Wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC kutoka Tanzania wakifuatilia mkutano huo unaofanyika kwa njia ya video katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam |
Wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC kutoka Tanzania wakifuatilia mkutano huo unaofanyika kwa njia ya video katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amefungua Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC na kuzitaka nchi wanachama kushirikiana na kuchukua hatua zinazotekelezeka katika kukabiliana na madhara yatokanayo na mlipuko wa janga la Virusi vya Corona.
Amesema
changamoto zitokanazo na ugonjwa wa COVID
19 zipo wazi na zinazikabili nchi zote hivyo hazina budi kuungana na kutafuta
suluhisho la pamoja ili
kunusuru uchumi
na athari nyingine za kijamii.
Prof.
Kabudi amesema ili kupata suluhisho la
kudumu dhidi ya janga hilo Nchi za SADC ni
vyema zikashirikiana na Jumuiya nyingine za kikanda kama EAC na COMESA ili kuwa
na miongozo na viwango vya pamoja katika kuendesha shughuli za
usafirishaji wa binadamu,
bidhaa na huduma huku hatua za kujikinga
zikuichukuliwa.
Amesema
ni muhimu kwa nchi za SADC
kuzingatia miongozo ya wataalamu wa afya wakati
zikiendesha biashara na usafirishaji wa bidhaa na huduma ili kulinda uchumi na
kuondoa umasikini huku zikikabiliana na ueneaji wa janga la
Corona.
Mkutano wa Baraza la Mawaziri umejadili
utekelezaji wa maazimio ya Baraza la Mawaziri dhidi ya mapambano ya ugonjwa wa
COVID 19, kupokea taarifa ya Mkutano wa Kamati ya Wataalamu ya SADC ya
kusimamia utekelezaji wa Itifaki ya Afya ya SADC uliofanyika tarehe 05 Juni
2020 na upendeleo utakaotolewa na India kwa nchi za SADC zitakaponunua dawa,
vifaa kinga na vifaa tiba kwa ajili ya COVID 19.
Mkutano pia umepitia na kujadili
Mwongozo wa Kikanda wa Urazinishaji (harmonization)
na uwezeshaji wa shughuli za usafirishaji ndani ya SADC pamoja na masuala ya
uratibu, usimamizi na uangalizi wa usafirishaji kwa njia ya barabara katika
vituo vya kuingilia, ukaguzi dhidi ya Virusi vya Corona vinavyotambuliwa na
SADC na namna ya kuendeleza shughuli za biashara wakati huu wa janga la CORONA
ili kunusuru uchumi na kupunguza umasikini ndani ya jumuiya.
Mkutano huo umekutanisha Mawaziri wenye
dhamana ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Fedha na Mipango, Viwanda
na Biashara, Uchukuzi, Utalii na Afya kutoka nchi 16 wanachama wa SADC ambazo
ni Angola, Afrika Kusini, Botswana, Comoro, DRC, Eswatini, Lesotho, Malawi,
Mauritius, Msumbiji, Madagascar, Namibia, Visiwa vya Shelisheli, Zambia,
Zimbabwe na Mwenyekiti Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment