Wajumbe wa Mabaraza ya Kata Manispaa ya Kinondoni wametakiwa kusimamia sheria ikiwa ni pamoja na kutoa haki kwa Wananchi kuhusiana na masuala ya migogoro ya Ardhi yanapoletwa kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo akizungumza na wajumbe
wa Mabaraza ya Kata ya Halmashauri hiyo jana wakati wa kikao cha
kujadili changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo. Wa kwanza kushito
ni Katibu Tawala Bi. Stella Msofe.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo jana
alipokutana na wajumbe wa Mabaraza hayo kikao kilichokuwa na lengo la
kujadili changamoto mbalimbali zinazo wakabili ambapo pamoja na mambo
mengine amewakumbusha kutambua wajibu na majukumu yao.
Alisema katika kutambua wajibu wao ni vema wakajiepusha kujihusisha na vitendo vya rushwa kwakuwa vinaweza kuharibu uaminifu waliopewa na Halmashauri pamoja na kusababisha migogoro kwa Wananchi.
Katika kikao hicho pia Chongolo na wajumbe wa Mabaraza hayo wamejadili hatua zitakazo wawezesha kupunguza kama sio kumaliza kabisa migogoro katika Wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto za wananchi na hivyo kuleta tija na ufanisi wa utendaji wa kazi zao.
Aidha amewataka wajumbe hao kuweka utaratibu wa kutembelea maeneo ambayo yanashukiwa kuwa na migogoro na kwamba kwakufanya hivyo itakua ni njia sawia katika kukabiliana na changamoto ambazo wananchi wanakutana nazo.
“Mabaraza haya yapokisheria, mnanguvu ya kuwachukulia hatua wale ambao wanakiuka sheria zilizoweka, kukaidi maelekezo mnayotoa, msiwe wanyonge fanyeni kazi kwakusimamia haki na sheria kama ambavyo siku zote Rais wetu Dk. John Pombe Joseph Magufuli anatuelekeza” alisema Chongolo.
Katika hatua nyingine Mhe. Chongolo ameipongeza Idara ya sheria ya Manispaa hiyo kwakufanyakazi bega kwa bega na Mabaraza hayo na hivyo kuleta mafanikio makubwa ya utatuzi wa migogoro ya Ardhi.
No comments:
Post a Comment