|
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo akitoa maelekezo kwa watendaji juu ya namna rahisi ya
kuwashirikisha wadau ili kuweza kufanikiwa kampeni ya ugawaji wa
vyandaru kwa kaya.
Katika hatua kukabiliana na mbu waenezao ugonjwa wa Malaria
nchini, Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii jinsia, Wazee na
Watoto kwa ushirikiano na Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) imeendelea kutekeleza kampeni mbalimbali za kudhibiti Malaria ikiwa
ni miongoni mwa hatua za kutokomeza ugonjwa huo hadi kufikia mwaka 2030.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya Peter Gitanya amesema
kuwa Kampeni hiyo ambayo imelenga kugawa vyandarua 719,254 kwa mkoa wa Rukwa ni
muendelezo wa kampeni kubwa tatu za uhamasishaji wa ugawaji wa vyandarua kwa kaya zilizowahi kufanyika miaka ya 2009, 2010 na
2015/2016 na kuongeza kuwa Bohari ya Dawa (MSD) itahusika na usafirishaji wa
vyandarua kutoka maghala yao katika kila mkoa hadi kituo cha ugawaji katika Kijiji
ama mtaa husika | | |
|
|
Shekhe
wa Mkoa wa Rukwa Shekh Rashid Akilimali (katikati) akisikiliza kwa
makini mafunzo ya kampeni ya uhamasishaji wa ugawaji wa vyandandarua
katika kaya yaliyofanya na wawakilishi wa Wizara ya Afya mkoani Rukwa.
“Halmashauri ambako kampeni itafanyika ni zile
halmashauri ambazo zina kiwango cha chini cha umiliki wa vyandarua, chini ya
40%, na pia maambukizi ya malaria yapo katika kiwango cha juu na cha kati,
Halmashauri zenye kiwango cha chini cha uwepo wa malaria zilizozungukwa na halmashauri
zenye kiwango cha juu na cha kati cha uwepo wa malaria na halmashauri ambazo
mpango wa ugawaji wa vyandarua kupitia wanafunzi shuleni haufanyiki,”
Alisisitiza.
Katika kusisitiza hilo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh.
Joachim Wangabo amewataka wahusika wote wa kampeni hiyo kushirikiana kwa karibu
katika kufikisha elimu iliyosahihi kwa wananchi juu ya matumizi sahihi ya
vyandarua na kuongeza kuwa ili kufanikisha mpango wa serikali kufikia uchumi wa
kati ifikapo mwaka 2025 ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha tunapambana na
maradhi hayo ili kuwa na jamii yenye afya na yenye uwezo wa kuzalisha.
|
|
|
|
Baadhi ya Washiriki wa mafunzo ya kampeni ya uhamasishaji wa ugawaji wa vyandandarua katika kaya yaliyofanya na wawakilishi wa Wizara ya Afya mkoani Rukwa. |
“Mimi nitoe wito tu kwamba ili mpango huu uweze
kufanikiwa, tunahitaji tushikamane, tushirikiane kwa nguvu zote, kufikisha elimu
iliyosahihi kwa wananchi, vinginevyo tusipotoa elimu kwa nguvu zote na watu
wakaelewa tunaweza tukatwanga maji kwenye kinu, kwahiyo jambo kubwa liwe ni
elimu, elimu iwafikie wananchi kwa nguvu zote, kama tulivyoanza hapa
kushirikishana hivi, tuendelee kushusha kuwashirikisha wadau mbalimbali,”
Alisema.
Aidha, aliishauri wizara ya afya na taasisi zilizopo
chini ya wizara hiyo kuona namna ya kufanya utafiti juu ya miti shamba
inayotumika kufukuza mbu katika baadhi ya maeneo vijijini ili wananchi waweze
pia kutumia miti hiyo kwa kuipanda maeneo ya nyumba zao na hatimae kuwafukuza
mbu hao.
Kampeni hiyo itagawa vyandarua 7,097,565 katika Halmashauri
50 kutoka katika mikoa 10 nchini ikiwa na lengo la kugawa vyandarua hivyo vyenye
dawa kwa walengwa kwa asilimia 100 na Kwa mkoa wa Rukwa kampeni hiyo itagawa
vyandaru katika halmashauri zote nne za mkoa kwa kuwatambua walengwa na
kuwahamasisha juu ya matumizi na utunzaji wa vyandarua hivyo.
No comments:
Post a Comment