Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe Omary Mgumba (Mb) akisisitiza jambo wakati akifunga kikao kazi cha Bodi ya Ushauri ya NFRA jijini Dodoma hivi karibuni. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Serikali
imeweka bayana mpango mkakati wa kuhakikisha kuwa Wakala wa Taifa wa
Hifadhi ya Chakula (NFRA) unajiendesha kibiashara pamoja na kutoa
huduma bora kwa wananchi.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe Omary Mgumba (Mb) amebainisha mkakati huo jijini Dodoma wakati akifunga kikao kazi cha Bodi ya Ushauri ya NFRA hivi karibuni.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe Omary Mgumba (Mb) amebainisha mkakati huo jijini Dodoma wakati akifunga kikao kazi cha Bodi ya Ushauri ya NFRA hivi karibuni.
Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba (Mb) akisisitiza jambo wakati akifunga kikao kazi cha Bodi ya Ushauri ya NFRA jijini Dodoma hivi karibuni. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Mhandisi Yustas Kongolle (Kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa NFRA Ndg Milton Lupa (Kulia)
Ameutaka wakala huo kufanya manunuzi ya mazao kwa ajili ya kuhifadhi kama akiba kwenye maghala ya serikali lakini pia kwa ajili ya biashara kwa kutafuta masoko ndani na nje ya Nchi.
Naibu Waziri Mgumba amesema wakala huo una jukumu la kuhifadhi mazao ya kila aina na siyo kuchagua mazao ya kuhifadhi akitolea mfano Mahindi kuwa ndiyo yamekua yakipewa kipaumbele ukilinganisha na mazao mengine.
Mgumba
amesema kuwa serikali imetathmini mwenendo wa NFRA katika kipindi cha
miaka mitatu mfululizo na kujiridhisha kuwa umeanza kutekeleza majukumu
yake ipasavyo hivyo kuongezewa jukumu muhimu la kununua nafaka kwa ajili
ya kuhifadhi kadhalika kujiendesha kibiashara.
Ameutaka wakala huo kufanya manunuzi ya mazao kwa ajili ya kuhifadhi kama akiba kwenye maghala ya serikali lakini pia kwa ajili ya biashara kwa kutafuta masoko ndani na nje ya Nchi.
Naibu Waziri Mgumba amesema wakala huo una jukumu la kuhifadhi mazao ya kila aina na siyo kuchagua mazao ya kuhifadhi akitolea mfano Mahindi kuwa ndiyo yamekua yakipewa kipaumbele ukilinganisha na mazao mengine.
Amesema
kuwa serikali imetekeleza maelekezo ya ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya
ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa hivyo NFRA inapaswa kuhakikisha
kuwa inanunua nafaka ya kutosha kwa ajili ya kuhifadhi kadhalika kufanya
biashara.
Amesema
kuwa NFRA inapaswa kununua mahindi, mpunga na mtama kwani Mazao hayo ni
fursa kutokana na uhitaji mkubwa wa Chakula nchini na nje ya nchi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Mhandisi Yustas Kongolle akizungumza wakati wa kikao kazi cha Bodi ya Ushauri ya NFRA jijini Dodoma hivi karibuni.
|
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
"Unaweza
kuwa na fedha nyingi lakini Kama huna mipango mizuri ya ununuzi huwezi
kupata Mazao hivyo NFRA ni lazima mjipange vizuri ikiwemo kuongeza
vituo vya ununuzi" Alisema na kuongeza kuwa
"Msije mkanunua
mahindi kisiasa, ni lazima mtenganishe siasa na biashara, mkifanya
hivyo mtajichimbia shimo wenyewe, hivyo lazima mkafanye biashara kwa
ajili ya kupata faida"
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Mhandisi Yustas Kongolle ameishukuru Wizara ya Kilimo kwa kuwaamini yeye na wajumbe wa bodi hiyo kiasi cha kuwateua kuhudumu kwa miaka mitatu huku akisema watafanya kazi kwa bidii na weledi mkubwa zaidi.
"Kuaminiwa na Wizara maana yake Nchi imetuamini, tunaahidi kufanya kazi kwa bidii na kutimiza maagizo yote ambayo tumeelekezwa kufanya ikiwa ni pamoja na kuifanya NFRA ijiendeshe kibiashara," Amesema Mhandisi Kongolle
Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Delphina Mamiro ambaye ni Mjumbe wa Bodi hiyo ya NFRA amesema kuwa Bodi hiyo imejipanga kufanya kazi kubwa na nzuri zaidi ili kutekeleza imani hiyo.
Amesema kuwa mradi wa ujenzi wa maghala na Vihenge vya kisasa utakamilika hivi karibuni hivyo kuna jukumu kubwa na muhimu la kuhakikisha kuwa utekelezaji wa ununuzi unakamilika kwa wakati.
No comments:
Post a Comment