Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mbunge wa Iramba Magharibi) akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Hafla iliyofanyika Wilayani Chato Mkoani Geita , , Mei 03, 2020.
Rais Dkt. John Magufuli amemuapisha Dkt. Mwigulu Lameck
Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Chato Mkoani Geita.
Rais Magufuli
amemtaka Waziri Nchemba kuendeleza kazi nzuri iliyofanywa na mtangulizi wake
Marehemu Balozi
Dkt. Augustine Philip Mahiga aliyefariki dunia tarehe 01 Mei, 2020 na pia
kushirikiana na viongozi wenzake katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya Serikali.
“Nimekuteua kwa mara ya pili
kwa sababu naamini unaweza kutekeleza jukumu hili vizuri, na bahati nzuri
vijana wengi niliowateua hawajaniangusha, kwa hiyo nakutakia heri katika kazi
zako na Mungu akutangulie” amesema Rais
Magufuli.
Rais Magufuli
amerejea kauli yake ya kuwataka Watanzania kutokuwa na hofu kubwa dhidi ya
ugonjwa wa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona (Covid-19)
na badala yake waendelee kuchukua tahadhari kama zinavyoelekezwa na wataalamu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini hati ya kiapo ya Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mbunge wa Iramba Magharibi) kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Hafla iliyofanyika Wilayani Chato Mkoani Geita , Aprili 22, 2020.
Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mbunge wa Iramba Magharibi) akizunguma mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuapishwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Hafla iliyofanyika Wilayani Chato Mkoani Geita , , Mei 03, 2020.
Amefafanua kuwa kumekuwa
na upotoshaji mkubwa ambao unasambazwa na baadhi ya watu kupitia mitandao ya
kijamii na kusababisha hofu kubwa kwa wananchi, hali ambayo haisadii kupunguza
tatizo bali kuliongeza na kutengeneza sintofahamu kubwa.
Rais Magufuli
amewahakikishia Walimu ambao ni asilimia 49 ya wafanyakazi wote hapa nchini
pamoja na wafanyakazi wengine kuwa licha ya changamoto za kiuchumi
zinazosababishwa na ugonjwa wa Corona, Serikali imejipanga kuhakikisha wanalipwa
mishahara yao kama kawaida na ametoa wito kwa taasisi za kifedha za kimataifa
zilizoonesha nia ya kusaidia uchumi wa nchi zinazoendelea, kusamehe mikopo
badala ya kutaka kuzikopesha mikopo mipya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza mara baada ya kumuapisha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mbunge wa Iramba Magharibi) kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Hafla iliyofanyika Wilayani Chato Mkoani Geita , Aprili 22, 2020.
Rais Magufuli
amempongeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Prof. Mabula Mchembe (aliyeteuliwa
kushika wadhifa huo hivi karibuni) kwa kuchukua hatua
ya kufanya uchunguzi wa vifaa vya uchunguzi wa ugonjwa wa Corona na ameagiza
maabara kuu ya Taifa inayofanya uchunguzi wa ugonjwa huo ichunguzwe vizuri ili
kujiridhisha juu ya usahihi wa majibu ya sampuli zinazopelekwa kuchunguzwa.
Amewataka Watanzania
wote hasa wanasiasa pamoja vyombo vya habari kuacha kueneza taarifa
zinazowajaza watu hofu ama kutumia ugonjwa huu kwa manufaa ya kisiasa na badala
yake waungane kutoa elimu sahihi na kuhimizana kuchukua tahadhari za
kutoambukizwa.
Mwigulu Lameck Nchemba (Mbunge wa Iramba Magharibi) akisaini hati ya kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuapa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Hafla iliyofanyika Wilayani Chato Mkoani Geita, Mei 03, 2020.
Rais Magufuli
amewapongeza Madaktari, Wauguzi, Wafanyakazi wa Afya na wadau mbalimbai walio
mstari wa mbele katika kuwahudumia watu wanaopatwa na maambukizi ya ugonjwa wa
Corona na amewahakikishia kuwa Serikali inachukua hatua madhubuti za
kukabiliana nao ikiwemo kupata dawa kutoka mahali popote itakapopatikana.
Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mbunge wa Iramba Magharibi) mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Hafla iliyofanyika Wilayani Chato Mkoani Geita. Mei 03, 2020.
PICHA NA IKULU
Ameelezea
kushangazwa kwake na viongozi ambao wanazuia watu wanaofariki dunia
kusafirishwa kwenda kuzikwa nyumbani kwao, na Viongozi wa Dini walioonesha
kutetereka kiimani, hivyo ametoa wito kwa viongozi wote kusimama imara,
kuonesha uongozi wa kweli na kuwapa matumaini wananchi badala ya kuwajaza hofu.
Rais Magufuli amempongeza
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zubeiry bin Ally na Rais wa
Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga pamoja na
viongozi wengine wa Dini waliosimama katika imani na kuwataka Waumini waendelee
kusali, kufunga na kumuomba Mwenyezi Mungu aepushe ugonjwa huu.
No comments:
Post a Comment