|
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Sanare akitoa maelekezo kwa Watendaji wa
Wilaya ya Ulanga Wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya Mh. Ngollo Malenya mara
baada ya kukagua soko la Mahenge |
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare amewapongeza
Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Ngollo Malenya na Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya hiyo Jonas Malosa kwa kusimamia vizuri Miradi ya
Maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Wilaya hiyo ikiwemo Hospitali
ya Wilaya.
Loata Sanare
ametoa pongezi hizo Mei 18 mwaka huu baada ya kutembelea Miradi miwili
ya Maendeleo ambayo ni Ujenzi wa Majengo matano ya Hospitali ya Wilaya
ya Ulanga yanayojengwa kwa ufadhiri wa fedha za Global Fund na Ujenzi wa
Soko la Mahenge Mjini.
Sanare
amesema kwa mara ya kwanza amefurahishwa na hatua iliyofikiwa ya
ukamilishaji ya miradi hiyo na kumpongeza Mkuu wa Wilaya Mkurugenzi
Mtendaji pamoja na watendaji wao wote kwa usimamizi wa miradi hiyo na
kuwataka wakamilishe kazi zilizobaki ili wananchi wa Mahenge waanza
kupata huduma zinazokusudiwa.
|
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh.LOATA OLE SANARE katika wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro kukagua utekelezaji wa miradi ya Maendeleo.
“Kwa
ujumla kazi imefanyika nikupongeza Mkurugenzi na Mkuu wa Wilyaa kwa
kusimamia kazi hii vizuri, toka niondoke et list sio kama nilivyoaacha,
ni maelekezo nilitoa wakati ule kwamba rekebisheni hapa na hapa,
nimejiridhisha kazi imefanyika vizuri” alipongeza Sanare
Hata
hivyo amewataka watendaji hao kuendelea kusimamia kazi chache
zilizobaki katika miradi hiyo na kuwataka kusimamia kwa umakini mkubwa
fedha zinazoletwa na Serikali au wadau wengine wa maendeleo zinafanya
kazi iliyokusudiwa.
Amesema
fedha za Serikali zinaletwa kwa ajili ya kuwahudumia wananchi, na lengo
hilo linakamilika pale tu huduma zinapoanza kutolewa kwa wananchi
katika mradi husika, hivyo amewaagiza watendaji hao kukamilisha kazi
hizo kabla ya mwezi Julai 2020 yaani kabla ya mwaka wa fedha wa mwaka
huu kuisha.
Majengo
matano yanayojengwa Katika Hospitali hiyo ya ya Wilaya ni pamoja na
jengo la famasi, jengo la incinerator (kichomea taka), jengo la wodi ya
wanaume, jengo la wodi ya wanawake, na jengp la kliniki ya macho.
Majengo haya manne yamejengwa kwa gharama ya shilingi 400Mil. ikiwa ni
fedha kutoka global fund kupitia OR- TAMISEMI na jengo moja la macho
limejengwa kwa ufadhili wa EYE CARE FOUNDATION kwa gharama ya Tsh. 65
Mil.
Kwa mujibu wa Afisa
Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga Joseph Mkude amesema Mradi wa
Soko hilo ulianza tarehe 17/10/2014 chini ya mpango wa DADP ikiwa ni
uamuzi uliopitishwa na wananchi ukiwa na lengo la kuhakikisha
wafanyabiashara wa mazao ya shambani na mifugo wanapata jengo bora la
kuhifadhia na kuuzia ili kuepuka kufanya biashara katika maeneo yasiyo
rasmi. Mradi huo umegharimu Shilingi 201Mil. Hadi kukamilika kwake.
Katika
hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Sanare amewataka
wafanyabiashara wa Mjini Mahenge husuan wanaojihusisha na uuzaji wa
sukari, kuuza bidhaa hiyo kwa kufuata maelekezo yaliyotolewa na
Serikali.
Ametoa
maelekezo hayo baada ya kutembelea baadhi ya maduka ya Mji wa Mahenge na
kubaini wafanyabiashara hao wakiuza sukari kilo moja shilingi Elfu Nne
tofauti na bei iliyoelekezwa na Serikali na kuwaagiza Mkuu wa Polisi wa
Wilaya ya Ulanga kushirikiana na Afisa Biashara na Maafisa wa TRA
kuwachukulia hatua za kisheria wote wanaouza Sukari kwa bei ya juu.
| |
No comments:
Post a Comment