|
Mkurugenzi wa Upasuaji
wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angella Muhozya akimuonesha Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile maendeleo ya afya ya mgonjwa
aliyefanyiwa upasuaji wa kupandikiza mshipa
wa damu kwenye moyo (Coronary
Artery Bypass Grafting-CABG). Mgonjwa huyo alifanyiwa upasuaji na wataalamu wa
Taasisi hiyo ambapo Dkt. Ndugulile aliwatembelea wagonjwa waliofanyiwa upasuaji
mkubwa wa kusimamisha moyo kwa ajili ya kuwajulia hali.
|
Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imewataka wataalamu wa afya
kuendelea kutibu watu wenye magonjwa mengine kama vile matatizo ya moyo na figo
katika kipindi hiki cha ugonjwa wa Covid-19.
Hayo yamesemwa na
Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Faustine Ndugulile baada ya kuitembelea Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na kuwaona wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa
kupandikiza mishipa kwa wagonjwa wenye matatizo ya moyo.
|
Daktari bingwa wa
wagonjwa walioko katika uangalizi maalum Said Kilindimo kutoka Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) akimweleza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile jinsi wanavyowahudumia wagonjwa walioko katika
chumba hicho. Dkt Ndugulile alitembelea Taasisi
hiyo kwa ajili ya kuwajulia hali wagonjwa waliofanyiwa upasuaji mkubwa wa
kusimamisha moyo.
|
|
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa chumba
cha wagonjwa walioko katika uangalizi maalum (ICU) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
wakati alipotembelea Taasisi hiyo kwa ajili ya kuwajulia hali wagonjwa
waliofanyiwa upasuaji mkubwa wa kusimamisha moyo.
|
Dkt. Ndugulile
amesema pamoja na kuwapo kwa maambukizi ya ugonjwa wa Corona, watu wenye
matatizo ya moyo, kupumua, figo, kisukari pamoja na matatizo mengine wanapaswa
kupatiwa matibabu.
“Tunaweza tukawa
tunapambana na Corona, tukawapoteza wagonjwa wengi kwa sababu tu hatujaweza
kuwapatia huduma ya matibabu ya kisukari, figo, presha au moyo, hivyo nitoe rai
kwa wahudumu wa afya wahakikishe wanaendelea kuwatibu watu wenye magonjwa haya
pamoja na magonjwa mengine,” amesema Dkt. Ndugulile.
|
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua taarifa za mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa kupandikiza mshipa wa damu kwenye
moyo (Coronary artery bypass grafting
(CABG) na wataalamu wa upasuaji wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI). Dkt Ndugulile alitembelea Taasisi hiyo kwa ajili ya kuwajulia hali
wagonjwa waliofanyiwa upasuaji mkubwa wa kusimamisha moyo.
Katika hatua
nyingine, Dkt. Ndugulile amewapongeza wataalamu wa JKCI kwa kufanya upasuaji wa
kupandikiza mishipa kwenye moyo kwa wagonjwa waliokuwa na matatizo ya
moyo.
“Sisi kama
Wizara ya Afya, tunapata faraja sana, mambo kama haya ni mazuri na lazima
tuseme kwa hiyo hii operesheni mliofanya ni kubwa na nje ya nchi ingetugharimu
shilingi milioni 80 hadi 90 kwa mtu mmoja, lakini hapa tumefanya kwa shilingi
milioni 29 kwa kutumia wataalamu wetu na wagonjwa wetu wanaendelea vizuri,”
amesema Dkt. Ndugulile.
|
|
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akimjulia hali
mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa
kupandikiza mshipa wa damu kwenye moyo (Coronary Artery Bypass Grafting-CABG) na wataalamu wa
upasuaji wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Dkt Ndugulile alitembelea
Taasisi hiyo kwa ajili ya kuwajulia hali wagonjwa waliofanyiwa upasuaji mkubwa
wa kusimamisha moyo.
|
Amesema awali
wataalamu kutoka nje ya nchi walikuwa wanakuja kufanya upasuaji kama huo,
lakini sasa Watanzania wazalendo wanafanya baada ya kutoa mishipa kwenye paja
na kwenye kifua cha mgonjwa husika.
“Leo nimekuja kuona
kazi kubwa iliyofanywa na wataalamu wazalendo wa JKCI ya upasuaji wa
kupandikiza mishipa kwenye moyo ili uweze kufanya kazi kwa wagonjwa waliokuwa
wakikabiliwa na matatizo ya moyo,” amesema Dkt. Ndugulile.
|
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa chumba
cha wagonjwa walioko katika uangalizi maalum (ICU) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
wakati alipotembelea Taasisi hiyo kwa ajili ya kuwajulia hali wagonjwa
waliofanyiwa upasuaji mkubwa wa kusimamisha moyo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed
Janabi. Picha na Jackson
Monela - WAMJW
Na John Stephen, WAMJW – Dar es Salaam
Naye Mkurugenzi wa
Upasuaji wa JKCI, Dkt. Angella Muhozya amesema kuwa wagonjwa wote waliofanyiwa
upasuaji na wataalamu wazalendo wanaendelea vizuri na kwamba wataruhusiwa muda
wowote kuanzia sasa.
Mmoja wa wagonjwa
aliyefanyiwa upasuaji wa moyo, Bw. Hamid Nassoro amesema baada ya kufanyiwa
upasuaji hivi sasa anaweza kuzungumza vizuri tofauti na awali alikuwa hawezi
kuzungumza na kwamba tayari ameshaanza mazoezi.
|
No comments:
Post a Comment