimu ya Mkombozi-Iringa
(hekta 10,000), mabwawa na skimu za Luiche-Kigoma (hekta 3,000) na Ibanda-Sengerema/Geita
(hekta 1,200), skimu za Ilemba (Sumbawanga – hekta 800) na Makwale (Kyela
– hekta 3,500) pamoja na mabwawa ya Nyisanzi (Chato – hekta 260), Kisese
(Kondoa-hekta 2,000), Msia (Mbozi – hekta 100), Idudumo (Nzega-hekta 200) na
Masasi (Chato – hekta 530); na Kujenga maghala 12 yenye uwezo wa kuhifadhi tani
2,000 na kufundisha vijana 400 kuhusu teknolojia ya vihenge vya kisasa kupitia
mradi wa TANIPAC.
7. SHUKRANI
49. Mheshimiwa
Spika, kabla
sijamaliza hotuba yangu naomba nitoe shukrani za dhati kwa taasisi, makundi, na
wadau mbalimbali tunaoshirikiana katika kuendeleza kilimo cha Tanzania.
Kwanza,
ninawashukuru kwa dhati watumishi wote wa Wizara; na wadau wa Sekta ya
Kilimo kwa juhudi, ushirikiano na ushauri uliowezesha kutekelezwa kwa majukumu
ya Wizara kwa mwaka 2019/2020 pamoja na kuandaa Hotuba hii. Ni matarajio yangu
kwamba, nitaendelea kupata ushirikiano wao katika mwaka 2020/2021.
50. Mheshimiwa Spika,
naomba nitumie fursa hii kuzishukuru Nchi na Mashirika mbalimbali ya Kimataifa
ambayo yamesaidia katika juhudi za kuendeleza kilimo. Nachukua fursa hii kutaja
baadhi yao kama ifuatavyo: Serikali za Japan, Marekani, Uingereza, Ireland,
Malaysia, China, Indonesia, Korea ya Kusini, India, Misri, Israel, Ubelgiji,
Ujerumani, Finland, Norway, Brazil, Uholanzi, Vietnam, Canada na Poland.
Ninayashukuru pia Mashirika na Taasisi za Kimataifa zifuatazo: Benki ya Dunia,
Benki ya Maendeleo ya Afrika, AU, IFAD, DFID, UNDP, FAO, JICA, EU, ENABEL, GIZ,
UNICEF, WFP, CIMMYT, ICRISAT, ASARECA, USAID, KOICA, ICRAF, IITA, IRRI, ILRI na
CABI. Nyingine ni EAC, SADC, AVRDC, AGRA, KILIMO TRUST, CIP, CIAT/PABRA, UNEP,
WARDA, Shirika la Kudhibiti Nzige wa Jangwani (DLCO-EA) na HELVETAS.
Wadau wengine ni Shirika la Kudhibiti Nzige Wekundu (IRLCO-CSA),Bill and Melinda
Gates Foundation, Gatsby Trust, Rockfeller Foundation, Clinton Foundation,
Aga Khan Foundation, Unilever, Kampuni za TAHA fresh Limited, Africado na
Rugwe Avocado Companyna Asasi zisizo za kiserikali nyingi ambazo hatuwezi
kuzitaja zote hapa.
51. Mheshimiwa
Spika,natoa shukrani za wakulima wote nchi nzima kwa kazi kubwa wanazofanya
kuendeleza kilimo nchini. Ni wazi kuwa mafanikio haya makubwa ya kilimo
yanatokana na jududi na ushirikiano mkubwa na serikali. Kipeke nirudie
kuwashukuru wananchi wa Jimbo langu la Vwawa kwa namna wanavyoniunga mkono na
kunipa ushirikiano. Naomba wote watumbue kuwa kilimo ni chakula, maisha,
uchumi, biashara, viwanda na ajira. 8.
MAOMBI YA FEDHA KWA MWAKA 2020/2021.
8.1 Makusanyo
ya Maduhuli
52. Mheshimiwa
Spika,katika
mwaka 2020/2021, Wizara inatarajia kukusanya Shilingi 5,793,400,000 kutokana
na ada za ukaguzi wa mazao yanayouzwa nje ya nchi au kuingizwa nchini, uuzaji
wa nyaraka za zabuni, ukodishaji wa mitambo ya Tume ya Umwagiliaji.
8.2 Fedha
kwa Mafungu yote (43, 24 na 05)
53. Mheshimiwa
Spika,katika
mwaka 2020/2021, Wizara ya Kilimoinaliomba Bunge lako Tukufu liidhinishe
jumla ya Shilingi 229,839,808,000 kupitia Fungu 43,
Fungu 05 na Fungu 24 kama ifuatavyo;
8.2.1 Fedha
kwa Fungu 43
54. Mheshimiwa
Spika,katika
mwaka 2020/2021, Wizara inaomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi 202,504,117,000 kupitiaFungu
43 kwa ajili ya matumizi ya Kawaida na Maendeleo. Kati ya fedha hizo,
Shilingi 137,273,144,000 ni kwa ajili ya kutekeleza miradi ya
Maendeleo. Aidha, Shilingi 65,230,973,000 ni kwa ajili
yamatumizi ya kawaida, ambapo Shilingi 43,599,187,000 ni kwa
ajili ya mishahara na Shilingi 21,631,786,450 ni kwa ajili ya
matumizi mengineyo.
8.2.2 Fedha
kwa Fungu 05
55. MheshimiwaSpika, jumla
ya Shilingi 17,726,845,000 zinaombwa. Kati ya fedha hizo,
Shilingi 12,801,180,000 ni kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya
Maendeleo na, Shilingi 4,925,665,000 ni kwa ajili ya Matumizi
ya Kawaida ambapo Shilingi 4,040,481,000 ni kwa ajili ya Mishahara
ya Watumishi wa Tume na Shilingi 885,184,000 ni kwa ajili ya
Matumizi mengineyo.
8.2.3 Fedha
kwa Fungu 24
56. Mheshimiwa
Spika, jumla ya Shilingi 9,608,846,000 zinaombwa kwa
ajili ya matumizi ya kawaida ambapo Shilingi
No comments:
Post a Comment