Wazairi wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ameziataka ofisi za ardhi za mikoa zilizozanzishwa hivi karibuni kuwa na daftari maalum lenye orodha ya migogoro ya ardhi ili kurahisisha ufuatiliaji sambamba na utatuzi wa migogoro kwenye mikoa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya Ardhi ya Mkoa jana mkoani Manyara, Lukuvi alisema kila ofisi ya ardhi ya mkoa inatakiwa kuwa na daftari zuri lenye orodha ya migogoro yote ya ardhi kwenye mkoa husika ikiwa ni mkakati wa kushughulikia migogoro ya ardhi.
‘’Sasa hivi hatutegemei migogoro mipya maana migogoro tunayoshughulika nayo sasa ni ile ya miaka ya nyuma hivyo muorodheshe migogoro yote iliyopo wilayani na kuanza kuishughulikia’’ alisema Lukuvi.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akioongozwa na Kamishna Msaidizi wa Ofisi ya Ardhi mkoa wa Manyara Leonard Msafiri (kushoto) wakati wa uzinduzi wa ofisi ya ardhi ya mkoa huo jana. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexzander Mnyeti.
Katika hatua nyingine Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ameagiza kufanyika ukaguzi wa mashamba makubwa yaliyomilikishwa kwa wawekezaji kwenye mkoa wa Manyara ili kubaini mashamba yasiyoendelezwa.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza wakati wa uzinduzi wa ofisi ya ardhi ya mkoa uliofanyika mjini Babati mkoani Manyara. Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na kushoto kwa Waziri Lukuvi ni Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexzander Mnyeti.
Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexzader Mnyeti akizungumza wakati wa uzinduzi wa ofisi ya ardhi ya mkoa uliofanyika mjini Babati mkoani Manyara. Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Mary Makondo.
‘’Hatujatoa ardhi kwa ajili ya kuweka akiba, kazi ya ukaguzi mashamba ni ya kwenu hivyo myaangalie kama yameendelezwa, yana faida gani na yanalipa kodi’’ alisema Waziri Lukuvi.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akimkabidhi hati ya Ardhi mmoja wa wananchi wa mkoa wa Manyara ambaye ni askari polisi wakati wa uzinduzi ofisi ya ardhi mkoa wa Manyara. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
Na Munir Shemweta, WANMM Manyara
Mnyeti aliongeza kwa kusema kuwa, mkoa wa Manyara umekuwa na tatizo la wananchi kuvamia maeneo ya umma ambapo alisema uvamizi huo unachangiwa na kukosekana hati miliki za maeneo hayo na hivyo kutoa mwanya maeneo hayo kuvamiwa.
No comments:
Post a Comment