Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Dkt Faustine Ndugulile akitoa maelekezo katika chumba cha teleradiolojia kinachotarajiwa kufanyiwa majaribio siku ya ijumaa tarehe |
Naibu Vaziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile leo ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa maabara ya kisasa ya upasuaji wa Ubongo (Angio Suite) ambao umekamilika kwa asilimia 70.
Maabara hiyo ya kisasa imejengwa kwa gharama ya Tsh bilioni 7.9 ambazo zimetolewa na Serikali ya awrunu ya rano ikihusisha ununuzi wa mtambo kutoka Kampuni ya Simens ya Ujcmmani na ukarabati wa chumba hicho.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Dkt Faustine Ndugulile akitoa maelekezo katika chumba cha teleradiolojia kinachotarajiwa kufanyiwa majaribio siku ya ijumaa |
Pia, Dkt Ndugulile ametembelea mradi wa chumba cha tiba mtandao (Teleradiology) ambao pia unatekelezwa na Serikali ya awamu ya Tano kwa lengo la kutoa tiba kwa njia ya mtandao katika hospitali za Mikoa na Wilaya ambapo picha zitatumwa na kusomwa na majibu kurudishwa ndani ya muda mfupi.
"Lengo la ziara yangu ni kukagua miradi hii ya maabara ya upasuaji wa Ubongo, chumba cha teleradiolojia na kuangalia hali ya utaoaji huduma kacika kipindi hiki cha mlipuko wa ugmtjwa wa Corona. Natoa maelekezo kwamba ujenzi na usimikaji m.itambo ukrunilike na ifi.kapo mwezi Juni, mgonjwa wa kwan.za afanyiwe upasuaji hapa" aliscma Dkt Ndugulile
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akitoa taarifa kuhusiana na hatua ya ujenzi wa mradi wa maabara ya kisasa ya upasuaji wa Ubongo (Angio suite) ambao umekamilika kwa asilimia 70% |
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Boniface amesema ujenzi wa maabara hiyo umekamilika kwa asilimia 70.
"Kukamilika kwa maabara hii ya upasuaji wa Ubongo (Angio suite) kutaleta mageuzi makubwa kwenye matibabu ya Ubongo hapa nchini na nchi nyingine. barani Afrika hivyo kwa namna ya pekee nimshukuru Rais wa Jamhuri ya Ivluungano wa Tanzania Dkt John Pombe wlagufuli kwa uwekezaji mkubwa kwenye hospitali yeni ya MOI" Alisema Dkt Boniface
Maabara hii ya kisasa na ya kipekee itasaidia mataifa mengi ya ukanda huu wa Afrika mashariki na kati.
No comments:
Post a Comment